Tuesday, November 18, 2014

VIONGOZI MANYARA, KITETO WAKALIA KUTI KAVU


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akitoa kauli ya serikali bungeni jana, kuhusu mauaji ya wakulima na wafugaji wa Wilayani Kiteto, Mkoani Arusha.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali itafanya mabadiliko ya kiutawala katika ngazi mbalimbali Wilaya ya Kiteto na Mkoa wa Manyara wiki hii ili kuimarisha uongozi kukabiliana na mauaji ya wakulima na wafugaji yaliyosababisha vifo vya watu 17 tangu Januari 12 mwaka huu hadi sasa.

Pinda alisema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akitoa taarifa kuhusu vurugu zinazoendelea Kiteto kati ya wafugaji na wakulima na kusababisha mauaji.

Alisema mabadiliko ya uongozi wa kiutawala katika eneo hilo ni moja ya hatua ambazo zinachukuliwa kitaifa nyingine zikiwa ni kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya kuondoa na kuepuka na kutatua migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

“Kupanga mipango ya maeneo mbalimbali wilayani Kiteto na kutatua migogoro inayojitokeza kwa kushirikisha viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii kama vile malaigwanani, wazee wa kimila na viongozi wa dini,” alisema Pinda.

Alisema jambo lingine ni kupanga matumizi bora ya ardhi na upimaji wake katika matumizi mbalimbali na kuimilikisha kwa wananchi.

Pinda alisema hali ya mauaji Kiteto imekuwa ni ya kujirudia, kwani Januari 12 mwaka huu, wafugaji walifanya mashambulizi ya silaha za moto na za jadi kwa wafugaji na kusababisha vifo vya watu 10, kuteketeza pikipiki sita na mabanda 53 kuchomwa kitu ambacho kilionyesha kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupanga.

Pinda alisema Novemba 11, mwaka huu katika Kijiji cha Matui, mapigano ya wakulima na wafugaji yalitokea na kusababisha vifo vya watu watano na Novemba 13 katika Kijiji cha Chekanao, wakulima wawili waliuawa na maboma 13 kuchomwa.

“Pamoja na hali hiyo kudhibtiwa katika vijiji hivyo, bado wananchi wana hofu juu ya maisha yao,” alisema Pinda. Alisema Polisi Makao Makuu Dar es Salaam imetuma askari wake Mkoa wa Manyara. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...