Dereva
wa magari ya langa langa ya Formula 1 Jules Bianchi ametoka katika hali
ya kuwa mgonjwa mahututi na sasa anapua bila msaada wa mashine,
wamesema wazazi wake katika taarifa yao.
Dereva huyo wa timu ya
Marussia mwenye umri wa miaka 25, alijeruhiwa kichwani alipoligonga gari
la kuvuta magari katika michuano ya Japanese Grand Prix Oktoba 5,2014.Dereva huyo raia wa Ufaransa amehamishwa kutoka hospitali ya mjini Yokkaichi nchini Japan na kupelekwa katika hospitali ya Nice nchini Ufaransa kwa uchunguzi zaidi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz