Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Saturday, February 14, 2015
Sunday, February 01, 2015
Saturday, January 24, 2015
HIKI NDICHO ALICHOKISEMA PROF. MUHONGO ALIPOTANGAZA KUJIUZULU LEO...!!!
Aliyekuwa Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhuongo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhuongo, amejiuzulu wadhifa huo
kutokana na kuchoshwa na sakata la Akauti ya Tegeta Escrow.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Barabara
ya Samora, Profesa Sospeter Muhongo amesema ameamua kujiuzulu ili kuwa
sehemu ya suluhisho la suala la akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha
Muhongo alisema kuwa suala la ankauti ya Tegeta Escrow limekuwa
likizungumzwa na kufanya mambo mengine yasiendelee na huku watanzania
walio wengi ni masikini wakihitaji umeme na sio kuuliza tegeta Escrow.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Friday, January 23, 2015
HATIMA YA MUHONGO NDANI YA SAA 48 ZIJAZO...!!!
Zikiwa zimebaki siku tatu kabla
ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuanza mjini Dodoma, sasa hakuna shaka
kwamba Rais Jakaya Kikwete atafanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
wakati wowote kuanzia leo na kabla ya Jumapili (saa 48) kutokana na
kukabiliwa na safari ya nje.
Rais anatarajiwa kufanya mabadiliko hayo baada ya
kumwondoa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye
Akaunti ya Tegeta Escrow baada ya kuingiziwa Sh1.6 bilioni kwenye
akaunti yake.
Mwingine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, ambaye anatuhumiwa kutoshughulikia kwa makini sakata
hilo na kusababisha Serikali kupoteza fedha hivyo kuwapo kwa uwezekano
mkubwa wa kumvua uwaziri utakaomlazimu Rais kufanya mabadiliko madogo
kwenye baraza lake, ikiwa ni miezi isiyozidi mitano kabla ya kuvunja
Bunge kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Rais Kikwete anaweza kutangaza mabadiliko hayo wakati wowote kuanzia leo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
HUYU NDO MTANZANIA TAJIRI ANAYE ENDESHA MAGARI YA KIFAHARI NA YA BEI KULIKO MTANZANIA MWINGINE...!!!
Hi ni gari nyingine aina ya Lamborghini anayo miliki mfanyabiashara Davis Mosha huko Bongo.
"Heshima Pesa Shikamoo Makelele" Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz. |
EMIRATES KUMWAGA AJIRA KWA WATANZANIA
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya
Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba
Yahya
KATIKA kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa hususan kuwatafutia ajira Watanzania nje ya
nchi, Wizara hiyo kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, Umoja
wa Falme za Kiarabu umefanikisha kulishawishi Shirika la Ndege la
Emirates kuajiri Watanzania wengi zaidi kuanzia mwaka 2015.
Emirates, moja ya mashirika ya ndege tajiri zaidi duniani, linamiliki
zaidi ya ndege za kisasa 280, huku likiwa na safari za uhakika duniani
kote.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya
Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba
Yahya alisema shirika hilo litaajiri Watanzania katika kada mbalimbali.
“Wamekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo maofisa
wake wanaosimamia ajira watakuja nchini (Tanzania) Machi 2015 kwa ajili
ya kuwafanyia usaili Watanzania watakaoomba kazi hizo na kupata uteuzi
wa awali,” alisema.
Aliwataka Watanzania kuchangamkia ajira hizo, ambazo awali
zilitangazwa Julai 2014, lakini ni Watanzania wachache tu walioomba na
hivyo kutofikia lengo lililokusudiwa.
“Baada ya mazungumzo ya kina, uongozi wa Emirates umekubali kuongeza
muda wa kuzitangaza ajira hizo kwa mara nyingine na kupanga kufanya
usaili kama ilivyoelekezwa hapo awali,” alisema.
Aliwasisitiza Watanzania wenye sifa na vigezo stahiki, kutumia fursa
hiyo kuomba nafasi hizo na pia kujiandaa vyema katika usaili ili
wajihakikishe ajira katika soko la ajira la kimataifa.
Kaimu Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania
(TaESA), Boniface Chandaruba aliwataka waombaji wote kuhakikisha
wanapata barua kutoka wakala huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KAMATI TATU ZA BUNGE ZAMGOMEA MAKINDA
Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akiongoza kikao cha Kamati ya
Uongozi kinachojumuisha wenyeviti wote wa Kamati za Bunge kilichokutana
jana kupanga ratiba ya mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza vikao vyake
Jumanne ijayo. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge.
