Monday, April 11, 2016

CHINA KUJENGA VIWANJA 60,000 VYA SOKA KWA MIAKA 6...!!!

China inapania kujenga viwanja 60,000 vya Kandanda katika kipindi cha miaka 6 ijayo.
Uwanja wa taifa wa Beijing
Hayo ni baadhi ya mapendekezo katika ruwaza ya kandanda ya China ya 2050 ya kuifanya nchi hiyo iwe kati ya mataifa makuu duniani katika kandanda. Ripoti moja ya serikali imeelezea mipango ya kuimarisha idadi ya wachezaji na watoto wanaosakata dimba kutimia watoto milioni 50.
Viwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya. Kulingana na ruwaza hiyo China itakuwa na vilabu vyenye hadhi ya kimataifa kufikia mwaka wa 2050. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia la kandanda na hata kushinda kombe la dunia.
Aidha rais Jinping pia anaitaka kombe la dunia la kandanda liandaliwa nchini mwake. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...