Thursday, April 11, 2013

JOHARI AGOMA KUTINGISHA MAUNO YAKE MBELE YA RAY


MKONGWE kwenye ‘Industry’ ya Filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alitoa kali ya aina yake baada ya kukataa kuzungusha nyonga mbele ya mwigizaji mwenzake, Vincent Kigos ‘Ray’ anayedaiwa ni mpenzi wake

Tukio hilo lililonaswa na mwandishi wetu juzikati, lilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati wasanii hao walipojumuika pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kitokee kifo cha msanii mwenzao, Steven Kanumba.

Akiwa viwanjani hapo, Johari aliitwa kupanda jukwaani na wasanii wenzake kwa ajili ya kucheza sebene kidogo lakini yeye alikataa na mwandishi wetu alimsikia akijitetea kuwa hawezi kukata nyonga mbele ya wasanii wenzake hususan Ray ambaye ni bosi mwenzake kwenye kampuni yao ya RJ Company.

“Siwezi kujidhalilisha mbele ya umati huo kwa kukata kiuno tena na bosi mwenzangu yupo pale, labda ningekuwa nimelewa kiasi cha kutojitambua hapo ningefanya madudu kama hayo,” alisema Johari.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, MULUGO ATANGAZA VITA NA WAZUSHI WAKE

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya sekondari. Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha.

Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.

“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.

“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.

Kwa miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo alisema yanamchafulia jina katika jamii.

Kuhusu suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi.

Naye Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule Direct.

Muluigo alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini

HALI TETE KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;

1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)

2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.

3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.

4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'

5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.

6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.

*Pia kuna issue ya mkataba tata(White Elephant) kati ya TBC na Startimes(Wachina!) ambao Terms, Conditions, Investment, Dividend na Shares havijawekwa wazi na sawasawa, japokuwa Mkurugenzi mkuu na Bodi yake ya sasa wanadai wameurithi tu lakini sio 'wapishi' kamili wa hicho kilichopikwa!!

source: JF

KAULI YA ZITTO KUTOKA BUNGENI ASUBUHI HII

CAG ameweka mezani taarifa yake asubuhi hii. Katika mkutano wa Kumi wa Bunge, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Ukaguzi ya mwaka 2008 Kwa kubadilisha vifungu 38, 39 na 40 ambapo Serikali ingeleta majibu yake sambamba na Taarifa ya CAG. Serikali haikuleta majibu hayo. Wamevunja Sheria wakiisha nikiwa siku ya kwanza ya kuanza kutekelezwa kwake. Spika alipowataka Serikali kutoa majibu, Mawaziri walibaki kutazamana tu

HATARI : WALA MAHINDI HATARINI KUDUMAA AKILI

WATAALAMU wa masuala ya afya na kilimo kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamebaini mahindi, karanga na mihogo yenye sumukuvu ni moja ya vitu vinavyochangia saratani ya ini, udumavu wa mwili na akili kwa watoto.
Ingawa takwimu sahihi hazijapatikana kuonesha madhara ya kila 
nchi kutokana na utafiti hizo kuendelea, tatizo limeelezwa kuwa ni kubwa hasa katika nchi za Afrika kutokana na mfumo mzima wa uzalishaji katika sekta ya kilimo na ukuzaji wa mazao usiozingatia utaalamu.

Kutokana na ukubwa wa tatizo, wataalamu hao kutoka nchi 20, wanakutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu, kuanzia jana, kutafuta njia madhubuti za kukabiliana na sumukuvu. Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizochukua hatua za awali dhidi ya tatizo hilo.
Akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema,
“Lengo la mkutano huu ni kuwapa fursa wataalamu kuja na mikakati itakayoisaidia serikali na sekta binafsi kupambana na sumu ya aflatoxin kwa kuwa hata hapa Tanzania ni tatizo kubwa.”
Dk Mwinyi alifafanua kuwa, tatizo kubwa linaonekana kwenye mazao yanayoathiriwa zaidi na sumukuvu ambayo ni mahindi, mihogo na karanga na husababisha watumiaji kupata saratani ya ini na watoto hudumaa akili na mwili.
Alisema pamoja na serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na sheria ya kudhibiti vyakula vinavyoingia nchini, lakini sheria pekee haziwezi kumaliza tatizo hasa ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi wanatumia nafaka hizo wakati zikiendelea kukua shambani bila kuzipima kiwango cha sumukuvu kinachotakiwa.
Sumukuvu ni aina ya sumu inayosababishwa na kuvu katika mazao na ingawa haiepukiki katika nafaka, kuna kiwango kinachopaswa kuwepo na kinapozidi, huleta madhara hayo.

