Wednesday, January 14, 2015
GAZETI LENYE KIBONZO CHA MTUME LAUZWA TENA...!!!
Gazeti
la Charlie Hebdo leo limeanza kusambaza toleo la gazeti lake ambalo
limechapishwa kibonzo cha Mtume Mohammad kwenye ukurasa wake wa mbele.
Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka.
Picha ya kibonzo hicho iliyopo ukurasa mbele wa gazeti hilo inamwonyesha Mtume Mohammad akilia.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa picha hiyo itachochea chuki.
Hata
hivyo waandishi wa habari wa gazeti hilo wanasema ukurasa wa mbele
unamaanisha Waandishi wa habari wamewasamehe waliotekeleza shambulizi la
kigaidi lilolofanyika jumatano wiki iliyopita.
Naibu Mhariri wa
Gazeti la Liberalation Alexandra Schwatzbrod anasema ulikuwa uamuzi
mwepesi kwa gazeti lake kuchapisha picha ya kibonzo hicho. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ONGWEN AKABIDHIWA KWA WANAJESHI WA UGANDA
Kamanda
mkuu wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda, aliyejisalimisha wiki
jana, Dominic Ongwen , amekabidhiwa kwa wanajeshi wa Uganda walio katika
Jamuhuri ya Afrika ya kati.
Muasi huyo, Dominic Ongwen,
anasemekana kuwa naibu kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony na alikamatwa
na wanajeshi wa Marekani wiki jana ingawa waasi wa Seleka wanasema wao
ndio waliomkamata. Waasi hao walisema kwamba walimkatama Ongwen baada ya makabiliano ya muda ingawa jeshi la Marekani lilisitiza kuwa alijisalimisha na tangu hao wamekuwa wakimzuilia.
Uganda imesema kwamba itamkabidhi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, ambako anatakikana kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Kundi la LRA liliwateka nyara wasichana na wavulana huku wavulana wakilazimishwa kuwa wapiganaji na wasichana wakifanywa watumwa wa ngono.
Ongwen pamoja na Joseph Kony wanatakikana na mahakama ya ICC kujibu tuhuma za kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Je Ongwen ni nani?
-Inaarifiwa alitekwa nyara na waasi wa LRA akiwa na umri wa miaka 10 wakati alipokuwa anaelekea shuleni Kaskazini mwa Uganda.
-Miaka iliyofuata, alipanda ngazi na kuwa kamanda
-Anatuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo, kuwatumia watoto kama watumwa.
-ICC ilitoa kibali cha kumkamata mnamo mwaka 2005.
-Kuliwa na madai kwamba aliuawa katika mwaka 2013 ambapo Marekani ilitangaza ahadi ya zawadi kwa yeyeote mwenye taarifa kumhusu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
AVULIWA NGUO KUTHIBITISHA JINSIA YAKE
Genoveva
Anonma alidhalilishwa,kwa takriban miaka minne,amekuwa akihisiwa kuwa
si mwanamke naye amekuwa akizidharau tuhuma hizo mara kwa mara.
Lakini
kuna kitu ambacho hakukitegemea kilichokuwa kinamuandama kufuatia uwezo
wake michezoni alipokuwa Equatorial Guinea mwaka 2008 katika michuano
ya soka la wanawake wa mataifa ya Afrika.Goli lake la ushindi katika ardhi ya nyumbani,na timu yake kuwa ya kwanza wakiifuatia Nigeria ,ambayo iliibuka kuwa washindi wa jumla,Anonma badala ya kuhesabika kuwa mkombozi na mwenye kuitimiza ndoto yake michezoni, badala yake amebaki njia panda.
Anonma awapo uwanjani huwa ana haha uwanjani huku na kule na nguvu alo nayo,timu pinzani humbeza kuwa hawezi kuwa mwanamke bali wanacheza na janadume,na ndipo sasa kituko kikaja kutokana na tuhuma hizo shirikisho la soka barani Africa walichagua njia ya kuhakiki jinsia ya Anonma. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KOCHA NOOIJ KUTAJA STARS MABORESHO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart
Nooij anatarajia kutaja kikosi cha Maboresho kitakachoingia kambini
Januari 18 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda
itakayofanyika Januari 22 mwaka huu jijini Mwanza.
Nooij atataja kikosi hicho kwenye
mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Januari 15 mwaka
huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Uwanja wa Karume. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER
Timu
ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) imepangiwa
kucheza na Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa ajili
ya fainali za Afrika ambapo michuano hiyo itafanyika Aprili mwaka huu
nchini Shelisheli.
Mwenyekiti wa Kamati ya Beach Soccer, Ahmed Idd
Mgoyi amesema jijini Dar es Salaam, kuwa Tanzania itaanzia ugenini
ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwaka huu
nchini Kenya.Mechi ya marudiano itafanyikaa Tanzania kati ya Februari 20 na 22 mwaka huu. Iwapo timu ya Tanzania itasonga mbele, katika raundi ya pili itacheza na Misri ikianzia nyumbani kati ya Machi 13 na 15 mwaka huu.
