Chelsea
itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha
nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.
Manchester
City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich
huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old
Trafford.
Arsenal itaialika West Ham
,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku
Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.
Msimu huu utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapaau tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
Man City yatoa pauni milioni 35m kumnunua Raheem Sterling
Klabu ya Manchester City imeimarisha ombi la kumsajili mashambulizi machachari wa Liverpool Raheem Sterling.
Mabingwa hao wa mwaka wa 2014 wametoa pauni milioni 35 sawa na dola milioni 55 kusajili huduma za mshambulizi huyo.
The Reds walikataa ombi la kwanza la kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 wakisema thamani yake ni pauni milioni 50.
Kuwepo kwa mchezaji huyo raia wa Uingereza katika soko kumetokana na nia yake ya kuondoka Liverpool .
Sterling alijiunga na Liverpool mwaka wa 2010 akitokea QPR kwa mkataba utakaomalizika mwaka wa 2017.
Hata hivyo alizua mjadala baada ya kuzima pendekezo la nyongeza ya mshahara wake hadi pauni laki moja kwa wiki. Manchester
City inaaminika kuwa iko tayari kutoa marupurupu mengine
yatakayofikisha gharama yake hadi pauni milioni 40 japo wanalalamika
kuwa Liverpool imeongeza maradufu thamani yake ikifahamika kuwa wenyewe
hawakuwa hata wakimlipa pauni laki moja kwa juma. Kwa upande wake
kocha Brendan Rodgers anashikilia kukutu kuwa anamtarajia Sterling
kusalia Anfield hadi kandarasi yake itakapokatika.
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotangaza nia ya kugombea urais, sasa ni wazi wanapigana vikumbo kila kona ya nchi.
Hatua hiyo inatokana na kila mtangaza nia kwa nyakati tofauti kutoa kauli nzito.
Wapo makada ambao kauli zao zinaonyesha wazi kuwa kuna mgongano ndani ya
CCM, huku wengine wakitangaza nini watakifanya endapo watateuliwa
kuongoza nchi.
MEMBE: SINA UNDUGU NA JK
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hana undugu na Rais Jakaya Kikwete.
Membe ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, alikanusha undugu wake na Rais
Kikwete mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuwania urais kupitia CCM. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Watoto
walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa
mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo
zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto
wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la
kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto
duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel
Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa
hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto
kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema
haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa
za kupunguza makali.
Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina
viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye
chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina
ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa
matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa
maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa
Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha
upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono
mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi ya kumiliki mpira na kupiga pasi
Kocha wa Yanga (mwenye jezi ya njano) akifuatilia mazoezi.
van Pluijm akitoa mazoezi kwa mchezaji wa mpaya kigeni wakati wa mazoezi. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kwa wale wanaojiuliza ni lini Arsenal watatoa jezi zao mpya za Puma kwa ajili ya msimu wa 2015/2016, jibu hili hapa.
Jezi za nyumbani za Arsenal
zitakazotumika msimu ujao wa 2015/2016 zimevuja….hivyo mashabiki wa
London na duniani kote wajiandae kupata mzigo mpya.
Cheki uzi mpya wa nyumbani wa Arsenal chini;
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wakuu
wa magereza Nchini Afrika Kuisini wamesema kuwa Oscar Pistorius,
ataachiliwa kutoka gerezani mwezi Agosti mwaka huu miezi kumi baadaye,
ili atumikie kifungo cha nje, cha hukumu aliyopewa ya miaka mitano.
Bingwa
huyo wa nishani ya dhahabu katika mbio za Olimpiki, alikutwa na hatia
ya kumpiga risasi bila ya kukusudia na kumuuwa mpenziwe, Reeva
Steen-kamp,
na kumuuwa mwana mitindo huyo.
Mahakama kuu
Nchini Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka huu, itasikiliza rufaa ya
waendesha mashtaka ya kujaribu kupunguza makali ya hukumu iliyotolewa
dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Dar es Salaam. Baada ya wiki nzima ya makada wa
CCM kutangaza nia na hatimaye kuchukua fomu za kugombea urais, wapinzani
ndio wanaonekana kunufaika zaidi kutokana na wengi kutumia hotuba zao
kuelezea udhaifu wa kila mmoja.
CCM imepanga mwezi mzima, kuanzia
Juni 3 hadi Julai 2 kuwa ni muda wa makada wake kuchukua na kurudisha
fomu kabla ya vikao vya juu vya chama hicho kukutana kuanzia Julai 12
kuchuja wagombea na baadaye kumpata mmoja atakayesimama kwenye Uchaguzi
Mkuu kupambana na wa vyama vingine.
Tayari makada 15
wameshachukua fomu na wengine wanaendelea kuchukua, huku waliochukua
wakiwa wameshaanza kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini 30 kila mkoa ili
kupata idadi ya wadhamini 450. Wanatakiwa kupata wadhamini kwenye mikoa
15, kumi ya Bara na mitano ya Zanzibar. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.<
Gari ilikuwa imebeba wasaidizi wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM,
Makongoro Nyerere likiwa limeanguka wilayani Kasulu, Kigoma jana wakati
likiwa kwenye msafara kwa ajili ya kusaka wadhamini. Picha na Blog ya
Michuzi
Akitoa taarifa za ajali hiyo, kamanda wa polisi wa
Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina
ya Toyota Land Cruiser lililokuwa linaendeshwa na Julius Kambarage
Nyerere ambalo lilipinduka saa 4:30 lilipofika eneo la Mwilamvya na
kujeruhi watu watano.
Nunua gari kwa bei rahisi bofyahapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SERIKALI imekiri kuruhusu uanzishwaji wa kiwanda cha kusindika nyama ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
Imekiri hivyo baada ya Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohamed (CUF),
kuibua hoja hiyo juzi (ijumaa) jioni wakati wa kupitisha makadirio ya bajeti ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Katika hoja yake, alitaka kujua juhudi zilizofanywa na Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), kukagua viwanda vya usindikaji wa
chakula ikiwa ni pamoja na kiwanda hicho. Nunua gari kwa bei rahisi bofyahapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Barcelona
walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa
Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa
katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Hata hivyo Alvaro Morata
alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa
Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya
gusa ni guse kati yake na Messy.
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.
Mechi
hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi
Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Takriban
watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo
kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo
uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo
walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha
raia wengi bila makaazi pamoja na stima.
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Mlipuko huo ulitokea hapo jana
wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha
mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.
Mshambuliaji
wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya
Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana
wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani
mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.
Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi. Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki.
Sterling
amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool
akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa
kushinda mataji. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Serena
Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French
Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na
kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu
kucheza fainali za mwaka huu.
Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi. Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.
Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa. Mapema
katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa
nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika
fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi
cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Hofu
kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa
kwamba kundi la wapiganaji wa Al shabaab Limeviteka vijiji kadhaa katika
mpaka wa Kenya na somalia.
Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu
kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea
ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo
hilo. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Mji huo ulikuwa umeshambuliwa saa za alfajiri siku ya jumanne na washukiwa wa kundi la Boko haram .
Saa
chache baadaye ,mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua katika soko la
kuuza ngombe la Gamboru ndani ya mji huo kulingana na walioshuhudia.
Wakati
wa kuapishwa kwake rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kuwa
anayahamisha makao makuu ya kijeshi katika vita dhidi ya wapiganaji hao
kutoka mji mkuu wa Abuja hadi Maiduguri. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.