Saturday, April 30, 2016

WAZIRI MKUU "TUTAUFANYIA KAZI USHAURI WA WAZIRI MKUU"

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeupokea na itaufanyia kazi ushauri wa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliyetaka Benki ya Standard ICBC ya Uingereza na kampuni dada ya Stanbic Tanzania kuchunguzwa juu ya mkopo wa hatifungani wa Sh1.2 trilioni ambao umegubikwa na ufisadi.

Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais-Tamisemi na Utawala Bora mwaka 2016/17 na kutaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza suala hilo na ukweli ukibainika, Serikali itakwepa kulipa deni la Sh2 trilioni ambazo Tanzania inatakiwa kulipa ikiwa ni deni na riba.

Majaliwa alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari juu na hatua ambazo Serikali imezichukua kutokana na sakata hilo linalodaiwa kuwa na harufu ya ufisadi, kwamba baada ya uchunguzi kukamilika taarifa itatolewa.

“Nikiwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni nimeupokea ushauri wake na kwa kweli tutaufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuchunguza,” alisema Majaliwa.

Wakati akichangia mjadala huo, Zitto alisema Machi 2013, Serikali ilikopa Sh1.2 trilioni kwa msaada wa Benki ya Standard ya Uingereza, ambayo kwa sasa inaitwa Standard Bank ICIC plc na kwamba mkopo huo umeanza kulipwa Machi mwaka huu mpaka mwaka 2020 kwa mikupuo tisa.

Alisema mpaka kufika mwaka 2020 Tanzania italipa deni pamoja na riba ya Sh2 trilioni huku kukiwa na wasiwasi kwamba fedha ambazo zilipatikana kutokana na mkopo huo hazikufika kule kunakotakiwa. Taarifa zinaeleza katika kikao hicho ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuhudhuria, Rais aliwakumbusha maofisa hao majukumu yao ya kazi na kupanga mikakati mbalimbali.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...