Tuesday, August 12, 2014

MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA APIGWA, ALAZWA...!!!




Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Kundi la 201, Thomas Mgoli akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma, jana.

Dodoma. Mjumbe wa Bunge la Katiba, kutoka Kundi la 201, Thomas Mgoli amelazwa katika Hospitali ya Dodoma baada ya kupigwa na watu aliodai kuwa ni wafuasi wa Chadema.

Mjumbe huyo alidai kuwa kati ya watu waliompiga yumo mtumishi wa Bunge na ameshamshtaki kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta huku akisema akimuona anaweza kumtambua.

Mgoli ambaye anatokea Chama cha Alliance Democratic Change (ADC), alisema kuwa alipokea kipigo kikubwa juzi katika maeneo ya Area A karibu na Shule ya Msingi Chamwino A.

Akiwa katika wodi ya daraja la kwanza hospitalini hapo, alieleza kuwa chanzo cha mapigano hayo ni mabishano waliyokuwa nayo na vijana wanne mmoja aliyemtaja kwa jina la Vampaya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UCHAWI WASHIKA KASI, ALBINO WAANGAMIA


Vifaa vinavyodaiwa kuwa ni vya kishirikina

Jana tulichapisha habari za kusikitisha kutoka wilayani Urambo, mkoani Tabora kuhusu Pendo Sengerema, msichana wa miaka 15 mwenye ulemavu wa ngozi (albino), ambaye watu wenye imani za kishirikina wamemkata mkono wa kulia na kuondoka nao.

Huu ni uthibitisho kwamba Watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi wanaendelea kupoteza maisha au kupata vilema vya kudumu kutokana na sehemu ya jamii yetu kukumbwa na imani potofu za kishirikina kwamba viungo vya watu hao vinaleta utajiri mkubwa na wa haraka.

Hatuna maneno stahiki ya kuelezea tukio hilo, isipokuwa tu kusema kwamba linasikitisha na kufadhaisha.

Kama msichana mdogo hivyo anaweza kufanyiwa ukatili wa kiwango kikubwa kiasi cha kupoteza kiungo muhimu kama mkono, ambao ungekuwa tegemeo kubwa kwake katika kufanya shughuli za kumwezesha kujitegemea kimaisha, basi tukubaliane kwamba ushirikina umeigeuza jamii yetu kuwa sawa na jamii ya wanyamapori.

Ni imani hizo potofu ambazo zimeikumba jamii yetu tangu mwaka 2000 wakati nchi yetu ilipoanza kushuhudia mauaji ya kinyama dhidi ya ndugu zetu hao wenye ulemavu wa ngozi.

Miaka 14 imepita sasa na vitendo hivyo vinaendelea. Bahati mbaya Serikali imeshindwa kuonyesha dhamira ya kutokomeza uovu huo, bali imebakia kutoa machozi ya mamba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HIKI NDICHO KIOJA ALICHOZUA MTUHUMIWA MAHAKAMANI


Rwanda imekuwa ikiendedesha harakati za upatanishi na pia kuwakumbuka waliokufa katika mauaji hayo
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Emmanuel Mbarushimana amekataa uendeshwaji wa kesi yake na mahakama ya Kigali kwa kutoa pingamizi kwamba hana haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.
Mshukiwa huyo alikabidhiwa Rwanda na nchi ya Denmark mapema mwezi wa saba mwaka huu ili kujibu mashitaka ya kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Mushukiwa huyo Bwana Emmanuel Mbarushimana amesema kesi yake haiwezi kusikizwa hadi pale atakapopata haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka. Hoja yake ilikuwa kwamba ni lazima na yeye aruhusiwe kukaa badala ya kusimama wakati kesi yake ikisikilizwa na wakati huo huo mwendesha mashitaka asimame badala ya kukaa kama ilivyozoeleka.
Aidha, amesema kuwa hajafurahia utaratibu unaotumiwa wa kuingia katika chumba cha mahakama ambapo mwendesha mashitaka na majaji wanaingia kwa kutumia mlango mmoja kinyume na mushitakiwa. 
Mwendesha mashitaka amemshitaki kwa kushiriki katika mauaji dhidi ya watutsi yaliyotokea katika maeneo mbali mbali katika mkoa wa zamani wa Butare kusini mwa Rwanda. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MKUU WA POLISI LIBYA AUAWA


Kanali Muhammad Suwaysi aliteuliwa kama mkuu wa polisi mjini Tripoli mwaka 2012
Mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Libya Tripoli, ameuawa na watu wasiojulikana.
Kanali Muhammad Suwaysi alipigwa risasi, alipokuwa anaondoka kwenye mkutano katika eneo la Tajoura , mtaa ulio mashariki mwa mji mkuu Tripoli.
Wenzake wawili walitekwa nyara kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ndani.
Libya imekumbwa na vurugu zinazosemekana kusababishwa na wapiganaji wa kiisilamu, ambao walisababisha harakati za kumuondoa mamlakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka Tripoli. Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuondolewa mamlakani kwa Gadaffi, jeshi la polisi nchini Libya linasemekana kuwa dhaifu,
ikilinganishwa na wapiganaji wanaodhibiti sehemu kubwa za nchi hiyo.

