Thursday, April 02, 2015

RAIA WA YEMEN WAKIMBILIA SOMALIA

Raia wa Yemen wakikatika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo
Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia, Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao.

Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.

Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BUHARI AAHIDI KUTOKOMEZA BOKO HARAM NIGERIA

Muhammadu Buhari, Rais mteule wa Nigeria
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa linalokabili nchi.

Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.

 "Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."

Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.

"Tumebaini matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe. 

Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."

 Anasema rais huyo mteule wa Nigeria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Friday, March 27, 2015

GWAJIMA ASAKWA NA POLISI KWA KUMKASHIFU KARDINALI PENGO

GWAJIMA
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kujisalimisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.


Hatua hiyo ya polisi imekuja baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko, ambapo inadaiwa Mchungaji Gwajima alitoa lugha ya kashfa dhidi ya Kardinali Pengo ambaye alipinga tamko lililotolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) la kuipigia kura ya Hapana Katiba Inayopendekezwa.


Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Suleiman Kova, imemtaka Mchungaji Gwajima kujisalimisha haraka katika Kituo cha Polisi cha Kati kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

JK ATEUA WABUNGE WAPYA

rais-kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Dk. Grace Puja na Innocent Sebba kuwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, ilisema uteuzi huo unatokana na mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e).


Alisema ibara hiyo, inampa mamlaka rais ya kuteua wabunge wasiozidi 10 na kwamba uteuzi wa wabunge hao ulianza Machi 20, mwaka huu. Kibanga alisema kuteuliwa kwao kumekamilisha idadi ya wabunge ambao rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kikatiba.


Alisema awali Rais Kikwete aliwateua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Asha Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria), Saada Salum Mkuya (Waziri wa Fedha) na Janeth Mbene (Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara).


Wengine walioteuliwa awali ni Profesa Sospeter Muhongo, Shamsi Vuai Nahodha, Zakhia Meghji na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 27, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KILIMANJARO KINARA WA POMBE YA VIROBA


Mji wa Moshi, Tanzania

 Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe  hasa ya  viroba,  ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.

Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.

Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa Matumizi ya Pombe kwa vijana  katika mikoa ya  Kilimanjaro, Mwanza, Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza  kwa unywaji wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIL WAYNE AMTANGAZA CHRISTINA MILIAN KUWA MPENZI WAKE MPYA

lil-wayne na mpenzi wake christina-milian
BOSI wa kundi la Young Money, Lil Wayne, amemuweka wazi mpenzi wake mpya, Christina Milian, ambaye ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo analoliongoza.
Baada ya kuweka wazi habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa Twitter, aliandika, “Samahani kwa kusubiri muda mrefu kujua nini kinaendelea, kwa sasa hakuna tena maswali nikiwa na Christina, huyu ni mpenzi wangu.”
Wayne ni baba wa watoto watano, na sasa yeye, mpenzi wake huyo na mtoto wake wa kwanza, Regina aliyezaa na mama mwingine wanafanya kazi pamoja katika kundi hilo.

Thursday, March 26, 2015

LOWASSA AKUBALI YAISHE URAIS CCM

Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa
Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa

SIKU moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kumuonya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.
Pia Lowassa ametumia nafasi hiyo na kuwaomba wale wote ambao bado wana nia ya kumshawishi agombee nafasi hiyo ya urais, wasubiri kwanza hadi pale chama chake hicho kitakapotoa maelekezo.
Akizungumza na vijana 60 wa bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali, Mbeya waliokwenda pia kumshawishi agombee nafasi hiyo, mjini Dodoma jana, alisema si vyema kwa maofisa wa chama kuzungumzia masuala ya wanachama wao kwenye vyombo vya habari wakati kuna vikao vya chama.
Alisema watu waliojitokeza na kumshawishi kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ya Urais, hajawaita wala kuwalipa chochote kama inavyodaiwa na kwamba walikuwa wakifuata maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa mkoani Ruvuma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya Uhuru.
Alisema katika siku hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania wawashawishi viongozi wanaoona wanafaa ili wajitokeze kugombea nafasi hiyo ya Urais. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MACHI 26, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
..


Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'VIJANA WENGI HAWANA NGUVU ZA KIUME'

Dk. mwele 
Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),imesema vijana wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea, wanaongoza kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela alisema kwa sasa tatizo hilo ni kubwa ambalo linawakumba vijana wengi hususan barani Afrika.
Alisema hali hiyo,imesababisha vijana hao kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya Mundex, AAili waweze kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
“Vijana wengi wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea wana matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo limewafanya kutafuta dawa za kuongeza nguvu ili waweze kuzitumia na kupunguza ukubwa wa tatizo.
“Tangu tugundue dawa hii, idadi kubwa ya wanaokuja kununua ni vijana hasa wenye umri wa miaka 30, hali ambayo inaonesha wazi kuwa tatizo hili linakua kwa kasi,” alisema Dk Mwele.
Alisema kipindi kilichopita, matatizo hayo yalikuwa yanawapata wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea, lakini sasa hivi ni tofauti kabisa ambapo vijana wenye umri huo ndiyo wenye matatizo hayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ASKARI WAWILI MBARONI KWA FEDHA BANDIA


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo akionyesha sare za jeshi la wananchi zilizokamatwa kutoka kwa askari polisi baada ya kupekuliwa nyumbani kwake. 

