Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia
askari wawili wa magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa
pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo
alisema askari hao walikamatwa juzi saa tisa mchana katika Mtaa wa Old
Maswa, Kata ya Nyakabindi, wilayani Bariadi.
Alisema askari hao walifika kwenye kibanda cha
M-pesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa,
Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki aina ya Sunlg kwa lengo la
kuweka fedha hizo katika simu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Alisema baada ya mwalimu huyo kupokea noti 10
zenye thamani ya Sh100,000 alizitilia shaka na kuamua kuzikagua zaidi
ndipo alipogundua kuwa siyo fedha halali.
Mkumbo alisema mwalimu huyo baada ya kugundua hilo
aliomba msaada wa kukamatwa kwa askari hao. Alisema majirani walipofika
walihoji, ndipo mmoja wao alipotoa kitambulisho kuwa yeye ni askari na
mwingine kujitambulisha kuwa ni dereva bodaboda.
Alibainisha kuwa baada ya wananchi kuambiwa hivyo
waliwatilia shaka zaidi na kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Bariadi
na kisha kukamatwa.
Mkumbo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari
mwenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Simiyu, na mwenye namba B.6499 WDR Edmund
Masaga (28) wa Magereza wilayani Bariadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa, baada ya askari hao
kukamatwa mmoja wao PC Selemani alipopekuliwa katika mfuko wa suruali
yake, alikutwa na noti nyingine za bandia za Sh100,000.
Mbali na hilo Mkumbo alisema askari huyo
alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na sare za JWTZ ambazo ni kaptula
nne, fulana mbili, kombati moja pamoja na kitambaa.
Alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini
mtandao mzima wa usambazaji wa noti bandia ndani ya mkoa na kwamba baada
ya uchunguzi kukamilika askari hao watachuliwa hatua za kinidhamu
pamoja na kisheria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment