Rais
wa Tanzania amewashangaa na kuwalaani CHADEMA kwa kutangaza kufundisha
vijana namna ya kujilinda na kusema kuwa ni watu wa ajabu kama wamefikia
huko.
Mh.
Rais kayasema hayo katika kuhitimisha kongamano la amani huku bwana
Cheyo nae akisema kuwa hata kama ni kutaka kuwa rais wa nchi CHADEMA
wamefika kubaya....
Wakati
mh. Rais akiwashangaa CHADEMA,Katibu Mkuu wa chama hiyo, Dr Wilbroad
Slaa amelitaka jeshi la polisi kuvunja mara moja makambi yote ya CCM
nchini yanayotoa mafunzo kwa vijana wanaoitwa Green Guards.
Kauli
hiyo ya Dr. Slaa imekuja baada ya polisi kuwazuia CHADEMA
kuanzisha kambi yoyote ya kujihami na kwamba hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao endao watakaidi agizo hilo
Dk.
Slaa, amesema kauli ya Jeshi la Polisi inadhihirisha namna wahusika
wasivyofahamu sheria kwa kile alichoeleza kuwa wao hawaundi majeshi bali
vikundi vya ukakamavu.
Alisema
ni heri msemaji wa jeshi hilo angekaa kimya kuliko kulifedhehesha Jeshi
la Polisi kwa tamko lisilokuwa na ushawishi wa kisheria.
“Nawashauri
hawa waanze na Tendwa…ila kwanini wameanza leo sisi tulishayalalamikia
makundi ya CCM kwa barua na hata walipomaliza mafunzo yao kule Igunga
tukapiga na picha wao hawakuinua mdomo kuliongelea,” alisema Dk. Slaa.
Alisema
katika miaka minne iliyopita CHADEMA ilikuwa ikionyesha kwa ushahidi
namna vijana wa CCM wanavyopewa mafunzo ya kijeshi, ikwamo silaha kutoka
nje ya nchi huku wahusika wakiendelea kukaa kimya.
Aliongeza
kuwa hali hiyo ya kuamka baada ya kauli ya CHADEMA inatia nguvu shaka
yao, aliyodai kuwa makundi ya CCM yanafanya mafunzo kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi.
Dk.
Slaa alitolea mfano kundi la vijana wa CCM walioweka kambi katika shule
ya wazazi katika Kata ya Ivumwe, Mbeya mjini na kisha kuwateka katibu
wa CHADEMA Mbeya mjini na baadhi ya wanachama wake.
Alisema
katika tukio la Ivumwe wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani wa hivi
karibuni, CHADEMA walitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Mbeya ambaye
aliwajibu kuwa wapeleke ushahidi kama vijana hao ni wahalifu.
Alibainisha
kuwa CCM imekuwa na kawaida ya kukusanya vijana kutoka maeneo tofauti
na kisha kuwapa mafunzo ya kijeshi na silaha kwa ajili ya kuwadhuru
wapinzani na kutolea mfano Kambi ya Ulemo aliyosema ilikuwa na vijana
waliopewa mafunzo ya kijeshi.
“Tunawasubiri
tuone hatima yao ni nini, sisi tunajua Jeshi la Polisi limeshajitoa
kulinda viongozi wa CHADEMA sasa kwanini tusijilinde wenyewe,” alisema
Dk. Slaa.
Source: BBC, Tanzania Daima,Jamii Forum
No comments:
Post a Comment