Mgoyi alisema maandalizi ya Tanzania kushiriki kwenye mashindano hayo yameanza ambapo timu ya Tanzania Bara itacheza na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kupata kikosi kimoja kitakachoingia kwenye michuano hiyo ya Afrika.
Benchi za ufundi la timu ya Tanzania litaongozwa na John Mwansasu wakati Msaidizi wake ni Ali Shariff 'Adolf' kutoka Zanzibar, na Meneja wa timu hiyo ni George Lucas. Wote hao walishiriki kwenye kozi ya ukocha wa beach soccer iliyoendeshwa mwaka jana nchini na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kocha Mwansasu atatangaza timu ya Tanzania Bara, Januari 19 mwaka huu, na mazoezi ya pamoja na timu ya Zanzibar yatafanyika Januari 24 na 25 mwaka huu.
Wachezaji wa timu ya Tanzania Bara watatokana na michuano ya beach soccer iliyofanyika mwaka jana ikishirikisha timu za vyuo vya elimu ya juu vya Mkoa wa Dar es Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Tuesday, January 13, 2015
"WALIOJITOKEZA KUWANIA URAIS CCM HAWANA SIFA" KINGUNGE
Harakati za
kuwania urais ndani ya CCM zimeingia katika hatua mpya baada ya
mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale - Mwiru kuibuka na kudai kuwa wote
waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha
kutaka kuingia Ikulu.
Kauli ya mwanasiasa huyo ambayo imekuja siku moja
kabla ya Kamati Kuu ya CCM kukutana leo mjini Unguja na moja ya ajenda
ikitajwa kuwa suala la maadili, inaweza kuwa mwiba mchungu kwa wanasiasa
hao ambao wanaongezeka kila kukicha.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kingunge alisema:
“Kuna suala la kukosa uadilifu, kuna suala la matumizi ya pesa na
nikwambie ukweli, hao wanaotangaza urais wote wanatumia pesa, wanatumia
faulo mbalimbali na wananchi wanajua.” Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
AFRIKA YAJIFUNGULIA MTANDAO WAKE WA AFRILEAKS
Mtandao
mpya mfano ule wa Wiki Leaks , unaolenga kutangaza visa vya ufisadi
umezinduliwa barani Afrika. Mtandao huo kwa jina 'Afri Leaks' unanuiwa
kutumiwa kulinganisha na kutangaza wazi visa vya ufisadi katika bara
nzima.
Kile Afrileaks inaahidi ni mfumo wa hali yajuu wa kama
posta mtandaoni ambapo mtu anaweza kuutumia kufichua habari za siri
lakini muhimu kwa jamii bila wao wenyewe kujulikana.Mwenye habari nyeti ataweza kuzipeleka kwa vyombo vya habari kote barani Afrika ambavyo wamejiridhisha navyo kwamba viko huru na wana uhariri wa hali ya juu unaotambulika kimataifa.
Mojawapo ya Maswala yanayowakera wengi ambayo huenda yakapata kuchipuliwa kwa wingi iwapo mfumo huo wa Afrileaks utafana , ni kashfa za ufisadi.
Licha ya kuwa na viwango vya kuridhisha vya ukuaji wa uchumi,Mataifa mengi ya Afrika hata yale yaliyo na utulivu wa kisiasa hupoteza mabillioni ya fedha kila mwaka kutokana na ufisadi uiokithiri, huku taasisi hafifu zikibuniwa bila kuwa na nia ya dhati ya kukabiliana na rushwa. .
Shirika hilo la Afrileaks linasisitiza kuwa halitachapisha habari zozote za kibanfsi za mfichua siri.
Na kwamba lengo lao ni kuwaunganisha wenye taarifa muhimu na waandishi habari wanaoandika makala zilizopelelezwa na kuchunguzwa kwa kina. Pia wameahidi kutoa mafunzo zaidi kwa waandishi habari waliobobea ili kufahamu vyema vipi kuzishughulikia taarifa kama hizo.
Mashirika kadhaa ya habari barani Afrika tayari yameshajisajili na Afrileaks -ikiwemo kutoka nchini Zimbabwe, Mozambique, Angola na Botswana.
Hivyo wenye habari nyeti ambazo alikuwa anatafuta kwa kuzipeleka bila kutambuliwa anahimizwa kuziwasilisha kwa tovuti hiyo ya Afrileaks lakini wanapaswa kufuata utaratibu uliowekwa na wala wasitumie computer za ofisini mwao ili kutotambulika na kujiweka katika hatari.
Je nani atakuwa wa kwanza kujitosa na habari moto moto katika Afrileaks! Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC Swahili
KAMANDA WA LRA KUFIKISHWA ICC
Kamanda
wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda ambaye alijisalimisha katika
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Dominic Ongwen atakabidhiwa kwa mahakama ya
kimataifa ya ICC, yasema serikali ya Uganda.
Kamanda huyo ni
miongoni mwa watu wa kundi la LRA wanaosakwa na viongozi wa mashitaka
katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kutenda uhalifu dhidi ya
binadamu.Waasi wa Seleka walioko katik Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako Ongwen alikamatwa walisema kuwa muasi huyo alikamtwa ingawa wanajeshi wa Marekani wanasema kuwa alijisalimisha.