Wapiganaji wa kiisilamu ambao wamekuwa wakizua vurugu nchini Libya
Afisa huyo aliuawa wakati alipokuwa anatoka katika mkutano na maafisa wa mtaa wa Tajoura. Maafisa wengine wawili waliokuwa naye, walitii masharti ya washambuliaji na kuondoka kwenye gari lao huku wakitekwa nyara.
Mamia ya watu wamefariki katika miezi ya Julai na Agosti katika kile kinachoonekana kuwa kukithiri kwa vurugu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ANGALIA PICHA ZA MELI ALIYOKODI TAJIRI BILL GATES KWA TSHS BILLION 8 KWA WIKI...!!!

article-2719109-2057AB6700000578-788_634x422 Katika meli hiyo helikopta zinamchukua Gates kumpeleke nchi kavu kucheza golf na kumrudisha Ni tajiri namba moja duniani mwenye utajiri unaofikia dola bilioni 79.2 hivyo kutumia shilingi bilioni nane kwa wiki si kitu kinachoweza kumpunguzia chochote Bill Gates. Na ndio maana Bill Gates yupo mapumzikoni ambayo tunategemea kwa mtu tajiri zaidi duniani ayafanye. 
article-2719109-2057BE7A00000578-683_634x422 

Tajiri huyo amekodi meli binafsi maarufu yacht ambayo analipa dola milioni 5 (zaidi ya shilingi bilioni 8) kwa wiki.  Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BUNGE MAALUMU LA KATIBA MTEGONI TENA LEO

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Samuel Sitta. PICHA |MAKTABA

Mjadala kuhusu masuala ya Muungano unatarajiwa kurejea upya katika kamati za Bunge Maalumu leo, wakati zitakapoanza kujadili sura za saba, nane, kumi na moja, 18 na 15 za Rasimu ya Katiba.
Kamati zimepewa siku sita kujadili sura hizo tano ambazo zina jumla ya ibara 79, huku miongoni mwake zikigusa masuala mengi ambayo msingi wake umejengwa juu ya mfumo wa serikali tatu.
Miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na baraza la mawaziri, tume ya kusimamia na kuratibu uhusiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika (Tanganyika na Zanzibar), Sekretarieti ya Tume ya Uhusiano na Uratibu, Masuala yanayohusu Benki Kuu na Fedha pamoja na uteuzi wa watumishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Suala la aina ya muungano lilianza kujadiliwa katika sura ya kwanza na ya sita katika awamu ya kwanza ya Bunge iliyomalizika mwishoni mwa Aprili mwaka huu na kuzua mvutano mkali ambao hatimaye ulisababisha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu kususia mchakato huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UNYAMA HUU: BINTI WA KAZI AMWAGIWA UJI NA MKE WA BOSI WAKE KISA WIVU WA MAPENZI...!!!


MSICHANA mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka), amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri yake na kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Singida, wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian amefahamisha kuwa binti huyo amejeruhiwa sehemu za sikio la upande wa kulia na mgongoni, ambapo amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoyapata hospitalini hapo.
Akizungumza Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa jina la Pendo, amesema majeraha ya moto yapo katika sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.
Pendo amesema kuwa tukio hilo limetokea Jumamosi Agosti 9, 2014 saa nane mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina la, Charles Kamnde.

Amesema akiwa anaendelea na kazi zake za kuuza bidhaa mbalimbali dukani hapo, ghafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto na kuwa alimmwagia usoni ambapo baada ya kumwagiwa uji huo alitaka kujiokoa ili usimmwagikie usoni na ndipo ulimuunguza kwenye sikio la kulia na mgongoni na kuwa baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa kisu kutaka kumchoma kifuani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 12, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BBC YAZINDUA OFISI MPYA DAR

