Mji wa Moshi, Tanzania
Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe hasa ya viroba, ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe hasa ya viroba, ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa
ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive
ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa
kati ya miaka 15 hadi 24.
Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa
Matumizi ya Pombe kwa vijana katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza,
Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa unywaji
wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.