Msemaji wa jeshi la Uganda, ameambia shirika la habari la Reuters kwamba Ongwen atakabidhiwa ICC na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako alijisalimisha.
Ongwen alikabidhiwa wanajeshi wa Marekani wiki jana na bado anazuiliwa na wanajeshi hao.
Marekani ilikuwa imeahidi kutoa kitita cha dola miliono 5 kama zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa kamanda huyo, kuhamishwa kwake na hatimaye kufunguliwa mashitaka.
Maafisa wakuu nchini Uganda wanasema kwamba Ongwen atapelekwa nchini Uganda katika siku chache zijazo.
Anajaulikana kwa jina "White Ant", jina lake la msituni na yeye ndiye naibu kamanda wa kundi la LRA Joseph Kony ambaye pia anasakwa na mahakama ya kimataifa ya ICC.
Kundi la LRA liliwateka nyara maelfu ya watoto na kuwalazimisha kupigana huku wasichana wakifanywa watumwa wa ngono. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Thursday, January 08, 2015
NAIBU WAZIRI AZOMEWA MCHANA KWEUPEEE...!!!
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga akisindikizwa na Polisi kutoka katika Ukumbi wa Arnautoglu Dar es Salaam jana, baada ya mafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kumzonga alipokwenda kuhudhuria hafla ya kuapishwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.
Wakati utata
ukizidi kujitokeza katika uapishaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa
Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na waliodaiwa kushinda kuwekwa kando na
kuapishwa walioshindwa, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro
Mahanga jana alikumbana na zomeazomea hadi kulazimika kuondoka kwenye
Ofisi za Manispaa ya Ilala, Arnatouglou ambako shughuli hiyo ilikuwa
ikifanyika.
Dk Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Segerea (CCM),
alizomewa akitakiwa kuondoka katika eneo hilo, akidaiwa kwamba
angebadilisha matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa chama chake.
Eneo hilo lilijaa wafuasi wa Chadema, CUF na CCM
huku kila kundi likiwa limesindikiza wenyeviti wake kuapishwa katika
shughuli ambayo ilifanyika kwa awamu tatu kwa kila jimbo; Segerea, Ilala
na Ukonga kupewa saa mbili.
Waziri Mahanga aliwasili wakati wa zamu ya Segerea
saa saba mchana, ndipo kundi la mashabiki wa upinzani lilipoanza
kumzomea na kuimba nyimbo za kumkashifu na kutaka atoke katika ukumbi
ulioandaliwa kwa ajili ya kuwaapisha wenyeviti. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ESCROW YAWANG'OA WAFANYAKAZI 7 TRA
Wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi ikiwa ni
mwendelezo wa utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge kuhusu ripoti ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu kashfa hiyo.
Wengine ambao tayari wameshawajibika katika kashfa
hiyo ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
aliyejiuzulu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Tibaijuka aliyefukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi aliyesimamishwa kupisha
uchunguzi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
POLISI UFARANSA WATOA PICHA ZA WASHUKIWA
Polisi
wa Ufaransa wametoa majina na picha ya washukiwa wawili waliohusika na
shambulio katika ofisi za jarida la vibonzo nchini humo.
Polisi wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye silaha.Cherif Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iraq.
Vyombo vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea, ambako watu 12 waliuawa.
Uchunguzi mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
UN KUSHIRIKIANA NA DRC KUWAONDOA FDLR
Umoja
wa Mataifa umesema Rais Joseph Kabila ameahidi kuwa jeshi lake
litaungana na la UN katika operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.
kikosi
cha wanajeshi elfu 20 wa umoja huo watashirikiana na wale wa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo katika kampeni zilizopangwa kuanza karibuni dhidi
ya waasi wa Kihutu wa Rwanda.Wanamgambo wa Kihutu, wanaojulikana kama FDLR, wamekuwa wakilitumia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama kambi yao ya kufanya mnashambulizi dhidi ya serikali ya nchi jirani ya Rwanda.
Waasi hao wameshindwa kufikia muda wa mwisho wa kimataifa uliowekwa wiki hii wa kuweka silaha chini na kuondoka katika eneo hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MAREKANI KUPAMBANA NA UKIMWI AFRIKA
Marekani itatoa madawa ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa zaidi ya watoto laki tatu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo.
Nchi
hiyo imetangaza kwamba madawa hayo yatatolewa katika nchi zilizo kusini
mwa jangwa la Sahara, barani Afrika, katika kipindi cha miaka miwili
ijayo.Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wake wa dola milioni mia mbili zilizoandaliwa kwa ajili ya kupambana na virusi vya ukimwi na ukimwi.
Balozi wa Marekani, Deborah Birth amesema mpango huo utalenga pia kuzuia maambukizo ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Umoja wa Mataifa umesema asilimia 95 ya watoto walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi wanaishi katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
Subscribe to:
Posts (Atom)