Wafanyakazi wa BBC wakiwa kazini kupeperusha matangazo ya Dira ya Dunia redio
Idhaa ya kiswahili ya BBC imezindua rasmi studio zake mjini Dar es Salaam kwa mbwembwe na haiba kuu.
Uzinduzi huo ni matokeo ya mkakati na uwekezaji wa miaka mingi wa shirika la BBC duniani kuhakikisha kuwa matangazo yake yanawafikia wasikilizaji katika hali ya ubora wa hali ya juu na ya kisasa zaidi.
Katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika ofisi hizo hizo mpya zilizoko eneo la Mikocheni, mkuu wa kitengo cha uandishi wa habari katika BBC, Nicki Clarke, ameshukuru serikali ya Tanzania, kwa kuwaruhusu kujenga studio hizo za kisasa zitakazoinua tasnia ya habari nchini humo na uhuru wa habari kwa ujumla.
Naye mkuu wa ofizi ya Dar es Salaam, Hassan Mhelela mbali na kuwataka wafanyakazi wa BBC Tanzania, kuzidi kuonyesha ushirikiano pamoja na utendaji kazi wa pamoja, pia ametangaza kuanishwa rasmi kwa ushirikiano kati ya BBC na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari.
Eric David Nampesya akizipa taabu Tumba kwenye sherehe ya ufunguzi wa ofisi za BBC Dar es Salaam
Ushirikiano huo amesema kuwa unalenga kusaidia kutoa mafunzo kwa wandishi wa habari chipukizi walioko mafunzoni katika chuo hicho, ambao kwa nyakati tofauti, watakuwa wakijiunga na BBC ili kupata mafunzo katika uandaaji vipindi vya redio na televisheni pamoja na utangazaji.
Kwa upande wa BBC, kuanzishwa kwa ofisi hii, yenye studio za kisasa kabisa za redio na televisheni mbali na kuongeza ubora wa vipindi lakini pia kutawezesha matangazo ya redio na televisheni kufanyika moja kwa moja kutokea Dar es Salaam.
Na kuanzia sasa matangazo ya Amka na BBC yatakuwa yakiandaliwa Dar es Salaam.
Itakumbukwa kuwa Tanzania mbali na kuwa na wasikilizaji wengi wa idhaa ya kiswahili ya BBC, lakini pia ndiko kunakozungumzwa zaidi lugha ya kiswahili.
Tanzania pia ina rekodi ambapo mtangazaji wa kwanza au sauti ya kwanza iliyosikika mwaka 1957, ilikuwa ya mtanzania Oscar Kambona ambapo alikuwa mwanafunzi mjini London. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, August 11, 2014

BUNGE LAKODI VIPAZA SAUTI KWA SH. 8.9 MILLION KILA SIKU....!!!


Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16  ambazo kamati zitakutana, gharama hizo zitafikia Sh142.56


Wakati kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la Maalumu la Katiba linagharimu fedha nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni kukodi vipaza sauti kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha kukodiwa kwa vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12 na kwamba kila gharama ya chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani (Dola moja ni wastani wa Sh1,650).

Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16  ambazo kamati zitakutana, gharama hizo zitafikia Sh142.56. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MREMA AWATAMBIA UKAWA, AMUONYA MBATIA

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP)

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) amedai kitendo cha yeye kubaki kwenye Bunge Maalumu la Katiba kumetumiwa vibaya na wahasimu wake wa kisiasa jimboni kwake.

“Ukawa na ubunge wa Vunjo vimegeuka propaganda chafu dhidi yangu. Wamediriki kuwaambia wananchi wangu kuwa nimeahidi kuwaachia jimbo langu,” alisema.
Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa taifa wa TLP, alitoa kauli hiyo jana jimboni kwake katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kuelezea kwa nini hakuwaunga mkono Ukawa.
Mrema alisema malengo ya Ukawa siyo katiba bali Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na ndiyo maana tangu waliposusia Bunge agenda yao imebadilika na kuwa muungano wa kuelekea uchaguzi 2015.
“Mimi nimeamua kubaki bungeni kwa ajili ya masilahi mapana ya wananchi wa jimbo langu la Vunjo na Watanzania kwa jumla. Sitishwi na Ukawa na nitatetea kiti changu 2015,” alisisitiza.
Mrema alitumia mkutano huo kumshambulia mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye ni James Mbatia kutokana na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo mwakani. Kwa mujibu wa Mrema, ndiye Mtanzania pekee mwenye sifa na aliweza kugombea ubunge katika majimbo matatu tofauti na kushinda.
“Mimi ni Mtanzania pekee ambaye nimewahi kuwa mbunge wa majimbo matatu tofauti ya Moshi Vijijini, Temeke na Vunjo. Sifa hizo hazipo kwa wengine,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ZESCO YATIBUA SHEREHE YA SIMBA DAY...!!!

