Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. PICHA|MAKTABA
Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda ametoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia
maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za
harusi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kwebwe aliyezungumza kwa niaba ya Pinda
katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari
Mwenyeheri Anuarite iliyopo Makoka, jijini Dar es Salaam.
“Urithi pekee kwa watoto wetu ni elimu, unaweza
kumwachia mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo
urithi pekee…: Watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu
kama ambavyo tunafanya katika sherehe,” alisema Kebwe akiongeza:
“Utamkuta mtu anachangia fedha nyingi katika
harusi na kama tunavyojua harusi moja, ukianza na ‘send off’, ‘kitchen
part’ na harusi yenyewe ni fedha nyingi, lakini mtu huyo huyo ukimwambia
achangie masuala ya elimu, hutamwona.”
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu
Gaudence-Makoka wamiliki wa shule hiyo, Padre Evarist Tarimo, alisema
kuwa malengo ya sherehe hiyo ni kuchangisha Sh250 milioni kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana ili kuondoa adha wanayoipata kwa
sasa.
“Hivi sasa vyumba vya madarasa tunavitumia kama
mabweni, hivyo wanasomea humo na kulala humo humo, jambo ambalo
kitaaluma si zuri. Tunatarajia tutakapomaliza ujenzi huo tutawawezesha
wanafunzi wetu kusoma na kulala katika mazingira mazuri na nina hakika
juhudi za wadau zitaweza kukamilisha ujenzi huu,” alisema. Habari
tulizozipata baadaye zilisema jumla ya Sh41.2 milioni zilikusanywa.
Fedha taslimu ni Sh13.3 milioni. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz