Thursday, April 09, 2015

WABUNGE 50 KUHAMIA ACT...!!!

 
Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wahariri wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, yaliyopo Tabata Relini, Dar es Salaam jana.

Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa mwezi uliopita.
Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'NATAZAMWA NA CCM KILA KONA' LOWASSA

 
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema anashindwa kujitokeza kuzungumzia au kufanya mambo yanayohusiana na urais kwa kuwa Kamati ya Maadili ya CCM inamfuatilia kwa karibu.
Alisema hayo jana alipoulizwa kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita akiwa Marekani ambako alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10.
Kikwete alisema: “Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa pamoja na furaha ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”
Kauli ya Lowassa inakuja ikiwa ni siku chache baada ya makada wengine wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM kueleza maoni yao juu ya kauli hiyo ya Rais.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameshalieleza gazeti hili kuwa kauli hiyo inampa hamasa kwa nia yake ya kutaka kuwania urais na kwamba alitangaza nia hiyo huku akifahamu kwa asilimia 100 uzito wa jambo hilo akisema kufahamu changamoto hizo ndiyo moja ya vitu vilivyomsukuma kuchukua uamuzi huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRILI 09, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC01106


DSC01107

DSC01108

DSC01109

DSC01110 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

AUAWA KWA KUPELEKA WAGANGA KIJIJINI

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamwela.

MZEE mwenye umri wa miaka 68, Celestine Mushi, mkazi wa kata ya Motamburu wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, ameuawa na wananchi wanaotajwa kukasirishwa na kitendo chake cha kupeleka waganga wa jadi kijijini kwa lengo la kuifanyia zindiko nyumba yake.

Mushi anadaiwa kuwatoa waganga hao wawili jijini Dar es Salaam na kuwapeleka Rombo kwa kazi hiyo maalumu.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamwela aliyesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 2.30 usiku nyumbani kwa Mushi katika kitongoji cha Mbomai Juu, wakati waganga hao wakiendelea na zindiko lao.
Kamwela aliwataja wanaodhaniwa ni waganga wa jadi kuwa ni Ashraf Mjengwa (22) na Peter Mmaka (25), wote wakazi wa Magomeni, Dar es Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

HII NDIO YANGA: YAIFUNZA COASTAL UNION ADABU, YAIFUNGA 8 - 0....!!!

Kiungo wa Yanga, Salum Telela, akimiliki mpira mbele ya
wachezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga imeshinda 8-0.

(Picha na Francis Dande).
Simon Msuva akishangilia bao aliloifungia timu yake.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CHRISTIANO RONALDO AFUNGA GOLI LA 300

cr7

CRISTIANO RONALDO, jana alifunga goli katika ushindi wa magoli 2-0 wa Real Madrid dhidi ya Rayo Vallecano.
Kwa kufunga kwake jana, mchezaji huyo amefikisha magoli 300 tokea aanze kuichezea Real Madrid, na amekuwa mchezaji wa tatu kwenye historia ya timu hiyo kufikisha idadi hiyo ya magoli baada ya wakongwe waliomtangulia kina Alfredo Di Stefano na Raul Gonzalez.
Sasa Cristiano bado magoli manane amfikie Di Stefano na 23 amfikie Raul.
Raul ndie mfungaji bora wa kihistoria kwenye timu hiyo akiwa amefunga magoli 323 katika mechi 741, wakati marehemu Di Stefano anashika nafasi ya pili akiwa amefunga magoli 308 katika mechi 396.
Cristiano Ronaldo amefunga magoli 300 katika mechi 288. Hivyo wastani wake ni mzuri kuliko wachezaji hao wote wawili akiwa na wastani wa kufunga goli moja katika kila mechi na amefunga magoli mengi kuliko idadi ya jumla ya mechi alizocheza.
Di Stefano naye wastani wake ni mzuri kuliko Raul. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Taifa Stars ya Tanzania
Ratiba ya michuano ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika imetolewa leo na CAF huku Tanzania ikiwa kundi G pamoja na nchi za Nigeria, Misri na Chad.
Makundi ni kama ifuatavyo:

Kundi A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti.
Kundi B: Congo DRC, Angola, Jamhuri ya Kati, Madagascar.
Kundi C: Mali, Guinea ya Ikweta, Benin, Sudan Kusini.
Kundi D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoro.
Kundi E: Zambia, Kenya, Congo Brazzaville, Guinea Bissau.
Kundi F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome.
Kundi H: Ghana, Msumbiji, Rwanda, Mauritius.
Kundi I: Ivory Coast, Sudan, Sierra Leone, Gabon.
Kundi J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Shelisheli.
Kundi K: Senegal, Niger, Namibia, Burundi.
Kundi L. Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland.
Kundi M. Cameroon, Afrika ya Kusini, Gambia, Mauritania.

Fainali zake zitafanyika Gabon 2017 na droo imefanyika Misri, makao makuu ya CAF. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, April 02, 2015

MWIGULU KUFUTA MAADHIMISHO MBALIMBALI YA KITAIFA...!!!

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba juzi alijikuta akitamka kuwa anakusudia kufuta maadhimisho mbalimbali ya kitaifa yanayotumika kama kichaka cha kutafuna fedha za Serikali baada ya wabunge  wa upinzani kuitoa jasho Serikali wakati wa kupitisha Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2015.
Mwigulu alitoa kauli hiyo pale alipoingilia kati mjadala huo, akiponda kitendo cha watumishi wa Serikali kutumia magari na fedha lukuki katika wiki za kuadhimisha kumbukumbu mbalimbali za kitaifa.
Kilichoibua mjadala huo ni suala la uanzishwaji wa Mfuko wa Vijana na maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo imepangwa Oktoba kila mwaka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRILI 02, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TRENI DAR - KIGOMA KAMA NDEGE...!!!

 
 Mwonekano wa ndani ya treni ya kisasa ya abiria ya Kampuni ya TRL iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan Mwinjaka, Dar es Salaam jana.

Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

RAIA WA YEMEN WAKIMBILIA SOMALIA

Raia wa Yemen wakikatika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo
Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia, Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao.

Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.

Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BUHARI AAHIDI KUTOKOMEZA BOKO HARAM NIGERIA

Muhammadu Buhari, Rais mteule wa Nigeria
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa linalokabili nchi.

Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.

 "Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."

Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.

"Tumebaini matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe. 

Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."

 Anasema rais huyo mteule wa Nigeria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Friday, March 27, 2015

GWAJIMA ASAKWA NA POLISI KWA KUMKASHIFU KARDINALI PENGO

GWAJIMA
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kujisalimisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.


Hatua hiyo ya polisi imekuja baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko, ambapo inadaiwa Mchungaji Gwajima alitoa lugha ya kashfa dhidi ya Kardinali Pengo ambaye alipinga tamko lililotolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) la kuipigia kura ya Hapana Katiba Inayopendekezwa.


Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Suleiman Kova, imemtaka Mchungaji Gwajima kujisalimisha haraka katika Kituo cha Polisi cha Kati kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

JK ATEUA WABUNGE WAPYA

rais-kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Dk. Grace Puja na Innocent Sebba kuwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, ilisema uteuzi huo unatokana na mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e).


Alisema ibara hiyo, inampa mamlaka rais ya kuteua wabunge wasiozidi 10 na kwamba uteuzi wa wabunge hao ulianza Machi 20, mwaka huu. Kibanga alisema kuteuliwa kwao kumekamilisha idadi ya wabunge ambao rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kikatiba.


Alisema awali Rais Kikwete aliwateua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Asha Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria), Saada Salum Mkuya (Waziri wa Fedha) na Janeth Mbene (Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara).


Wengine walioteuliwa awali ni Profesa Sospeter Muhongo, Shamsi Vuai Nahodha, Zakhia Meghji na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 27, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...