Tuesday, June 09, 2015

WAGOMBEA URAIS VIKUMBO KILA KONA

mangula press
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotangaza nia ya kugombea urais, sasa ni wazi wanapigana vikumbo kila kona ya nchi.
Hatua hiyo inatokana na kila mtangaza nia kwa nyakati tofauti kutoa kauli nzito.
Wapo makada ambao kauli zao zinaonyesha wazi kuwa kuna mgongano ndani ya CCM, huku wengine wakitangaza nini watakifanya endapo watateuliwa kuongoza nchi.

MEMBE: SINA UNDUGU NA JK

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hana undugu na Rais Jakaya Kikwete.
Membe ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, alikanusha undugu wake na Rais Kikwete mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuwania urais kupitia CCM. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 09, 2015 YALE UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03482
DSC03483
DSC03484
DSC03485
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WATOTO KUNUFAIKA NA DAWA MPYA ZA ARV

Dawa za sasa zinaelezwa kuwa na ladha nzuri kuliko zinazotumiwa hivi sasa
Watoto walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa za kupunguza makali.

Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WACHEZAJI WAPYA WANOGESHA MAZOEZI YANGA

Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi ya kumiliki mpira na kupiga pasi
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi ya kumiliki mpira na kupiga pasi
Kocha wa Yanga (mwenye jezi ya njano) akifuatilia mazoezi
Kocha wa Yanga (mwenye jezi ya njano) akifuatilia mazoezi.
van Pluijm akitoa mazoezi kwa mchezaji wa mpaya kigeni wakati wa mazoezi
van Pluijm akitoa mazoezi kwa mchezaji wa mpaya kigeni wakati wa mazoezi. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UZI MPYA WA ARSENAL 2015/16 HUU HAPA...!!!

n2
Kwa wale wanaojiuliza ni lini Arsenal watatoa jezi zao mpya za Puma kwa ajili ya msimu wa 2015/2016, jibu hili hapa.
 Jezi za nyumbani za Arsenal zitakazotumika msimu ujao wa 2015/2016 zimevuja….hivyo mashabiki wa London na duniani kote wajiandae kupata mzigo mpya.
Cheki uzi mpya wa nyumbani wa Arsenal chini;
Screen Shot 2015-06-09 at 12.17.50 
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

OSCAR PISTORIOUS KUACHILIWA, AUGUST

Oscar Pistorious, akilia kwa uchungu
Wakuu wa magereza Nchini Afrika Kuisini wamesema kuwa Oscar Pistorius, ataachiliwa kutoka gerezani mwezi Agosti mwaka huu miezi kumi baadaye, ili atumikie kifungo cha nje, cha hukumu aliyopewa ya miaka mitano.
Bingwa huyo wa nishani ya dhahabu katika mbio za Olimpiki, alikutwa na hatia ya kumpiga risasi bila ya kukusudia na kumuuwa mpenziwe, Reeva Steen-kamp,
na kumuuwa mwana mitindo huyo.
Mahakama kuu Nchini Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka huu, itasikiliza rufaa ya waendesha mashtaka ya kujaribu kupunguza makali ya hukumu iliyotolewa dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Sunday, June 07, 2015

WAGOMBEA URAIS CCM WAWANUFAISHAUKAWA

Dar es Salaam. Baada ya wiki nzima ya makada wa CCM kutangaza nia na hatimaye kuchukua fomu za kugombea urais, wapinzani ndio wanaonekana kunufaika zaidi kutokana na wengi kutumia hotuba zao kuelezea udhaifu wa kila mmoja.

CCM imepanga mwezi mzima, kuanzia Juni 3 hadi Julai 2 kuwa ni muda wa makada wake kuchukua na kurudisha fomu kabla ya vikao vya juu vya chama hicho kukutana kuanzia Julai 12 kuchuja wagombea na baadaye kumpata mmoja atakayesimama kwenye Uchaguzi Mkuu kupambana na wa vyama vingine.

Tayari makada 15 wameshachukua fomu na wengine wanaendelea kuchukua, huku waliochukua wakiwa wameshaanza kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini 30 kila mkoa ili kupata idadi ya wadhamini 450. Wanatakiwa kupata wadhamini kwenye mikoa 15, kumi ya Bara na mitano ya Zanzibar. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.<

MSAFARA WA MAKONGORO NYERERE WAPATA AJALI

 
Gari ilikuwa imebeba wasaidizi wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Makongoro Nyerere likiwa limeanguka wilayani Kasulu, Kigoma jana wakati likiwa kwenye msafara kwa ajili ya kusaka wadhamini. Picha na Blog ya Michuzi 

Akitoa taarifa za ajali hiyo, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa linaendeshwa na Julius Kambarage Nyerere ambalo lilipinduka saa 4:30 lilipofika eneo la Mwilamvya na kujeruhi watu watano.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 07, 2015 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03387
DSC03388

Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.DSC03389

NYAMA YA PUNDA YASINDIKWA NCHINI...!!!

SERIKALI imekiri kuruhusu uanzishwaji wa kiwanda cha kusindika nyama ya punda kilichopo mkoani Dodoma.

Imekiri hivyo baada ya Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohamed (CUF), kuibua hoja hiyo juzi (ijumaa) jioni wakati wa kupitisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Katika hoja yake, alitaka kujua juhudi zilizofanywa na Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), kukagua viwanda vya usindikaji wa chakula ikiwa ni pamoja na kiwanda hicho. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BARCELONA YAWACHAPA JUVENTUS 3-1

http://jambotz8.blogspot.com/p/blog-page_26.html
Barcelona walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Hata hivyo Alvaro Morata alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya gusa ni guse kati yake na Messy.
http://jambotz8.blogspot.com/p/blog-page_26.html
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.

Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ANGALIA PICHA 10 ZA MASTAA WA MPIRA WALIPOKUWA WATOTO

messi
Lionel Messi wa sasa na wakati akiwa mtoto
ronaldo
Cristiano Ronaldo wa sasa na wakati akiwa mtoto.
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Friday, June 05, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 05, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03316
DSC03317
DSC03318
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

IDADI YA WALIOFARIKI GHANA YAFIKIA 175


Ghana moto
Takriban watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na stima.


Ghana moto
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.


Ghana moto
Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.

Ghana moto 
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu, Accra alipotembelea eneo la tukio. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

RAHEEM STRLING KUELEKEA OLD TRAFFORD

Raheem Sterling
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.

Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi. Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki.

Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

SERENA ATINGA FAINALI FRENCH OPEN 2015

Serena William,mchezaji tenis nambari moja duniani akifurahia ushindi.
Serena Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu kucheza fainali za mwaka huu.

Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi. Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.

Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa. Mapema katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

Tuesday, June 02, 2015

AL-SHABAAB WADAIWA KUVITEKA VIJIJI KENYA

Alshabaab
Hofu kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kundi la wapiganaji wa Al shabaab Limeviteka vijiji kadhaa katika mpaka wa Kenya na somalia.
Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo hilo. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 20 NIGERIA

Mlipuko nchini Nigeria
Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Mji huo ulikuwa umeshambuliwa saa za alfajiri siku ya jumanne na washukiwa wa kundi la Boko haram .
Saa chache baadaye ,mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua katika soko la kuuza ngombe la Gamboru ndani ya mji huo kulingana na walioshuhudia.
Wakati wa kuapishwa kwake rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kuwa anayahamisha makao makuu ya kijeshi katika vita dhidi ya wapiganaji hao kutoka mji mkuu wa Abuja hadi Maiduguri. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...