Msanii/Mtangazaji
Soggy Doggy ameacha mzigo pande za redio Uhuru na leo rasmi ameondoka Dar es
salaam nakwenda Iringa ambapo atakuwa akifanya kazi katika kituo kingine cha
Redio kinachoenda kwa jina la Ebony Fm.Soggy Doggy ashawahi kufanya kazi katika
vituo vya redio mbalimbali hapa nchini kama Arusha na Mwanza.
Friday, March 01, 2013
Mtendaji mkuu TAZARA Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika aachia ngazi.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa
Mbikusita-Lewanika,(Pichani) hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha
kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa
miaka mingine mitatu.
Hatua
hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la
Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo
aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi
mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa
wao.
Habari
za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake
cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi
maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu
kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya Tanzania
kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika
kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza
la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu
huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha
nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali
ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Taarifa
za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania
haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo,
ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na
uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi
wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia
kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali
nchini.
Tarehe
25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail,
liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye
anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila
(chief),
Gazeti
hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe 22 Februari, 2013
kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na
Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa
kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya
Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.
Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.
Google Waja na Miwani Inayopiga na Kurekodi Picha kwa Maelekezo.
TEKNOLOJIA waliyotumia
Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au
kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya
Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia
na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google
glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa
kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo
unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua
video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu
unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na
kitu kama “Skype-style video chat”.
Umesafiri
kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua
kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na
unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.
Google
glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha,
kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote
haya bila kutumia mikono yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa
hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au
vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au
kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.
Kwa
nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh.
mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani,
sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka
kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa
hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa
hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia
kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
*Imeandaliwa na www.thehabari.comRais Kagame wa Rwanda akanusha kuwa na nia ya kugombea tena urais kwa awamu ya tatu.
Rais
Paul Kagame wa Rwanda amesema hana mpango wa kugombea tena muhula wa
tatu madarakani baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2017.
Akizungumza
mjini Kigali, rais Kagame amevishutumu vyombo vya habari kuanzisha
mjadala juu ya iwapo ataibadili katiba ili aweze kuwania muhula
mwingine.
Mjadala
huo ulifuatia hatua ya rais huyo mapema mwezi huu kuunda kamati katika
chama chake, kutafakari mwelekeo wa nchi baada ya muda wake madarakani
kumalizika.
Chama
cha upinzani cha FDU-Inkingi, kimetoa tangazo kikilaani njama zozote za
kuifanyia marekebisho katiba ili kuruhusu muhula wa tatu kwa rais.-DW
Hivi ndivyo Chadema walivyotikisa Mbeya jana
Mapokezi makubwa ya Mh. Freeman Mbowe katika viwanja vya Rwanda Nzovwe jijini Mbeya.
Burudani mbalimbali pia zilikuwepo
Mh. Mbowe pia alimtaka waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi kujiudhuru pamoja na naibu waziri wa wizara hiyo kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne na kusema kuwa katika siku 14 alizozitoa zimebaki siku tatu za wao kuendelea kuwepo madarakani na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo wataitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza waondolewe katika nafasi hizo. Mara baada ya kauli hiyo Mbowe aliwataka wananchi kuchangia fedha kwaajili ya wahanga siku ya maandamano ambapo zilichangishwa fedha kiasi cha sh. 3, 267, 550/=
Wakichangisha
fedha kwaajili ya wahanga wa maandamano yatakayofanyika pindi mawaziri
wataposhindwa kujiudhuru picha ya kwanza ni Mh. Sirinde, inayofuata ni
Mh. Msingwa na ya mwisho ni Mh. Mbowe.
Picha na Keny Pino
JOKETI KUPAMBA UZINDUZI KAMPENI YA UNYANYASAJI
Na Mwandishi
wetu
MWANAMITINDO
nyota nchini, Joketi Mwegelo, anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa kampeni ya kupinga
unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kike, unaotarajiwa kufanyika
keshokutwa, ambapo shughuli mbalimbali na mada zitatolewa.
Joketi, ambaye anawika katika tasnia mbalimbali nchini ikiwemo urembo, mitindo, muziki na filamu, atashiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama Okoa Mtoto wa Kike Tanzania utakaofanyika katika Kata ya Nyamongo wilayani Tarime, Mara.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group iliyoandaa kampeni hiyo, Mossy Magere, imesema kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika na Joketi atawasili wilayani Tarime kesho tayari kwa kushiriki na atatoa mada ya masuala ya ujasiriamali kwa washiriki wa tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.
Mossy alisema kuwa mbali na Joketi, wasanii mbalimbali watashiriki kutoa burudani wakiwemo wasanii nyota wa bongo fleva na wale wa asili wanaotamba mkoani Mara.
'Maandalizi yote ya msingi yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa uzinduzi ufike, Joketi anatarajiwa kuwasili hapa kesho tayari kwa kushiriki nasi. Atapata fursa ya kutoa mafunzo na mbinu
za
kimaisha kwa washiriki ambao wengi ni wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani
hapa,' alisema Mossy.
Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi sita, itazinduliwa rasmi keshokutwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ameshirikishwa kwa karibu na Kampuni ya Nyumbani Kwanza.
Alisema mchakato wa uundwaji wa klabu za wapinga unyanyasaji katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Tarime ambapo kampeni hiyo inaanzia umekamilika na wanafunzi wamevutiwa na kujiunga kwa wingi kwenye klabu hizo ambazo zitakuwa kichocheo cha kuendeleza kampeni hiyo.