Danadana zimeendelea juu ya
utekelezaji wa azimio la tatu la Bunge kuhusu kashfa ya Akaunti ya
Tegeta Escrow linaloagiza kuwajibika kwa wenyeviti wa kamati zake tatu
za kudumu, baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda kukaririwa akisema
wameshajiuzulu, lakini wajumbe wake wameibuka jana na kusema
hawatafanya uchaguzi hadi watakapopata maelekezo kutoka Ofisi ya Spika.
Azimio hilo ambalo ni moja ya manane ya Bunge hilo
linasema: “Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na
kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao
wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.”
Wenyeviti hao na kamati zao katika mabano ni
Victor Mwabalaswa (Nishati na Madini), Andrew Chenge (Bajeti) na William
Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala).
Juzi, Spika Makinda aliwaeleza waandishi wa habari
kwamba wenyeviti waliotakiwa kuvuliwa nyadhifa zao tayari wamejiuzulu
na kamati husika zinatakiwa kufanya uchaguzi kupata wengine wapya. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
CCM YAREJESHA AMANI SUDAN KUSINI
BAADA ya miezi mitano ya mazungumzo ya kurejesha amani Sudan Kusini
yaliyoratibiwa na chama tawala, CCM, hatimaye Rais wa nchi hiyo, Salva
Kiir na hasimu wake, Riek Machar wamesaini makubaliano ya kusitisha
mapigano, yaliyoibuka tangu mwaka 2011.
Kutokana na machafuko hayo, zaidi ya raia 20,000 wa Sudan Kusini,
wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni moja wakikosa makazi.
Walisaini makubaliano hayo juzi usiku jijini hapa, huku marais wa
ndani na nje ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, wakishuhudia.
Wengine walioshuhudia makubaliano hayo ni Rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta, Naibu Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa , Rais wa
Uganda, Yoweri Museveni, Salva Kiir, Riek Machar na Makamu wa Rais wa
Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
CHANJO DHIDI YA EBOLA KUWASILI LIBERIA
Chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola iko njiani kuelekea nchini Liberia.
Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo hii kupelekwa kwenye nchi iliyoathiriwa zaidi na Ebola.
Lakini
Wataalamu wanasema, wakati huu maambukizi ya Ebola yakiwa
yanapungua, itakuwa vigumu kubaini kama chanjo hii inatoa kinga dhidi ya
Virusi vya ugonjwa huo.
Chanjo hii ilitengenezwa na Kampuni moja ya Uingereza, GlaxoSmithKline (GSK )na Taasisi ya kitaifa ya afya nchini Marekani. GSK imesema ndege iliyo na dozi za awali takriban 300 za chanjo inatarajiwa kufika Monrovia siku ya ijumaa.
Kampuni ina matumaini mtu wa kwanza kujitolea atapata chanjo hiyo wiki chache zijazo.
Wanasayansi wanalenga kuwahusisha watu watakaojitolea takriban 30,000 katika majaribio hayo wakiwemo wafanyakazi wa afya. Ikiwa taratibu zote zitafuatwa, Watu 10,000 watapatiwa chanjo ya GSK.
Idadi hiyohiyo ya watu watapata chanjo aina ya Placedo ,na wengine 10,000 chanjo nyingine ya majaribio. Matokeo yatalinganishwa ili kubaini kama kuna chanjo yeyote kati ya hizo imefanya kazi dhidi ya Virusi vya Ebola.
Majaribio kama hayo tayari yalifanyika kwa wafanyakazi wa afya 200 waliojitolea nchini Uingereza, Marekani, Switerland na Mali.
Shirika la GSK limesema chanjo hizo zimeleta matokeo chanya. Lakini ni kwa nchi zilizoathirika pekee ambapo wataalamu watasema kama inatoa kinga thabiti.
Kampuni
inasisitiza kuwa Chanjo bado iko katika uboreshwaji na Shirika la Afya
duniani, WHO na wakaguzi wengine wanakazi ya kuhakikisha kuwa
wanajiridhisha kuhusu ubora na usalama wake kabla ya kampeni za matumizi
ya kinga hiyo .
Chanjo hizo pia zimepangwa pia Guinea, Liberia,na Sierra Leone miezi kadhaa ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
MFALME ABDULLAH WA SAUDIA AFARIKI DUNIA
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa mfalme wa Saudia Abdullah bin Abdulaziz amefariki dunia akiwa hospitalini .
