Marekani imetangaza kwamba
imetuma kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia kuwatafuta
wasichana takriban 200 wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na
wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa
wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja
ili kulikomesha Boko Haram.Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kutumia utekeji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana na kuangamiza Boko Haram.
Nchini Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake, Daktari Reuben Abati.
"msaada huo kutoka kwa Rais Obama uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni John Kerry kama saa tisa alasiri hivi," Daktari Abati alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo BBC