Monday, January 13, 2014

HODI TENA...!!! OPERESHENI TOKOMEZA YA PILI KUANZA KARIBUNI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
WAKATI hatua zaidi zikisubiriwa kuchukuliwa kwa watendaji waliohusika na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa Operesheni Tokomeza, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza kuanza kwa awamu ya pili ya Operesheni hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema wakati wowote Rais Kikwete atatangaza kuanza kwa Awamu ya Pili ya Operesheni Tokomeza na itazingatia haki zote ikiwemo haki za binadamu.
Nyalandu alisema ingawa awamu ya kwanza kulikuwa na kasoro zilizojitokeza, awamu hii ya pili kasoro hizo zitafanyiwa kazi ili kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa.
Kusitishwa kwa operesheni hiyo kulikosababisha uteuzi wa mawaziri watatu kutenguliwa na waziri mmoja, kujiuzulu kwa mujibu wa Nyalandu, kulisababisha pia tembo 60 kuuliwa.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Kikwete mwishoni mwa mwaka jana ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo) huku Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), akijiuzulu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TAARIFA YA CHADEMA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA M/KITI, FREEMAN MBOWE

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE
Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza;

Tuhuma hizo ni pamoja na;

1.     Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.

2.     Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa
Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa.

3.    Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.

4.     Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.

Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;

1.    Hakuna ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.

2.     Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.

3.    Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

4.     Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.

5.     Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.

6.     Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika.

Imetolewa leo Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

MALINZI AZINDUA KAMPENI YA ISHI HURU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu hiyo iliyozimduliwa tarehe 10 Januari mwaka huu jijini Dar es Salaam iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika (partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya Marekani.
Rais Malinzi amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamekuwa yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa maendeleo ya vijana ambapo ameipongeza Africa Inside Out kwa programu hiyo kwa vile itazuia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
"Moja athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.
"TFF tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu hii. Lakini pia tutaingiza Ishi Huru katika programu zetu za mpira wa miguu kwa vijana. Tutahamasisha jamii katika kupambana na dawa za kulevya," amesema.
Katika uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua semina ya waelimishaji na kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika shule na vituo vya vijana nchini.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MBUNGE WA CHADEMA MH. NDESAMBURO AMKINGIA KIFUA LOWASSA ASEMA ASISAKAMWE

Philemon Ndesamburo na Edward Lowassa 
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionekana kutikiswa na ushawishi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wa kutaka kutimiza safari yake ya kuwapatia Watanzania elimu bure, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), amejitokeza kumkingia kifua na kutaka asisakamwe.

Kauli ya Ndesamburo inakuja siku chache wakati kukiwa na harakati za wazi wazi kuwapinga wanaotajwa kutaka kuwania urais, zikishika kasi ndani ya CCM na kuonekana kuzigonganisha vichwa jumuiya zake.  
Akitoa salamu zake za mwaka mpya jana, pamoja na kuzungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani, Ndesamburo alisema Lowassa hapaswi kushambuliwa kwa kigezo cha kutangaza safari yake.  
“Wanaotangaza nia mbona wako wengi sana huko CCM na wala siyo Lowassa peke yake? Kwenye urais na hata huku chini kwenye ubunge na hata udiwani wako wengi tu wanafanya hivyo. Ina maana hao wanaomnyooshea kidole Lowassa hawa wengine hawawaoni?
“Hata huku kwenye vyama vyetu CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wapo wanaotuvuruga, lakini sasa hivi habari ya mjini ni Lowassa, Lowassa… kama kweli hatupendezwi na hali hiyo tuwanyooshee wote basi, kama hatuwezi wamwache aendeleze ndoto yake. The best way to predict the future is to invent it,” aliongeza Ndesamburo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

CHELSEA YATOA PAUNI MILIONI 25 KUMSAJILI NEMANJA

Kiungo wa Benfica, Nemanja Matic (kulia) anahusishwa na kurejea Chelsea kwa Pauni Milioni 25
Toughness: Jose Mourinho sees Matic as the man to fill Chelsea's need in the holding role
Jose Mourinho anaona Matic ndiye anayefaa katika nafasi ya kiungo mkabaji Chelsea
KLABU ya Chelsea imetoa ofa ya Pauni Milioni 25 kumsajili kiungo wa Benfica ya Ureno, Nemanja Matic arejee Stamford Bridge.
Kiungo huyo hodari alijiunga na Chelsea mwaka 2009, lakini akacheza mechi mbili tu kabla ya kutimkia Ureno mwaka kama sehemu ya dili ya David Luiz kutua Stamford Bridge.
Pamoja nayo, kocha Jose Mourinho sasa anaona Matic kama mtu anayefaa katika nafasi ya kiungo mkabaji wa timu yake.
Chanzo:BIN ZUBEIRY

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

ISRAEL KUMUAGA ARIEL SHARON, ALIKUWA MAHUTUTI KWA MIAKA 8....!!!

