Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa akiwa katika matembezi ya kupinga mauaji ya albino.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowasa, jana alithibitisha kwa vitendo kuwa afya yake iko safi baada ya kutembea umbali wa kilomita tano kwa miguu kwenye matembezi ya kupinga mauaji ya albino nchini.
Kwa muda mrefu, Lowassa ambaye ni mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, amekuwa akidaiwa kuwa na matatizo ya afya na kuwa hawezi kuhimili mikimiki ya kampeni na shughuli nyingine zinazohitaji nguvu.
Lakini matembezi ya jana yaliyoongozwa na Lowassa kuanzia Uwanja wa Taifa wilayani Temeke mpaka viwanja vya TCC Chan’gombe na kutumia dakika 25, yamedhihirisha vinginevyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.