Mabao matatu yaliyofungwa na Jackson Mwanza, Clatons Chama na Winston Kalenga, yamesababisha siku ya Simba ‘Simba Day’ kuwa chungu baada ya Zesco kuizamisha miamba hiyo kwa mabao 3-0.
Safu ya ulinzi ya Simba iliyoshindwa kuelewana iliizawadia Zesco ya Zambia mabao matatu, wakati wa mchezo huo wa kuadhimisha siku muhimu ya klabu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ikiwa inatumia mchezo huo kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wake wapya iliyowasajili, Simba iliendeleza rekodi yao ya kutoshinda katika mchezo wa Simba Day tangu kuanza kuiadhimisha siku hiyo.
Ukihudhuriwa na mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, ambaye aliwataka Simba kucheza kimataifa zaidi, kikosi hicho cha kocha Zdravko Logarusic kilijikuta katika siku mbaya msimu huu.
Simba ilianza kuruhusu bao la kwanza dakika ya 14, wakati Mwanza akiunganisha kwa kichwa krosi safi kutoka wingi ya kushoto. Mabeki wa kati wa Simba, Donaldi Mosoti na Joseph Owino walionekana kushindwa kujua nani wa kumkaba na kumuacha Mwanza akiruka peke yake.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Paul Kiongera alishirikiana vizuri na Amissi Tambwe, lakini hawakuwa makini kwani Tambwe alikosa nafasi kadhaa za wazi.
Nafasi ya kwanza kwa Tambwe ilikuwa dakika ya saba, wakati shuti la Kiongera lilipopanguliwa na kipa wa Zesco, lakini Tambwe alishindwa kuumalizia mpira huo vizuri.
Simba ilikuwa na kipindi cha pili kibaya zaidi, kwani mabeki wake wa kati walisababisha penalti kwa kumwangusha Chama aliyekuwa anakwenda kufunga na mshambuliaji huyo kuukwamisha mkwaju huo wavuni.
Dakika tano za nyongeza zilikuwa mbaya zaidi kwa Simba, ambapo shambulizi la kushtukiza lilizaa bao baada ya mabeki wa Simba kwa mara nyingine wakishindwa kuondoa krosi ndogo ambayo ilimaliziwa kiufundi na Kalenga. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 11, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MADAKTARI WATOA TAHADHARI YA EBOLA

madaktari wakitoa huduma dhidi ya Ebola
Shirika la Madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontiers wametahadharisha kuhusu wizara ya afya nchini Liberia kuzidiwa nguvu na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi.
Mratibu wa mambo ya dharura wa shirika hilo nchini humo amesema serikali haikutilia maanani vya kutosha madhara ambgayo yangesababishwa na ugonjwa huo na kwamba mfumo wa afya kwa sasa upo katika hali ya kushindwa.
Nchini Siera Lione, majeshi yameweka vizuizi katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.
Raia wa Uingereza ambaye ni mfanya biashara katika eneo la Kanema kaskazini mwa nchini hiyo anaeleza madhara wanayopata kutokana vizuizi vya zilivyowekwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI KUENDELEA KUISHAMBULIA IRAQ

Wapiganaji wa Kurdi
Marekani imeendeleza mashambulizi ya anga kaskazini mwa Iraq kwa lengo la kuwasaidia Wakrud katika mji wa Erbil dhidi ya wapiganaji wa kiislam wa kundi la Jihad.
Wapiganaji wa kundi hilo la Kiislam hivi karibuni wameendelea kuimarisha ngome yao katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuiteka ngome kubwa ya Iraq katika mji wa Mosul. Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Sunni waliokuwa wamejificha katika milima iliyo eneo la wakimbizi la Yazid.
Hata hivyo Uingereza imesema inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Wakurdi ambapo Ofisa wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Alistair Burt anasema nchi hiyo inaweza kusaidia eshi la Wakurdi.
Wakati huo huo vikosi vya majeshi ya Iraq na vyombo vya usalama vimesambaa katika katika maeneo mbalimbali ya mji wa Baghdad huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufuatia kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo ya Iraq Nouri al-Maliki inayodaiwa kuwa ni ya utovu wa nidhamu kwa Rais wa nchi hiyo Fuad Masum.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri hiyo amevunja katiba mara mbili,mara ya kwanza ni pale alipojiongezea muda wa kukaa madarakani,wakati alistahili kutangaza kuvunja bunge. Hata hivyo kipindi chake kiliisha august saba alhamisi iliyopopita.
Hata hivyo papa Francis ameelezea gogoro wa Ira kwamba msingi wake mkubwa ni masuala ya tofauti za kidini. Melfu ya watu nchini Iraq wamekuwa wakilazimishwa na wapiganaji wa kiislam ambao wameimarisha ngome ao kaskazini mwa nchi hiyo.Katika ujumbe wake wa jumapili ,papa Francis ametoa wito kwa dunia kukomesha uhalifu huo unaoendelea nchini Iraq. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...