Sunday, April 29, 2018

SERIKALI YAINGILIA KATI MATIBABU YA MZEE MAJUTO, SASA KUPELEKWA INDIA, WADAU NAO WAJITOKEZA

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) jana Aprili 28, 2018 amemtembelea msanii nguli wa filamu Bw. Amri Athumani (Mzee Majuto) ambaye alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Tumaini, Dar es Salaam. 

Dkt. Mwakyembe akizungumza katika tukio hilo amesema Serikali imeamua kumpeleka Mzee Majuto nchini India kwa ajili kupata matibabu zaidi. 


"Kwa kuanzia tumeamua kumuhamishia Mzee Majuto katika hospitali ya Muhimbili ili kukamilisha maandalizi muhimu ya kiafya kabla ya safari ya kuelekea India", alisema Dkt. Mwakyembe.

Thursday, April 26, 2018

NENO LA MIZENGO PINDA KUHUSU WATU WAOFANYA VURUGU NCHINI

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Hii ilikua Juni 20, 2013, akizungumza katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu .

Mh. Pinda alisema “Ukifanya fujo umeambiwa usifanye hiki ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu maana hakuna namna nyingine maana wote lazima tukubaliane nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria sasa kama wewe umekaidi hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine maana tumechoka sasa”.

HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR


Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.


Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.

Wednesday, April 25, 2018

ALICHOSEMA KAMANDA WA POLISI DODOMA KUHUSU MAANDAMANO YA KESHO

Bofya hapo chini upate kusikiliza kauli ya kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto kuhusu maandamano ya kesho. Usisahau ku-subscribe, kulike na kucomment.

Thursday, April 19, 2018

BABU SEYA NA WANAE WATINGA BUNGENI LEO

Mwanamuziki nguli wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake ambao ni Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza, leo Aprili 19, 2018 wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma baada ya kualikwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile.

Babu Seya na familia yake, walishangiliwa na Bunge zima baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo.

Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.

MSUKUMA 'LEMA SASA HIVI KIDOGO AMEKUWA BINADAMU'

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma, amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, kupeleka bungeni muswada  kubadilisha sheria ili makosa ambayo hayastahili mtu kufungwa apewe adhabu ndogo ili kuondoa msongamano katika magereza.

Pia mbunge huyo aliwataka baadhi ya wabunge waache kupiga kelele bungeni juu ya matukio ya watu kupotea na kutekwa, badala yake waviache vyombo vya sheria na vya usalama vifanye kazi yake.

Hayo ameyasema Bungeni wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na Sheria jana, Aprili 18, 2018.

PICHA ZA HARUSI YA ALIKIBA ILIYOFANYIKA MOMBASA



 Baada ya ukimya na usiri wa muda mrefu kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi hatimae leo April 19, 2018 Ali kiba amefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum Mombasa nchini Kenya akiwa ameozeshwa na sheikh Mohammed Kagera.


Alikiba  amemuoa Amina Khalef Ahmed mkazi wa Mombasa ambapo ndipo sherehe za harusi hiyo zinafanyika hii leo huku sherehe nyingine kubwa ikitarajiwa kufanyika April 29, 2018 jijini Dar es Salaam.

Sunday, April 08, 2018

WADAU WA USAFIRI TABORA WATAKA MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO KUBANWA

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadaau wa Usafiri wamependekeza uanzishwaji wa matumizi ya vitabu (log book) kwa magari ya mizigo ili kudhibiti madereva kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na magari mengine kutokana na uchovu.

Tamko hilo limetolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitabu hivyo vitasaidia kuonyesha muda alitoka , mahali alitoka na kama amesafiri muda mrefu atalazimisha apumzike ili kuepusha ajali.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 08, 2018 YA DINI, MICHEZO NA HARDNEWS


TUCTA YAWALILIA WATUMISHI DARASA LA SABA YATAKA WARUDISHWE KAZINI

Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA ) jana Jumamosi Aprili 7, 2018 limetoa tamko lenye mambo saba, likiwemo la kupinga uamuzi wa Serikali kuwafuta kazi watumishi wake wenye elimu ya darasa la saba.

