Monday, May 05, 2014

HUKUMU YA WANAJESHI WABAKAJI DRC LEO

Wanajeshi wa serikali ya DRC
Hukumu inatarajiwa kutolewa baadaye leo kwenye kesi inayowahusu wanajeshi 39 wanaotuhumiwa kuendesha ubakaji na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kusababisha machafuko yanayoendelea kwenye mji mdogo wa Minova ulio mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2012.
Waasi wa M23 ambao wanadaiwa nao kujihusisha na vitendo vya ubakaji
Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.
Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale serikali. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...