Thursday, July 11, 2013

RAIS KIKWETE AWASHANGAA CHADEMA KUTAKA KAMBI YA KUJILINDA... DR. SLAA NAYE AWATAKA POLISI WAYAVUNJE MAKAMBI YA CCM


Rais wa Tanzania amewashangaa na kuwalaani CHADEMA kwa kutangaza kufundisha vijana namna ya kujilinda na kusema kuwa ni watu wa ajabu kama wamefikia huko.
Mh. Rais kayasema hayo katika kuhitimisha kongamano la amani  huku bwana Cheyo  nae akisema  kuwa  hata kama  ni kutaka kuwa rais wa nchi CHADEMA wamefika kubaya....

Wakati  mh. Rais  akiwashangaa CHADEMA,Katibu Mkuu wa chama  hiyo,  Dr Wilbroad Slaa amelitaka jeshi la polisi kuvunja mara moja makambi yote ya CCM nchini yanayotoa mafunzo kwa vijana wanaoitwa Green Guards.
Kauli  hiyo  ya Dr. Slaa  imekuja  baada  ya  polisi  kuwazuia  CHADEMA kuanzisha  kambi  yoyote  ya  kujihami  na  kwamba  hatua  kali  za kisheria  zitachukuliwa  dhidi  yao  endao  watakaidi  agizo  hilo

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI...!!!

Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.

 

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
  

Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
Na  Mbeya yetu

DIAMOND AELEZA SABABU YA KULALA NA IRENE UWOYA, MAJANGAAAAA...!!!

http://1.bp.blogspot.com/-bO7oXuF0ztg/UTJYht12RUI/AAAAAAAAcgw/-_tbpau4RoE/s1600/IRENE+UWOYA.bmp
 
SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.

Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa  maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.


UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULAI 11, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS




DSC 0697 9cbdb

DSC 0698 d13fc
DSC 0699 4ab80

HII NDO HISTORIA FUPI YA FREEMASON SOMA HAPA....!!!

 
HISTORIA FUPI YA FREEMASON.
Ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.

Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.


1
. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times). Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).
Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.

2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k

MAMA MZAZI WA PROFESA J AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNGONGWA NA GARI HUKO MBEZI JUU, DAR ES SALAAM


Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake. Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'

HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.

ANGALIA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA SHULE WALIZOPANGIWA HAPA...!!!



WASICHANA....<<< BOFYA HAPA>>


WAVULANA....<< BOFYA HAPA>>>

>>Ukitaka kuya download bofya hapo chini

WASICHANA: << DOWNLOAD>>

WAVULANA: << DOWNLOAD>>


1. KWA KUANGALIA MATOKEO YA WAVULANA CLICK LINK HII https://docs.google.com/file/d/0B6EsT3rjf-pzamlnNDhZcXJVeUU/edit?usp=sharing

2. KWA KUANGALIA MATOKEO YA WASICHANA CLICK LINK HII https://docs.google.com/file/d/0B6EsT3rjf-pzY0VGVHBfcXdfazQ/edit?usp=sharing

Wednesday, July 10, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 10, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

MWANAMUZIKI MARIAH CAREY ADONDOSHWA CHINI NA VIATU VIREFU...!!!

Mariah Carey
Mariah Carey
MUIMBAJI mwenye sauti yenye mvuto nchini Marekani Mariah Carey ajikuta katika wakati mgumu na aibu ya aina yake baada ya viatu virefu maarufu kwa jina la 'high heels' kumdodosha wakati akicheza shoo ya video ya nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Beautiful'
Viatu virefu ni moja ya vitu ambavyo muimbaji huyo huvipenda lakini huenda hatotaka tena kuvisikia kutokana na hali iliyompata kudondoshwa na viatu hivyo na kumsababishia maumivu makali na hatimaye kukimbizwa hospitali .

Mtu wakaribu wa mwanamuziki huyo aliiambiwa chanzo kimoja cha habari kuwa ajali hiyo ilitokea wakati wa utengenezaji wa video ya remix ya 'Beautiful' iliyokuwa ikiongozwa na muwewake Nick Canno, ndipo muimbaji huyo alidondoka na kusababisha maumivu ya bega. 

Wakati huo huo chanzo kingine kiliuambia mtandao wa New York Post kuwa ajali hiyo ilitokana na viatu virefu alivyokuwa amevaa wakati anacheza video hiyo. 

HII NDIO TWEET YA AGNES MASOGANGE BAADA YA TAARIFA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Katika picha agnes masogange anaonekana akihesabu mihela yake na akatweet kuwa " Anatafuta hela sio umbeya watu wasile bata mnazusha"

KAMATI KUU YA CHADEMA YABARIKI FUJO MIKUTANONI .... WAANDAA "RED BRIGADE"

MUHTASARI
Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.
RIPOTI KAMILI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE 06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM.

Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura kuanzia tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na mambo mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini.

