Thursday, February 15, 2018

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI ZIMBABWE AFARIKI DUNIA

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.

Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65, na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.

Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jioni ya Februar 14.

Monday, February 12, 2018

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARY 12, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

 
Subscribe YouTube Channel @jambotz

ZUMA KUNG'OLEWA LEO...?!!

Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.

Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.

Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.

AGONGWA NA TRENI NA KUFARIKI AKIJIPIGA SELFIE...!!!

Picha haihusiani na tukio hili. 

Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand.

Rafiki yake alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliyokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi.

Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi.

Rafiki huyo wa kiume alipata majeraha mabaya. Idadi ya watu wanaofariki wakipiga selfie katika maeneo hatari inaongezeka.

Wednesday, February 07, 2018

MKUTANO WA KUMJADILI RAIS ZUMA WAAHIRISHWA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma.

Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma.

Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika upinzani.

Siku ya jumanne bunge la taifa hilo liliahirisha hotuba ya kitaifa iliyotarajiwa kutolewa na rais Zuma.
Hata hivyo baadhi ya mitandao nchini humo imekaririwa ikisema kuwa rais Zuma anajiandaa kuachia madaraka iwapo makubaliano katiika mambo kadhaa yatafikiwa.

Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC Cyril Ramaphosa.

Upande wa upinzani wenyewe unashinikiza Zuma kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani, huku kikao cha kamati kuu kikidaiwa kuwa na nguvu ya kuweza kumuondoa Zuma madarakani hata bila hiari yake.

Friday, February 02, 2018

MZEE KINGUNGE AFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO

Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo..

Mzee Kingunge enzi za uhai wake amelitumikia Taifa la Tanzania mpaka ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri.

Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana. Yeye kingunge ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Animal. 

Tuesday, January 02, 2018

TAZAMA PICHA 9 ZA BABU SEYA NA FAMILIA YAKE WAKIWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM




Disemba 09, 2017 kwenye sherehe za Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 8,158 ikiwemo familia ya Nguza Viking.

RAIS MUSEVENI ASAINI SHERIA YA KUONDOA UKOMO WA UMRI WA RAIS

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha mswada unaoondoa kikomo cha umri kwa wagombea urais nchini humo, hatua inayompa nafasi ya kuwania tena urais mwaka 2021.

Mswada huo pia unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.

Kwa kuwa sheria hiyo itaanza kutekelezwa sasa, Bw Museveni anaweza akaongoza taifa hilo hadi 2031.

IKULU YAFUNGUKA KUHUSU KUAPISHWA KWA DR. SLAA

Zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi.

Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa.

Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu.

TAZAMA VIDEO YA BABU SEYA NA WANAE WALIPOENDA IKULU KUMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA ALIOWAPA

Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza walipofika Ikulu jijini Dar Leo Januari 2, 2018 kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha wake aliotoa kwao dhadi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani tangu walipohukumiwa miaka 13 iliyopita.

Wednesday, December 13, 2017

VIGOGO WENGINE WA ACT WAHAMIA CCM

 Mwenyekiti na katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Singida, wamejivua uanachana na vyeo vyao na kuhamia CCM.

Viongozi hao ni aliyekuwa mwenyeketi Wilfred Noel Kitundu na katibu wa mkoa wa chama hicho, Loth Robert Thomas.
Viongozi hao wamechukua uamuzi huo mbele ya mkutano mkuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhazili mjini hapa juzi.

Kwa nyakati tofauti walisema changamoto ambazo upinzani walikuwa wakizipigia kelele, Rais John Magufuli ameendelea kuzitatua kwa ufanisi.

Tuesday, December 05, 2017

MBWA WA POLISI WAMUUMBUA ALIEDANGANYA KUWA KAPOLWA MIL. 20 ZA KAMPUNI

Mfanyakazi  wa kampuni ya saruji ya Simba Cement, Edward Ngassa amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kutengeneza tukio la uongo la kuporwa Sh. milioni 20.4 na majambazi jana.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, mbwa wa polisi mwenye mafunzo ndiye aliyegundua udanganyifu huo wa Ngassa nyumbani kwake.

Kamanda Muroto alisema mtuhumiwa huyo alitengeneza tukio la uongo kwamba ameporwa fedha na majambazi katika eneo la Uhindini karibu na mgahawa wa Sunja.

Saturday, December 02, 2017

MKULIMA AFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI AKIWA SHAMBANI USIKU

Mkazi mmoja wa kijiji cha Senga Kata ya Kamsamba wilaya ya Momba aliyetambuliwa kwa jina la Cleo Saini (23/25)amefariki baada ya kupigwa na radi alipokuwa analima kwa jembe la kukokotwa na ng'ombe mapema saa tisa usiku.

Pamoja na marehemu kufariki pia ng'ombe wawili waliokuwa wakikokota jembe wamekufa. Mtendaji wa kijiji cha Kamsamba Venance Athanas ametoa taarifa Polisi Kituo cha Kamsamba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Mathias Nyange amekiri kutokea kwa tukio ambapo Polisi wamekwenda eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DECEMBER 02, 2017 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

https://jambotz8.blogspot.com/

 
Subscribe katika YouTube channel ya Jambo Tz upate kuona habari na matukio mbalimbali toka duniani kote.