Tamko la kifo cha mfalme huyo zilitolewa na kaka wa mfalme huyo aitwaye , Salman,ambaye naye aliwahi kuwa mfalme.
Kabla
ya tamko hilo television ya taifa la Saudi lilikatiza matangazo yake na
kuweka nyimbo za quraan ,kama ishara ya kifo cha kiongozi wa juu wa
ufalme.
King Abdullah, amefariki dunia akiwa na miaka 90, alilazwa
hospitalini kwa wiki kadhaa tangu December mwaka wa jana kutokana na
maambukizi kwenye njia ya hewa.
Mfalme huyo aliingia madarakani mwaka 2005 lakini alikuwa ni dhaifu mwenye kushambuliwa na maradhi mara kwa mara. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
MWAMUZI YANGA, RUVU AFUNGIWA
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe
SIKU moja baada ya Klabu ya Yanga kulalamika kudhalilishwa kwa
mchezaji wake, Amisi Tambwe katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting,
Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemwondoa
kuchezesha mechi za Ligi Kuu mwamuzi wa pambano hilo kwa kushindwa
kulimudu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Chama,
mwamuzi huyo Mohammed Theofil ameondolewa kuchezesha ligi hiyo ya
Tanzania Bara kwa kipindi kilichobaki.
Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa
Dar es Salaam na kusimamiwa na mwamuzi huyo wa kati, timu ya Ruvu
Shooting ilionesha mchezo wa kibabe ambapo baadhi ya wachezaji wake
walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu pasipo kuadhibiwa.
Mchezo huo ulisababisha mshambuliaji wa Yanga, Tambwe ambaye ni raia
wa Burundi, kulalamika kwamba alidhalilishwa, huku akidai kuumizwa
baadhi ya maeneo ya mwili wake na akidai kuwa aliitwa mkimbizi.
Lakini akizungumza jana akiwa jijini Mwanza, Chama ambaye pia ni
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Katibu wa Chama cha Soka Kagera,
alithibitisha kuondolewa kwa mwamuzi Theofil. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ARSENE WENGER "VIBALI VYA KAZI VIFUTWE"
Meneja
wa Arsenal Arsene Wenger ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya
kazi kwa ajili ya wachezaji ambao hawamo kwenye umoja wa ulaya zifutwe.
Wenger
anaejaribu kumsajili Gabriel Paulista kutoka Villarreal ambae anahitaji
kibali cha uidhinisho toka nchini kwake sababu hajawahi kulitumikia
taifa lake.
Bosi huyo amekosoa mpango wa mapendekezo ya kupunguza
idadi ya wachezajitoka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa Ulaya wenye
pasipoti katika michezo ya ligi ya England msimu ujao.
Akasema "Kusema ukweli inapaswa funguliwa kabisa, na kila mtu anaweza kungia"
Kwasasa
kibali cha kufanyia kazi kwa nchi zisizo umoja wa Ulaya kunahitajika
kuwa katika nafasi 70 za juu katika ubora wa viwango vya Fifa na awe
amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa ndani ya miaka miwili.
"Ili kumsajili Paulista tungeweza kuwashawishi maofisa wa kwao kuwa ni beki wa kipekee mwenye kipaji."
Chama
cha Soka cha Englan kinataka kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua
wenyeji wa jumuiya ya ulaya kufikia asilimia 50 kwenye ligi. Lakini Wenger anadhani kuondoa kanuni itakuwa bora kwa ajili vijana wachezaji Kiingereza.
"kufunga mipaka ya nchi na kuruhusu kucheza wachezaji wa Kiingereza tu Nini kitatokea? Ni kuua mvuto wa ligi dunia kote. Wenger alisema Arsenal walitaka kumsajili winga wa kimataifa wa Ajentina Angel Di Maria lakini kibali cha kazi kikaleta shida.
Wenger aliongeza "Tulimtambua Di Maria alipokuwa 17.Tulimuona akiwa katika mashindano ya kimataifa na tulitaka aje hapa.
"Lakini
alikwenda Ureno, na kutoka Ureno alikwenda Hispania. Kwa nini? Kwa
sababu hakuweza kupata kibali cha kufanya kazi England. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
TETESI ZA USAJILI: DE GEA KUUZWA?