Kamati kuu imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

1:0. Hali ya Siasa Nchini.

Kamati kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na kuzingatia mambo yafuatayo:

a) Shambulio la Bomu Arusha.

 Kamati Kuu imesikitishwa na kulaani kwa nguvu zote tukio la Bomu Arusha lililosababisha watu wanne kuuwawa na zaidi ya watu 70 wengine kujeruhiwa vibaya.

KASEJA ANAWINDWA KILA KONA, USIKU NA MCHANA



KLABU za APR ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya zipo katika harakarti za kumwania aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Simba, Juma Kaseja, imefahamika.
Habari za uhakika ambazo Sports Lady Blog imezinyaka zinasema viongozi wa timu hizo wameshaanza mazungumzo na Kaseja ili kumsajili kwa msimu ujao katika nchi hizo.
 
Mdau mmoja wa soka ambaye yupo karibu na uongozi wa timu hizo, alidokeza jana kwamba, kwa nyakati viongozi wa timu hizo mbili, wamekuwa kwenye harakati za kumsaka Kaseja, wakiamini bado ni kipa mwenye uwezo mkubwa langoni.
 
Licha ya kutemwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao, Kaseja bado kipa namba moja wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen, raia wa Denmark.
Habari zaidi zinasema, klabu ya APR iliyofika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashabiki na Kati-Kagame Cup na kufungwa na Vital’o wiki moja iliyopira nchini Sudan, inapewa nafasi kubwa ya kumpata kipa huyo.
 
Hayo yanatokea huku Kaseja akiwa kwenye kambi ya timu ya Stars inayojiandaa na mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Afrika kwa Nyota wa Ndani –CHAN dhidi ya Uganda itakayopigwa Julai 13, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
“Ujue baada ya Simba kutangaza kuachana na Kaseja, kuna timu nyingi hasa za nje zimeonesha nia ya kutaka kumsajili lakini mpaka sasa ni APR na Gor Mahia ndio wako makini zaidi na mchakato huo,” kilisema chanzo hicho.

HUYU NDIE MWIGIZAJI WA HOLLYWOOD ALIYEMTUKANA OBAMA NA MKE WAKE

amanda bynes obama ugly tweet

 
 
Anaitwa Amanda Bynes ni mwigizaji maarufu HoolyWood. Wiki chache zilizopita alikua katika vita ya maneno na msanii Rihana kupitia mtandao wa twitter, sasa vita hiyo kaihamishia kwa Raisi wa nchi yake Obama pamoja na mke wake.

Katika tweet aliyoandika jana alisema “Barack Obama and Michelle Obama are Ugly” na mda mchache tu baada ya kuandika hivyo watu walianza kumshambulia kwa kumwambia kua alichofanya si kitu kizuri kabisa. Pia katika kuonyesha kua watu hawamungi mkono wengi wa followers wake walimunfollow.


Hii si mara yake ya kwanza kuwaita watu weusi ugly kwani alishawahi kumuita na Drake jina hilo

MWANAMKE APEWA MIMBA NA MAITI, ALIJIFANYISHA MAPENZI WAKATI ANAMUOGESHA.


Mwanamke mmoja mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti ameushangaza ulimwengu kwa kitendo chake cha Kujilazimishia mapenzi kutoka kwa mwanaume ambaye amekufa hadi kufikia kupata Ujauzito.
Felicity Marmaduke (38), Mkazi wa Lexington Missouri, alikumbwa na mkasa huo baada ya kumtamani marehemu huyo wakati wa kumuosha na ndipo alipoamua kujiweka juu yake na kuanza kufanya naye mapenzi, cha kushangaza ni kwamba maiti hiyo iliweza kutoa mbegu za kiume.

Baada ya wiki mbili, mwanamke huyo alienda kujipima ujauzito baada ya kujihisi tofauti na ndipo alipogundua ya kwamba ameshika mimba.
Ilimbidi atoe taarifa kwa familia husika ambayo ilimfungulia mashataka kwa kitendo chake hata hivyo naye amefungua mashtaka akidai iuzwe moja ya nyumba ya marehemu huyo ili alipwe gharama za matunzo.

MCHUNGAJI AKAMATWA KWA KOSA LA KUUPINGA USHOGA NA USAGAJI.



Tonny Miano ni Mchungaji kutoka nchini mMarekani ambaye alikwenda Nchini Uingereza katika Kufanya Mahubiri Huko. Kilichomkuta kilisababishwa na yeye kusema ya kwamba tabia za kishoga na kisagaji ni Dhambi na hazimvutii Mungu,.


Polisi walipigiwa simu na mwanamke mmoja aliyekuwa eneo la tukio akilalamika ya kwamba hajafurahishwa na maneno anayoongea Tonny, ambaye ni askari mstaafu wa jeshi la polisi nchini Marekani.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...