Akisoma tamko hilo mbele ya wajumbe wa baraza kuu la TUCTA katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika mkoani Morogoro mwenyekiti wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema uamuzi huo wa Serikali si sahihi na hivyo wametaka watumishi hao kurejeshwa kazini.

Amesema baraza limesikitishwa na uamuzi wa kuwaondoa kazini watumishi wa umma na taasisi zinazopokea ruzuku kutoka serikalini.

Saturday, April 07, 2018

MAGUFULI APIGA MARUFUKU ASKARI NA VIONGOZI KUFYEKA NA KUCHOMA MASHAMBA YA BANGI

Rais Magufuli amepiga marufuku askari wa jeshi la polisi, na viongozi wote wa serikali wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na makatibu wakuu kujishughulisha na kazi ya uchomaji na uteketezaji wa mashamba ya bangi na badala yake ameiagiza polisi kuwatumia wanakijiji kufanya kazi hiyo.
Hi
Ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari na kushuhudia maonesho ya utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.
“Kama bangi imelimwa karibu na kijiji, shika kijiji kizima, kuanzia wazee, wamama mpaka watoto ndiyo wakafyeke hilo shamba, maaskari wangu hawakuajiriwa kufyeka mashamba ya bangi.… Usiwatume maaskari wako kufyeka bangi, mwisho wataumwa nyoka mule, mmevaa sare nzuri halafu mnafyeka bangi, mnaaibisha jeshi”, alisema Rais Magufuli

Rais amesema wanaolima bangi wakikamatwa ndio wanaotakiwa kuzifyeka.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL 07, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS




ALIEVUMBUA MADINI YA TANZANITE APEWA MILLION 100 NA RAIS MAGUFULI

Bwana Jumanne Mhero Ngoma alivumbua dini la Tanzanite mwaka 1967.  
Jumanne Mhero Ngoma mvumbuzi wa madini ya Tanzanite.

Rais Dr. John Pombe Magufuli jana amezindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite huko Mererani mkoani Arusha ambapo katika uzinduzi huo alitambua uwepo wa mvumbuzi wa kwanza wa madini ya Tanzanite ambaye hakuwahi kutambuliwa na taifa.
Bwana Jumanne Mhero Ngoma alivumbua aina hiyo ya dini la Tanzanite mwaka 1967. Jumannne Ngoma ametambuliwa na Rais Magufuli na amemzawadia shujaa huyo milioni 100 kwa ajili ya kumsaidia kujikimu na matibabu baada ya mzee huyo kupooza sehemu ya mwili.

Rais Magufuli aliwahakikisha wachimbaji wadogo kwamba atawajengea 'mazingira ili kusudi wafaidi na Tanzanite zaidi'

Tanaznite ni madini ambayo ni ya kipekee kwa Tanzania haipatikani sehemu yeyote duniani. Mauzo ya Tanzanite duniani yanafikia dola za Marekani milioni 50. Tanzanite ni jiwe yenye miaka milioni mia 6 na iligundulika Mererani, Arsuha, kaskazini mwa Tanzania, mwaka 1967. Inasemekana kuwa na upekee hata ziadi ya alhmasi.

MAAJABU: JAMAA ATOLEWA MSWAKI TUMBONI

Mswaki 
Madaktari katika Hospitali Kuu ya Mkoa ya Pwani (CPGH) mjini Mombasa, Kenya wamefanikiwa kuutoa mswaki ambao ulikuwa umekwama tumboni mwa mwanamume mmoja kwa siku sita.

David Charo alikuwa akipiga mswaki alipoumeza kimakosa Jumapili wiki iliyopita apokuwa anajiandaa kwenda kazini Bamba, Kilifi. Kufikia jana, alikuwa ameanza kupata matatizo ya kupumua.
 Davis Charo 
Awali, madaktari walikuwa wamedokeza kwamba angehitaji kufanyiwa upasuaji kuutoa. Lakini Ijumaa asubuhi, madaktari wakiondozwa na Ramadhan Omar wamefanikiwa kuutoa mswaki huo bila kumfanyia upasuaji wa kawaida.

Badala yake, wamemfanyia upasuaji wa kutumia matundu madogo. Jumapili, Charo alipokuwa alipoumeza mswaki huo kimakosa, awali ulikwama ndani ya koo kabla ya kutumbukia ndani tumboni.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...