Mustakabali
wa kipa David de Gea kusalia Manchester United upo shakani baada ya
wakala wake Jorge Mendes kushindwa kuwakatalia Real Madrid mpango wa
kumsajili.
Manchester United inajianda kutoa ofa kwa timu ya
Villarreal ili kumpata kumpata beki Gabriel Paulista, raia wa Brazil
ambae yuko kwenye mazungumzo na Arsenal.
Klabu ya Chelsea iko katika mipango ya kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa.
Bosi
wa West Brom Tony Pulis imethibitisha kuhitaji kuwasajili winga wa
Wigan Callum McManaman na kiungo Darren Fletcher toka Man United katika
dirisha hili la usajili.
Timu ya QPR imetoa ofa ya kumsajili mshambuliji wa zamani Ac Milan Alexandre Pato,anayechezea timu ya Sao paul kwa mkopo.
Meneja
wa Swansea City Garry Monk anavutiwa na mpango wa kumsajilibeki wa
kushoto wa Norwich Martin Olsson, mwenye miaka 26,pamoja na kiungo
Alexandru Maxim toka Stuttgart
Meneja wa Liverpool Brendan
Rodgers anatarajia winga wake Raheem Sterling, atasaini mkataba wa muda
mrefu kusalia klabu hapo siku chache zijazo. Manchester City wameulizia uwezekano wa kumpata mshambuliaji Jay Rodriguez wa timu ya Southampton.
Hull City wanamfuatilia winga wa Tottenham timu Taifa ya England Aaron Lennon,ambae anataka kuondoka White Hart Lane kwa kukosa namba kikosi cha kwanza.
Kiungo wa zamani wa Chelsea Kevin de Bruyne,amekata kurejea katika ligi ya England kwa kusema havutiwi kurudi katika ligi pamoja na kwepo taarifa za kuwaniwa na Arsenal na Manchester United.
Klabu ya Roma inajaribu kiwashawishi Chelsea kukubali pauni 380,000 ili kumchukua winga Mohamed Salah kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Hull City wanamfuatilia winga wa Tottenham timu Taifa ya England Aaron Lennon,ambae anataka kuondoka White Hart Lane kwa kukosa namba kikosi cha kwanza.
Kiungo wa zamani wa Chelsea Kevin de Bruyne,amekata kurejea katika ligi ya England kwa kusema havutiwi kurudi katika ligi pamoja na kwepo taarifa za kuwaniwa na Arsenal na Manchester United.
Klabu ya Roma inajaribu kiwashawishi Chelsea kukubali pauni 380,000 ili kumchukua winga Mohamed Salah kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Thursday, January 22, 2015
MAFURIKO MTWARA, NYUMBA 200 ZAZINGIRWA NA MAJI
Wakazi wa Mtaa wa Kiangu Manispaa ya Mtwara Mikindani wakipita kwenye
maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji
katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kufuatia mvua zinazoendelea
kunyesha na kusababisha hasara kubwa ambayo thamani yake bado
haijajulikana.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima
Dendegu ametoa saa 24 kwa wataalam kuhakikisha wanayaondoa maji ndani
ya makazi ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilaman Ndile amemwambia
mkuu huyo wa mkoa alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo
kuwa zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika mitaa mbalimbali ya
manispaa hiyo.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza
maisha kutokana na mafuriko hayo lakini kumetokea uharibifu mkubwa wa
mali na vyakula.
“Mvua kubwa zilizonyesha jana usiku
zimeshababisha mafuriko haya…tatizo kubwa mji wetu hauna mifereji ya
kupeleka maji baharini…athari ni kubwa sana,” alisema Ndile.
Aliongeza kuwa “Mitaa ya Magomeni, Chuno, Kiangu, Skoya,Kisutu Nabwada ndiyo yaliyoathiriwa zaidi na tatizo hili”
Alia Mussa ni mmoja wa waathirika wa mafuriko hayo
kutoka Mtaa wa Kisutu eneo la Nabwada alisema kuwa amepoteza fedha
kiasi cha Sh300,000, nguo, chakula na vyombo vya ndani.
“Tunaomba msaada kwa viongozi kunusuru hali hii,
tunaona serikali yetu kama imetutupa, hatuna chakula, wala fedha za
kununua chakula, kila kitu kimeloa,” alisema Mussa.
Dendegu amewaagiza wataalam wa mipango miji,
zimamoto na manispaa kuhakikisha ndani ya saa 24 wanayaondoa maji hayo
katika ya makazi ya watu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)