Maelfu ya watu nchini Israel wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Ariel Sharon kabla ya mazishi yake hii leo.
Jeneza la Sharon liliwekwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem jana Jumapili huku waombolezaji wakimiminika kumtolea heshima za mwisho kabla ya maziko. Sharon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa miaka 8, akitumia mashine kupumua. Atafanyiwa ibada maalum ya kitaifa leo kabla ya kuzikwa karibu na shamba lake eneo la Sderot.
Waisreli pamoja na viongozi wa dunia, wametoa heshima zao za mwisho , lakini wale ambao wanaweza kusema hawajaguswa sana na kifo cha Sharon ni wapalestina. Mwili wa Sharon ulifikishwa katika bunge la taifa Jumapili ambapo watu waliruhusiwa kuutizama siku nzima. Maombi yalifanywa huku bendera zikipepea nusu mlingoti. Watu waliendelea kumiminika nje ya jengo hilo wengine wakiwasha mishumaa katika hatua ya kumuenzi Sharon.

Wageni mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria ibada maalum ya Ariel katika bunge la taifa wakiwemo makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mjumbe maalum wa Mashariki ya kati Tony Blair, na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.
Sharon anakumbukwa na wengi kwa siasa zake na harakati zake dhidi ya wapalestina wakati akiwa mwanajeshi. Aliidhinisha ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la Palestina na pia baadaye tume ya uchunguzi ilimpata na hatia ya kukosa kuzuia mauaji ya wapalestina yaliyofanywa na wakristo wa Phalangist baada ya Iisrael kuvamia Lebanon.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MBOWE KUMBURUZA ZITTO MAHAKAMANI

Freeman Mbowe na Zitto Kabwe MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anakusudia kumburuza mahakamani, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa madai ya kumkashifu na kumchafulia jina.  
Kwa mujibu wa taarifa toka Kurugenzi ya  Habari na Uenezi ya CHADEMA, Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza. Tayari Mbowe kwa mujibu wa taarifa hiyo, ameshawasiliana na wanasheria wake kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya aliyezusha uongo huo. Ingawa taarifa hiyo haikutaja jina la Zitto, lakini hivi karibuni mbunge huyo katika ukurasa wake wa facebook, aliibua tuhuma nzito dhidi ya Mbowe. 
 
  Zitto, Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo, walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA. Baadaye CC iliwatimua uanachama Mwigamba na Kitila kwa tuhuma za kukisaliti na kukihujumu chama, huku Zitto akikimbilia mahakamani kuzuia asijadiliwe. Akiwa na kesi mahakamani, Zitto aliingia mtegoni kwa kushambulia viongozi wake mitandaoni kwa kutoa tuhuma nzito dhidi ya Mbowe. 
  Katika tuhuma hizo, Zitto alidai Mbowe alipokea michango ya pesa kutoka kwa makada wa CCM, Nimrod Mkono na Rostam Azizi, kusaidia kampeni za CHADEMA mwaka 2005 na 2010.
Pia Zitto alidai kuwa Mbowe alipokea sh milioni 40 mwaka 2005 kutoka kwa Mkono ili asifanye kampeni katika Jimbo la Musoma Vijijini; na kwamba mwaka 2008 alimpatia sh milioni 20 kusaidia CHADEMA ishinde uchaguzi mdogo wa Tarime.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Sunday, January 12, 2014

RAIS KIKWETE ATANGAZA JUMATATU JANUARI 13, 2014 KUWA NI SIKU YA MAPUMZIKO

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
                                         
TAARIFA KWA  UMMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.               
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.               
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Mwisho.

Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
es Salaam.
12 January, 2014

ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YALIVYOFANA ZANZIBAR LEO.

 Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani  na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

CHAMA KIPYA CHA SIASA CHAJA, WALIOFUKUZWA WATAJWA KUKIANZISHA


MSA 775c5
*Chadaiwa kuundwa na waliofukuzwa upinzani
WAKATI fukuto la kufukuzwa uanachama kwenye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) likiwa bado bichi, chama kipya cha siasa kimeanzishwa na watu wanaodaiwa kuwa ni muungano wa wanachama waliofukuzwa kutoka vyama vya upinzani nchini.

Taarifa zilizotufikia na kuthibitishwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, zinakitaja chama hicho kuwa ni African Alliance for Change and Transparence (AACT) na kwamba mipango ya usajili wa muda wa chama hicho inadaiwa kuanza kuratibiwa kwa takribani mwezi mmoja sasa.
Chama hicho kimekamilisha baadhi ya taratibu na kinatarajiwa kupewa usajili wa muda na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siku ya Jumanne, wiki ijayo.
Upo uwezekano wa wanachama waliofukuzwa uanachama kutoka Chadema hivi karibuni kujiunga na chama hicho. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WAZIRI AUAWA KWA KUPIWA RISASI ALIPOKUWA ZIARANI...!!!

