Monday, February 12, 2018

AGONGWA NA TRENI NA KUFARIKI AKIJIPIGA SELFIE...!!!

Picha haihusiani na tukio hili. 

Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand.

Rafiki yake alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliyokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi.

Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi.

Rafiki huyo wa kiume alipata majeraha mabaya. Idadi ya watu wanaofariki wakipiga selfie katika maeneo hatari inaongezeka.


Kisa hicho kilitokea siku ya Alhamisi asubuhi ya wiki iliyopita katika kituo cha treni cha Samsen mjini Bangkok, kulingana na maafisa wa polisi wa Wissanusak Seub akiongezea kwamba maafisa walikuwa wakichunguza kilichotokea.

Kuchukua video huku umesimama mbele ya treni imeonekana kuwa swala hatari, hususan nchini India.

Mnamo mwezi Januari, mtu mmoja aliyekuwa akijichukua kanda ya video akisubiri treni iliokuwa ikikaribia aligongwa na treni hiyo mjini Hyderabad nchini India.

Mnamo mwezi Oktoba 2017, vijana watatu waligongwa na treni walipokuwa wakijaribu kuchukua picha ya selfie katika jimbo la Karnataka, huku vijana wengine wawili wakifariki wakati walipokuwa akipiga picha katika barabara ya reli mjini Delhi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...