Rais John Pombe Magufuli akiondoka
katika benki ya CRDB, Tawi la Holland baada ya kumaliza shughuli iliyompeleka.
Rais John Pombe Magufuli akiwapungia
wananchi mkono wakati akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland.
Wakati akikaribia
kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya
benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao
waliyokwishaingia. Like
page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram
@jambotz.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi
ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine
wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi
walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.
James Charles, ambaye ni dereva wa
taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona
ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye
gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua
tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa
kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa
na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri
tutasikia amefuata nini,” alisema Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa
chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa
tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia
nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu
alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema. Like
page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram
@jambotz.