
Rais Jakaya Kikwete amesema maadui
wote ambao walitaka kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kwa lengo
la kuvuruga amani ya nchi wamedhibitiwa .
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali
yake itaendelea kulinda amani ya nchi na maadui wote wanaohusika na
kutaka kuvuruga nchi watachukuliwa hatua kali za kisheria. "Kulikuwapo
na upepo mbaya, lakini kwa sasa Tanzania ni shwari na tumemshinda adui,"
alisema Rais Kikwete jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya
Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yaliyoandamana na sherehe
za kuzima Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.
Alisema katika siku za hivi karibuni,
maadui wasioitakia mema Tanzania walikuwa na mkakati wa kuvuruga amani
ya nchi, lakini Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola
vimewadhibiti na nchi iko salama.
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali
haiwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa amani kwa sababu inajua wazi
kwamba nchi ikiingia kwenye mgawanyiko, mshikamano utavurugika na
shughuli za maendeleo zitasimama.











Wafanyakazi hao wakibadilishana mawazo hapa na pale katika hospitali ya Muhimbili leo hii
Picha Kwa Hisani ya Fullshangwe Blog










