Monday, May 05, 2014

MAPIGANO MAKALI YAANZA TENA SUDAN KUSINI

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika mji wa Bentiu nchini Sudan Kusini ambapo vikosi vya serikali vinajaribu kuurejesha mji huo uliotekwa na waasi.
Mwandishi wa Habari wa BBC aliyeandamana na kikosi cha Umoja wa Mataifa nje ya mji huo anasema amesikia milio ya bunduki na silaha nzito nzito ambapo pia ameona kikosi cha majeshi ya serikali kikijipanga.
Hata hivyo amesema bado haijajulikana ni kundi gani kwa sasa linaloshikilia mji huo wa wenye utajiri wa mafuta.
Kwa upande serikali nchini Sudan kusini inasema majeshi yake yameudhibiti mji wa huo na ngome ya waasi ya Nasir.
Baadhi ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbia makazi yao hivi karibuni kutokana na vita
Mjumbe wa Umoja wa mataifa mjini humo anasema mji huo umedhibitiwa upya na kikosi cha serikali katika operesheni kubwa iliyoanza hapo jana Jumapili.
Shambulio hilo linajiri siku mbili baada ya rais Salva Kiir kumwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja na kiongozi wa waasi, Riek Machar. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...