MBUNGE NASSARI AVAMIWA NA MAJAMBAZI USIKU WA LEO

Katika ukurasa twitter wa Mh. Joshua Nassari ameandika kuwa amevamiwa na watu waliokuwa na silaha za moto, na mara baada ya yeye pamoja na mkewe kuwagundua waliamua kukimbilia kituo cha polisi yeye ili kuokoa maisha yao.

Sunday, November 26, 2017

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU SABA KWA VYOMBO VYA UCHUNGUZI KUBAINI MMILIKI WA MAGARI YALIYOTELEKEZWA BANDARINI

Haya ndio maagizo ya Rais John Pombe Magufuli Bandarini leo baada ya kugundua uwepo wa magari zaidi ya 50 yaliyoingizwa nchini kwa kutumia jina la Ofisi ya Rais.

Saturday, November 25, 2017

TAZAMA VIDEO YA WAZIMBABWE WAKIIGIZA JINSI MUGABE ALIVYOLAZIMISHWA KIJIUZULU

Subscriber to our channel on YouTube @jambotz upate video nyingine zaidi.

PROF. LIPUMBA "SIKUTEGEMEA KAMA DR. SLAA ATATEULIWA"

Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amezungumzia uteuzi wa Dk. Wilbroad Slaa kuwa balozi akisema hakutarajia.

Rais John Magufuli juzi alimteua Dk. Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chadema kabla ya kukihama chama hicho wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wakati wa mchakato wa uchaguzi huo, Profesa Lipumba na Dk. Slaa ambao vyama vyao vilikuwa katika umoja uliojulikana Ukawa, walijiondoa baada ya Chadema kumpitisha Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.

Akizungumza na Mwananchi jana, Profesa Lipumba alisema, “Imekuwa kama surprise, sikutegemea kama Dk. Slaa atateuliwa kwa sababu muda mwingi yupo Canada”.

Hata hivyo, Profesa Lipumba alisema hana shaka na uteuzi huo “Narudia, sikutegemea. Ila popote atakapopangiwa kazi Dk. Slaa atafanya kwa sababu najua ni mchapakazi,” alisema.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Rais Magufuli ana mamlaka kisheria ya kumteua mtu atakayemuona anafaa katika nafasi fulani.

FAMILIA YAPATA UPOFU KATIKA MAZINGIRA TATANISHI

(Picha hii haihusiani na tukio)

Mama mmoja aliyetambulika kwa jila la Doroth Otieno na watoto wake watatu wanaoishi Kisumu nchini Kenya, wamepata upofu wa ghafla bila kujua chanzo chake.

Doroth ambaye ameolewa na mkata miwa nchini Kenya, amesema hali hiyo imeleta matatizo kwenye ndoa yake na familia.

Akisimulia jinsi alivyopata upofu wake huo Doroth amesema mtoto wake wa kwanza nwenye miaka 16 na mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya wasichana ya Nyamonye, alipata upofu ghafla baada ya kuhisi kama macho yake yana mchanga, na kisha kuwa kipofu kabisa, huku watoto wake wawili wa kiume Vicent na Benson nao wakiwa na tatizo hilo hilo.

MUGABE NA MKEWE WASUSIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MPYA

 Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe Grace walikosa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa baada ya wananiasa hao kukubaliana kwamba Mugabe anaweza kupumzika.

Sababu kuu ilioteolewa ni kwamba bwana Mugabe alikuwa amechoka.
Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kujiuzulu kama rais kufuatia shinikizo kutoka kwa jeshi na raia.

Hatua hiyo inajiri baada ya Mugabe na mkewe kufumta kazi rais huyo mpya wakati alipokuwa makamu wa rais kwa madai kwamba alikuwa akipanga njama za kutaka kumuondoa madarakani rais Mugabe.

Saturday, November 18, 2017

WALEMAVU DAR WAANZA KUPATA NEEMA.

Hospitali ya CCBRT imeguswa na kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kutafuta miguu bandia kwaajili ya watu wenye uhitaji kwa kuwapatia matibabu wagonjwa 35 waliokatwa miguu kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Miguu hiyo ya kisasa ina thamani ya zaidi ya Shilling Million 157 ambapo kati ya wagonjwa 35 waliokuwa wakitembelea magongo kwa muda mrefu baada ya kukatwa miguu, 21 wameshawekewa Miguu Bandia na sasa wanaendelea na shuguli zao baada ya kuwa wazima.

Tuesday, November 14, 2017

TAZAMA VIDEO YA DR. SHIKA AKIREJEA NYUMBANI KWAKE KUTOKA KITUO CHA POLISI ALIPOKUWA AKISHIKILIWA


Dkt. Luis Shika akiwasili nyumbani akitokea Polisi.
Afafanua kwanini hakuweza kulipa 25% iliyokiwa mnadani adai tatizo ni kutokuelewana.

Monday, November 13, 2017

LULU AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA

Mahakama kuu ya Dar es salaam imemuhukumu muigizaji wa filamu, Elizabeth Michale, maarufu kama 'Lulu', kifungo cha miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku, mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.
Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii maarufu wa kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...