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo alisema askari hao walikamatwa juzi saa tisa mchana katika Mtaa wa Old Maswa, Kata ya Nyakabindi, wilayani Bariadi.

Alisema askari hao walifika kwenye kibanda cha M-pesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki aina ya Sunlg kwa lengo la kuweka fedha hizo katika simu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BABA MBARONI KWA KUWABAKA WATOTO WAKE...!!!

Mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka 11 na mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, wilayani Kibaha mkoani Pwani. 

Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Habari zilizolifikia gazeti hili, zilisema kuwa katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi na watoto wenyewe, baba huyo alianza kuwafanyia binti zake vitendo hivyo mwaka 2013 kwa siku ambazo mkewe ambaye nimama wa wasichana hao hakuwapo hadi usiku wa Machi 19, mwaka huu. Kwa sasa tunayahifadhi majina ya familia hiyo.
Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 15 anayesoma darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa akiwa darasa la tatu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAREKANI: UGANDA HATARINI KUSHAMBULIWA

Polisi wa Uganda wakidhibiti Al Shabab
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.
Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake. Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana.

Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

JESHI LA SAUDIA LASHAMBULIA WAASI, YEMEN

Wapiganaji Yemen
Saud Arabia imeanza operesheni zake za kijeshi nchini Yemen, ikiwa ni kujibu ombi la Rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansour Hadi. Balozi wa Saudi Arabia Nchini Marekani amesema kuwa, taifa lake na washirika wao wa ghuba wanatumia mashambulizi ya angani katika harakati za kuunga mkono serikali halali ya Yemen, ili isichukuliwe na kundi wa waasi la Houthi.

Awali duru zasema kuwa wapiganaji wa Houthi walikuwa wakikaribia kuutwa mji wa Aden, ulioko kusini mwa Nchi hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

HODGSON KUONGEA ULAJI ENGLAND

Roy Hodgson
Shirikisho la kandanda nchini Uingereza limesema lina mpango wa kuwa na mazunguzo na Kocha mkuu wa timu ya England Roy Hodgon mapema mwaka ujao.

Hodgon mwenye miaka 67 alipokea mikoba ya kuifundisha England mwaka 2012 kutoka kwa Fabio Capello lakini timu ikatolewa mapema katika hatua ya makundi kwenye kombe la dunia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Tuesday, March 24, 2015

CCM WATOANA MACHO URAIS...!!!


JOTO la Uchaguzi wa Rais ndani ya CCM linazidi kupanda huku makada na viongozi wa chama hicho wakipigana vijembe hadharani.

Hali hiyo inatokana na kile kinachojitokeza sasa, kuibuka kwa makundi ya jamii, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, kuwashawishi makada kadhaa wa CCM wawanie nafasi hiyo ya uongozi wa nchi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Makada ambao wamekuwa wakishawishiwa kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Wakati baadhi ya makada wengine wanaotajwa kutaka kuwania urais ndani ya CCM wakimlalamikia Lowassa, wachambuzi wa siasa wamekuwa wakihoji mpango wa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alipochapisha vitabu na kugawa kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu, lakini makada wenzake wamekuwa kimya, hawajalalamikia kitendo chake hicho.

KIKWETE AIONYA POLISI MATUMIZI YA NGUVU

jk
RAIS Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha kutumia nguvu kupita kiasi kwa wananchi wakati linapotekeleza majukumu yake ya kazi.

Pia amelitaka kuwa makini kutokana na nchi kukabiliwa na mambo matatu muhimu ya uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapigakura, kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipofunga mafunzo ya uongozi katika ngazi ya urakibu katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Kurasini (DPA).
Alisema polisi wanayo haki ya kuwachukulia hatua wananchi wanapodai haki lakini wafuate utaratibu ili wasivunje amani.

Hata hivyo, Rais Kikwete aliwaonya wananchi kutokujichukulia sheria mkononi akisema jeshi la polisi halitawafumbia macho watakaovunja sheria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TOFAUTI YA ADA VYUO VIKUU SASA BASI

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango

MWONGOZO wa ada elekezi utakaondoa utata wa utofauti wa kulipa ada baina vyuo na vyuo nchini, unatarajiwa kukamilika na kuanza rasmi kutumika mwezi ujao.
Kwa sasa mwongozo huo umeshaandaliwa na kinachosubiriwa ni mfumo wa kompyuta utakaosaidia kukokotolea ada zitakazotumika katika vyuo vikuu nchini ambao ndio utakamilika rasmi Aprili mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Makilagi (CCM), aliyetaka kujua mchanganuo wa ada baina ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na endapo unaendana na hali halisi.
Akijibu swali hilo, Kilango alikiri kuwa kumekuwa na tatizo hilo la utofauti wa utozaji ada katika vyuo mbalimbali nchini kwa muda mrefu, na kwa sasa Tanzania ina vyuo vikuu 53 na taasisi 21 zinazotoa shahada. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...