014915548-57daaf1f-2e9a-4da7-8305-4392c1149482_dcc90.jpg
Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte Mashariki mwa Tripoli ambako alizaliwa.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu wasiojulikana walimfyatulia risasi kadhaa Hassan al-Droui karibu na soko rasmi mjini humo. Ni mauaji ya kwanza ya afisa wa serikali ya mpito ya Libya.
Libya imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu kuondolewa mamlakani kwa hayati Muammar Gaddafi mwezi Oktoba mwaka 2011. Sirte ilikuwa ngome ya mwisho ambako mapigano yalitokea wakati wa harakati za mapinduzi ya Muamar Gaddafi ambaye alikamatwa na kupigwa risasi akijaribu kujificha kutoka kwa waasi.
Bwana al-Droui alikuwa mwanachama wa zamani wa baraza la mpito lililosimamia kipindi cha mpito baada ya Gadaffi kuuawa. Aliteuliwa kama naibu waziri na waziri mkuu wa kwanza wa mpito na kuendelea kushikilia wadhifa huo hata baada ya Ali Zeidan kuchukua mamlaka.
 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAKONDA AMVAA TENA MH. LOWASSA ...!!!


Paul Makonda, Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa, UVCCM
*******
KWA kipindi kirefu sasa vijana ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tumeshuhudia na kusikia kauli na vitendo vya baadhi ya wanachama wa CCM vinavyoashilia ukiukwaji wa makusudi wa maadili, miiko na kanuni za Chama. CCM katika uhai wake wa miaka 37 baada ya kuunganisha TANU na ASP, imeendelea kukua na kushamiri kutokana na misingi imara ya kikatiba tuliyojiwekea tangu mwaka 1977, ambayo wana CCM wote kwa utashi na hiari tumeienzi na kuifuata. Asiyetaka, ni ruksa kuondoka na kutuachia chama chetu.

Ni kwa njia hii tumeweza kuimarisha mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kutuwezesha kushinda katika chaguzi mbali mbali, hivyo kuendelea kutoa uongozi katika ngazi zote za utawala nchini. Hivyo basi, kitendo chochote kile chenye mwelekeo wa kubomoa mshikamano ndani ya Chama, ni kitendo cha kutudhoofisha, hivyo kutuengua katika uongozi wa nchi. HILI KWA VIJANA WA CCM, HALIKUBALIKI!
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

VIJUE VYAKULA 10 AMBAVYO MWANAUME ANATAKIWA KULA ILI KUONGEZA UWEZO WAKATI WA TENDO LA NDOA...!!!

Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
 
2. POMEGRANATE
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Saturday, January 11, 2014

MTOTO WA AJABU... ANAKULA SUFULIA ZIMA LA WALI, ANAKUNYWA MAJI NDOO MOJA NA KUMALIZA MIKATE SABA KWA MKUPUO LAKINI HASHIBI...!!!

AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo vyake.
Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo:

 
Mkazi wa Mbezi-Kibanda, Andrea Marcus.
Ana uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja,  amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima. Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba.
Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo.
“Sina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema mama wa mtoto huyo.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LAIVA....!!!

 
Rais Jakaya Kikwete, anaweza kutangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri wakati wowote kuanzia sasa.
Hatua hiyo inafuatia uteuzi wa mawaziri watatu kutenguliwa, mmoja kujiuzulu na mwingine kufariki dunia.

Desemba 20, mwaka jana, Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliwasilisha bungeni taarifa ya uchunguzi kuhusiana na athari zilizojitokeza katika Operesheni Tomokeza Ujangili iliyositishwa na serikali wakati wa Mkutano wa 13 wa Bunge kufuatilia malalamiko ya wananchi, wabunge na wadau.

Akiwasilisha ripoti hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, alisema uchunguzi wao ulibaini kuwa operesheni hiyo iliendeshwa bila kufuata taratibu na matokeo yake kusababisha mateso kwa raia, vifo na upotevu wa mali hususani mifugo.

Baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa, wabunge walichachamaa na kushinikiza mawaziri ambao wizara zao zilihusika katika utekelezaji wa operesheni hiyo wawajibike kisiasa au wawajibishwe.

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliamua kujiuzulu wakati mjadala ukiendelea na siku hiyo baadaye Rais Kikwete, alikubaliana na mapendekezo ya wabunge kwa kutengua uteuzi wa mawaziri watatu, Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi); Mathayo David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...