Monday, January 13, 2014

ISRAEL KUMUAGA ARIEL SHARON, ALIKUWA MAHUTUTI KWA MIAKA 8....!!!

Maelfu ya watu nchini Israel wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Ariel Sharon kabla ya mazishi yake hii leo.
Jeneza la Sharon liliwekwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem jana Jumapili huku waombolezaji wakimiminika kumtolea heshima za mwisho kabla ya maziko. Sharon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa miaka 8, akitumia mashine kupumua. Atafanyiwa ibada maalum ya kitaifa leo kabla ya kuzikwa karibu na shamba lake eneo la Sderot.
Waisreli pamoja na viongozi wa dunia, wametoa heshima zao za mwisho , lakini wale ambao wanaweza kusema hawajaguswa sana na kifo cha Sharon ni wapalestina. Mwili wa Sharon ulifikishwa katika bunge la taifa Jumapili ambapo watu waliruhusiwa kuutizama siku nzima. Maombi yalifanywa huku bendera zikipepea nusu mlingoti. Watu waliendelea kumiminika nje ya jengo hilo wengine wakiwasha mishumaa katika hatua ya kumuenzi Sharon.

Wageni mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria ibada maalum ya Ariel katika bunge la taifa wakiwemo makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mjumbe maalum wa Mashariki ya kati Tony Blair, na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.
Sharon anakumbukwa na wengi kwa siasa zake na harakati zake dhidi ya wapalestina wakati akiwa mwanajeshi. Aliidhinisha ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la Palestina na pia baadaye tume ya uchunguzi ilimpata na hatia ya kukosa kuzuia mauaji ya wapalestina yaliyofanywa na wakristo wa Phalangist baada ya Iisrael kuvamia Lebanon.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...