Tuesday, August 12, 2014

MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA APIGWA, ALAZWA...!!!




Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Kundi la 201, Thomas Mgoli akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma, jana.

Dodoma. Mjumbe wa Bunge la Katiba, kutoka Kundi la 201, Thomas Mgoli amelazwa katika Hospitali ya Dodoma baada ya kupigwa na watu aliodai kuwa ni wafuasi wa Chadema.

Mjumbe huyo alidai kuwa kati ya watu waliompiga yumo mtumishi wa Bunge na ameshamshtaki kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta huku akisema akimuona anaweza kumtambua.

Mgoli ambaye anatokea Chama cha Alliance Democratic Change (ADC), alisema kuwa alipokea kipigo kikubwa juzi katika maeneo ya Area A karibu na Shule ya Msingi Chamwino A.

Akiwa katika wodi ya daraja la kwanza hospitalini hapo, alieleza kuwa chanzo cha mapigano hayo ni mabishano waliyokuwa nayo na vijana wanne mmoja aliyemtaja kwa jina la Vampaya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

“Nimepanga nyumba katika eneo hilo, juzi (jana) saa mbili usiku nilitoka kwenda grocery (duka la vinywaji) kuchukua kinywaji ili nirudi nyumbani. Niliwakuta vijana hao ambao wakati wote tumekuwa tukitaniana,” alisema na kuongeza:

“Mara baada ya kufika wakaniuliza katika mchango wangu bungeni ni kwa nini nilimtukana Profesa Kabudi (Palamagamba), nikajaribu kueleza kilichotokea bungeni na kuhusu mchango wangu, basi wakaanza kunipiga ngumi nilipotaka kukimbia nikapigwa na kipande cha tofali.”

Mjumbe huyo alidai kuwa ni kawaida kukutana na vijana hao katika duka hilo na kupata vinywaji huku wakitaniana.

Sitta alifika hospitalini hapo kumjulia hali na alielezwa mkasa mzima.

Baadaye Sitta aliwaonya wajumbe wa Bunge lake kuwa mijadala ya Katiba inapaswa kufanyika ndani ya Bunge na siyo nje huku akiwasihi Watanzania kuwa wavumilivu ili Katiba bora ipatikane.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Mzee Nasoro alisema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri na kwamba alikuwa na maumivu ya juu katika maeneo ya usoni na mdomoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema tukio lilitokea wakati mjumbe huyo alipokuwa akipata kinywaji katika duka hilo ndipo kukatokea mabishano yaliyosababisha kupigwa kwake.

Alisema polisi wanaendelea kuwahoji watu watatu ili kupata ukweli wa jambo hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...