Tuesday, January 02, 2018

IKULU YAFUNGUKA KUHUSU KUAPISHWA KWA DR. SLAA

Zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi.

Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa.

Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu.


Kutokana na hali hiyo, mwandishi wetu aliwasiliana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili kujua kwa nini imechukua muda mrefu kumuapisha Dk. Slaa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, alimwambia mwandishi wetu kwa njia ya simu kuwa, si Dk. Slaa peke yake ambaye hajaapishwa.

“Utaratibu ukikamilika ataapishwa. Na sio yeye peke yake ambaye hajaapishwa,” alisema kwa kifupi Msigwa bila kuingia kwa undani zaidi kuhusu suala hilo.

Siku chache baada ya kutangazwa kushika nafasi hiyo, Dk. Slaa alikaririwa akisema anashukuru Mungu kwa kuteuliwa na rais.

Dk. Slaa kwa sasa yupo Canada na alitimkia nchini humo baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu Chadema.

Aliondoka Chadema baada ya kuwepo sintofahamu kati ya viongozi wa chama hicho, baada ya kumpokea waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyehama CCM.

Na GPL

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...