IPO misemo mingi ambayo huashiria
kutokea kwa jambo liwe nzuri au baya, moja ya misemo hiyo ni ule usemao
dalili ya mvua ni mawingu.
Msemo huu unaweza ukawa na na
maana kubwa hivi sasa kwa golikipa wa timu ya Dar es salaam Young
African, Juma Kaseja ambaye hivi sasa inaonekana hana mawasiliano mazuri
na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani
jijini Dar es salaam.
Mchezaji huyo mwenye heshima
kubwa nchini mwishoni mwa mwaka uliopita aliachwa katika kikosi cha timu
hiyo kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya mapinduzi,
lakini isitoshe jina la Kaseja halijaonekana kwenye orodha ya wachezaji
wa timu hiyo iliyotumwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa ajili
ya ushiriki wa kombe la shirikisho.
Matukio hayo yote yameibua
maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya
mlinda mlango huyo, hatua iliyotufanya tumtafute afisa habari na
mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro kutaka kufahamu kinaga ubaga
kinachoendelea kati ya Kaseja na Yanga..
Muro amesema Kaseja kutohusishwa katika kikosi kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF ni kujitakia mwenyewe.
Jerry Muro.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.