Wednesday, February 07, 2018

MKUTANO WA KUMJADILI RAIS ZUMA WAAHIRISHWA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma.

Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma.

Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika upinzani.

Siku ya jumanne bunge la taifa hilo liliahirisha hotuba ya kitaifa iliyotarajiwa kutolewa na rais Zuma.
Hata hivyo baadhi ya mitandao nchini humo imekaririwa ikisema kuwa rais Zuma anajiandaa kuachia madaraka iwapo makubaliano katiika mambo kadhaa yatafikiwa.

Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC Cyril Ramaphosa.

Upande wa upinzani wenyewe unashinikiza Zuma kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani, huku kikao cha kamati kuu kikidaiwa kuwa na nguvu ya kuweza kumuondoa Zuma madarakani hata bila hiari yake.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...