Wednesday, November 19, 2014

MOTO WATEKETEZA SOKO LA BIDHAA ZA UTAMADUNI JIJINI ARUSHA


Baadhi ya Mabaki ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa kuamkia leo. 

Bango la Soko hilo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi. "Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...