PETER WA P-SQUARE APATA MTOTO WA KIUME

DUNIANI KUNA MAMBO, HAWA WANASHEREHEKEA KIFO CHA MARGARET THATHER..........!!!




JK Atia Saini Kitabu cha Maombolezo ya Bi. Margaret Thatcher




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jana, Jumatano, Aprili 10, 2013 ametia saini Kitabu cha Maombolezo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Margaret Thatcher ambaye alifariki dunia Jumatatu wiki hii kwa ugonjwa wa kiharusi akiwa na umri wa miaka 87.

Rais Kikwete ametia saini Kitabu hicho kwenye Ubalozi wa Uingereza katika Tanzania ulioko Jengo la Umoja mjini Dar es Salaam.

Rais alikaribishwa kwenye Ubalozi huo na Balozi wa Uingereza katika Tanzania, Mheshimiwa Bi. Dianna Melrose na wafanyakazi wengine wa ubalozi huo na amekwenda moja kwa moja kutia saini kitabu hicho mara baada ya kuwasili kwenye Ubalozi huo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 11, 2013

DSC 0038 d286d

DSC 0039 807d7
DSC 0040 53179

Wednesday, April 10, 2013

Irene Uwoya afunguka kuhusu skendo yake na Diamond.......!!!

Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond platnumz kutawala vyombo vya habari na kwenye mitandao hapo juzi, hatimaye bongomovies.com tuliamua kumtafuta kwa simu mwanadada Irene Uwoya ili tuweze kumuuliza juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi lwa mwanadada Penny kwa kijana wa “mbongofleva” diamond platnumz.

Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.
Source:Bongo Movies

SHILOLE ANASA KWENYE PENZI LA MZUNGU...!!

SIKU chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’ wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.

Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.


Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa. 


Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.


Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).


Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”

ANGALIA YALIYOJIRI KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS UHURU KENYATTA .



SHAA AAHIDI KUVUA NGUO ZOTE HADHARANI ENDAPO VIDEO YAKE ITAFIKISHA VIEWS 100,000


Kwa  waliokuwa  na  hamu  ya  kumuona  huyu  naye  akiwa  nusu  uchi  na  kivazi  cha  kuogelea  tuu, huu  sasa  ni  wakati  wao.....

Coca Cola  pop Star  maarufu  kwa  jina  la  Shaa  amedai kuwa  yupo  tayari  kuvua  nguo  zake  hadharani  na  kuyaanika  maungo yake  nyeti  na  kubakiza  kichupi  cha  kuogelea  tu  endapo  video  yake  mpya  ya  Lava Lava itafikisha  views  100,000  katika  mtandao  wa  youtube 
Popout
“Lava Lava Video imefikisha views 44,000+ leo.Endapo  itafikisha 100,000 basi  ntavua  nguo  zote  na kuogelea coco beach mchana kweupe lets do,”Alitweet  Shaa  katika  mtandao  wa  kijamii wa Twitta  na  kuongeza

“Niliitupia kiutani tu nikidhani in one day kupata views elfu50 ni ngumu…sasa naona watu wameniamkia! Kwa spidi hii…mmmh…noma,”

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE APRIL 10, 2013

DSC 0014 88cc4

DSC 0011 7fee3

DSC 0008 4c17f

BUNGE KITANZINI LEO

Mchakato wa marekebisho ya kanuni za Bunge umeibua mjadala mkali baina ya wabunge, huku wengi wao wakieleza kuwa hatua hiyo ina lengo la kulifanya Bunge kukosa meno ya kuisimamia Serikali.

Miongoni mwa mambo yaliyozua mvutano katika kikao cha awali cha wabunge wote ni suala la muda wa wabunge kuchangia bungeni na jinsi wanavyotakiwa kupangwa kulingana na idadi yao kwa kila chama.

Bunge linakusudia kuwasilisha azimio la kutaka kubadili kanuni ambazo zilitarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika jana bungeni, lakini kutokana na baadhi ya mapendekezo kupingwa, hatua hiyo iliahirishwa hadi leo.


Mabadiliko hayo ni muhimu kabla ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuwasilishwa leo, kwani baadhi yake yanalenga kuwezesha mfumo mpya wa Bunge wa kuanza na Bajeti za wizara na baadaye kumalizia na Bajeti Kuu ya Serikali.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...