Saturday, May 03, 2014

MWENGE WA UHURU WAWASHWA RASMI JANA MKOANI KAGERA,TAYARI KUKIMBIZWA KATIKA WILAYA 127

 Makamu wa Rais wa, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera jana. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz


 Wakimbiza Mwenge kitaifa wakikimbiza Mwenge wa Uhuru kuelekea nje ya Uwanja wa Mpira wa Kaitaba tayari kuanza ziara ya kukagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispa ya Bukoba.
 Watu mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
 Watoto wa Haraiki wakionyesha michezo mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo mjini Bukoba.
Baadhi ya watoto wakifuatilia matukio mbalimbali wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru bila kujali mazingira yaliyopo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...