Kiongozi
mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na
Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao
umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani.
Wanachama wa Republican
wamepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi wa nusu muhula na kwa
sasa wanadhibiti mabunge yote mawili nchini Marekani. Kiongozi wa
baraza la Senate anayeingia madarakani Mitch McConnell amesema
ataliwezesha baraza hilo kufanya kazi na kupitisha miswada ya sheria.Bwana Obama amesema alikuwa na "hamu ya kufanyakazi na baraza jipya la Congress na kufanya miaka miwili yake aliyobaki kukaa madarakani kuwa na tija kadiri iwezekanavyo".