Mossy aliongeza kuwa, uundwaji wa klabu hizo unalenga kukiwezesha kizazi cha sasa na kijacho kuwa mstari wa mbele kukataa vitendo vya unyanyasaji.
“Kila jambo jema huanzia ngazi za chini, kwa sasa tunaendelea kuunda klabu za wapinga unyanyasaji ambazo zitakuwa zikipewa mafunzo na mbinu mbalimbali ili kuwajenga kufahamu madhara wakiwa wangali wadogo shuleni.
Thursday, February 28, 2013
Rais Kikwete apokea ujumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan.
SASA WATEJA WA NMB KUWEKA PESA ZAO KUPITIA M-PESA
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB
Mark Wiessing,( kulia) na Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt
wakitia sahihi katika mkataba kam ishara ya ushikiano na makubaliano ya
kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa
kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na Afisa Mkuu wa Biashara-
M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba kama ishara ya ushikiano
na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye
akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB
wakishuhudia.
…………………………………………………………………
NMB leo hii imeweka historia kwa
kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wake nchini kuweza
kuweka amana zao kupitia mawakala zaidi ya 40,000 wa M-Pesa Nchi nzima.
Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha kutoka NMB kwenda MPESA. NMB na
Vodacom zimezindua huduma hiyo rasmi leo hii kwenye makao makuu ya NMB.
Sasa mtu yeyote au wateja wa NMB
hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani
sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB bila kwenda tawini.
Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha
kwenda MPESA.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,
Bw.Mark Wiessing, “alisema “Ni huduma ya aina yake ambayo itawezesha
mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na
haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji
wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa
watanzania wote mijini na vijijini”.
MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO-CHADEMA JOHN MNYIKA:'NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAWO WA UMEME, SERIKALI IELEZE WANANCHI UKWELI NA HATUA KUHUSU UDHAIFU KWENYE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA DHARURA.'
Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema Mh John Mnyika-
---
Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28
Julai 2012.
Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa
bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa
nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na
Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa
kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.
Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka
viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli
wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka
zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo.
Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa
nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya
mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu
ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia
Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.
Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati
na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua
zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi
katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo
kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme.
Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi
maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za
ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa
Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27
Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja
ya Serikali tarehe 28 Julai 2012.
Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa
kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi
wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa
mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana
na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala
ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe
kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
27 Februari 2013
Mtanzania apewa uwaziri Rwanda
RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas
Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya
Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba
alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri
wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia
mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.
Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).
Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”
Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.
“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.
Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.
Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.
Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.
Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.
Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.
Chanzo: Mwananchi
Tigo yaboresha huduma za mawasiliano na KABAANG
Meneja Chapa ya Tigo bw. William
Mpinga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG kwa ajili ya wateja
wao.kulia ni bi. Jacqueline Nnunduma Mtaalam wa ubunifu wa ofa za Tigo.
Mbunifu wa ofa za Tigo bi.
Jacqueline Nnunduma akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi
wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG.kushoto bw. William Mpinga
Meneja Chapa ya Tigo.
Mshindi wa Tigo smartcard
promotion bw. Julius Raphael Kanza akiwa uwanja wa ndege J.K Nyerere
akiongea na waandishi wa habari kabla ya safari yake ya kuelekea Madrid
nchini Hispania kutazama mechi kati Real Madrid na Fc Barcelona jumamosi
wiki hii itakayofanyika kwenye uwanja Santiago Bernabeu.
Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama "KABAANG" ambayo itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu tatu kwenye kifurushi kimoja.
“KABAANG” ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi bila kikomo.
" Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali.
Kifurushi hiki cha wiki kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg. William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.
Ndg. Mpinga aliendelea kwa kusema " kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo".
Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi atume neno "Kabaang" kwenda 15711, na baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.
Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama "KABAANG" ambayo itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu tatu kwenye kifurushi kimoja.
“KABAANG” ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi bila kikomo.
" Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali.
Kifurushi hiki cha wiki kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg. William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.
Ndg. Mpinga aliendelea kwa kusema " kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo".
Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi atume neno "Kabaang" kwenda 15711, na baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akutana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi, Bw Philippe Dongie Ikulu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi,Philippe Dongie,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na Rais,leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi,Philippe Dongie,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman,ikulu-Zanzibar
MASHINDANO YA MPIRA YA MPINGA CUP YAANZA RASMI LEO
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya
Dar es Saalam Suleiman Kova akijiandaa kudaka mpira ikiwa ni ishara ya
uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki
maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga
cup imedhaminiwa na Airtel , Rotary Club, Mr price na Shoprite ikiwa
na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki
na kupunguza ajali barabarani . akishuhudia kushoto ni Mkuu wa kikosi
cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akidaka
mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup
inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi
leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na Airtel , Rotary
Club, Mr price na Shoprite ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama
barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani .
akishuhudia kushoto ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP.
Mohamed Mpinga.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akikagua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Michuano hii imeanza rasmi kwa mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese anayefata pichani ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga. Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akikagua timu kabla ya mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese leo wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup, anayefata pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
kikosi cha timu ya Kawe Tiptop katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi
oyesterbay , katikati pichani ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga. kikosi cha timu ya Manzese katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi
oyesterbay , katikati pichani ni Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es
Saalam Suleiman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akikagua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Michuano hii imeanza rasmi kwa mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese anayefata pichani ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga. Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akikagua timu kabla ya mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese leo wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup, anayefata pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
kikosi cha timu ya Kawe Tiptop katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi
oyesterbay , katikati pichani ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga. kikosi cha timu ya Manzese katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi
oyesterbay , katikati pichani ni Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es
Saalam Suleiman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga
Subscribe to:
Posts (Atom)