Friday, October 31, 2014

KIVUMBI CHA LIGI KUU ENGLAND

Golikipa Simon Mignolet wa timu ya Liverpool ashindwa kuupangua mpira.
Kitimtim cha ligi kuu ya England kitaendelea tena kesho wakati ambapo mashabiki wa soka nchini humo na duniani kote watapata nafasi ya kuzishuhudia timu zao zikitafuta pointi tatu muhimu.
Newcastle Utd wataikaribisha Liverpool katika mchezo ambao utarushwa moja kwa moja kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC majira ya saa tisa unusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Arsenal wao wataikaribisha Burnley, huku Chelsea nayo wakiialika QPR. Everton watakuwa nyumbani kucheza Swansea City. Hull City wataikabili Southampton. Michezo mingine ni itakayochezwa siku hiyo ya kesho ni kati ya Leicester City watakapo kwaana na West Brom, Huku Stoke City watakapoikabili West Ham utd.
Siku ya jumapili ni mpambano wa kukata na shoka ambapo Manchester United wataavaana na Manchester City mechi ambayo pia itatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ,huku Tottenham watakapokwaana na Aston villa. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Wednesday, October 29, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 29, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BAN KI MOON KUTEMBELEA KAMBI YA DAADAB

Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatembelea kambi ya wakimbizi ya Daadab, nchini Kenya.
Hii ni mara ya kwanza kwa kingozi huyo mkubwa katika Umoja wa Mataifa kutembelea kambi hiyo kubwa ya wakimbizi.
Ban Ki Moon anatarajiwa kutathmini hali ya msongamano katika kambi hiyo na hali ya usalama ambayo imekuwa ikizorota mara kwa mara.
Aidha ripoti zinasema, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataidhinisha kuondoka kwa baadhi wa wakimbizi wa kisomali waliojitolea kurudi nyumbani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

CHELSEA YAIBUKA KIDEDEA

Didier Drogba
Didier Drogba ameipa ushindi Chelsea wa mabao 2-1 dhidi ya Shrewsbury.
Mchezo huo wa kombe la ligi marufu kama capital one, umechezwa usiku wa kuamkia leo.
Timu kadhaa zilijitupa uwanjani ili kutafuta nafasi ya kuingia robo fainali yaligi hiyo katika ligi hiyo.
Mario Balotelli ametia chachu katika ushindi wa mabao 2-1 iliyoupata Liverpool katik mchezo dhidi ya Swansea City.
Mashabiki wa Fulham nao huenda walilala mapema baada ya kushuhudia timu yao ikipokea kichapo cha magoli 5-2 pale walipoialika Derby.
Bournemouth wakailaza West Brome kwa jumla ya mabao 2-1, huku Sheff Utd ikiibamiza MK Dons kwa ushindi wa mabao 2-1. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, October 18, 2014

'MEYA TABORA AMILIKI BODA BODA 400'


Meya wa Manispaa ya Tabora, Gullam Hussein Dewji akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam jana, baada ya kutoka kwenye Baraza ka Maadili ya Viongozi, alikoitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kujilimbikizia mali na matumizi mabaya ya madaraka. 


Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Tabora, Gulam Hussein Dewji ameshushiwa tuhuma nzito za kuidanganya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushindwa kutangaza mali anazozimikiki zikiwamo pikipiki 422, licha ya kutakiwa kufanya hivyo kisheria.

Sheria Namba 5 ya mwaka 2001 ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inamtaka kila kiongozi kujaza fomu za kutangaza mali zake na madeni na kuziwasilisha kwenye Sekretarieti hiyo kila mwisho wa mwaka.

Meya huyo alisomewa mashtaka yake jana na Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Hamisi Msumi.

Mwanasheria huyo alisema kuwa meya huyo anatuhumiwa kutotamka baadhi ya mali anazozimiliki na kuzitaja mali hizo kuwa ni pikipiki 422, magari matatu, viwanja vitano na nyumba moja.

Cyriacus alisema kwamba meya huyo alishindwa kutangaza mali zake katika kipidi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2010 hadi 2013. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KAMPENI URAIS CCM: NOTI ZAMWAGWA DODOMA


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), wakiwa katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa White House mjini Dodoma juzi na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete. 

Baadhi ya makada wa wa CCM wanaotajwa kuwania urais kupitia chama hicho wanadaiwa kugeuza mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), kuwa sehemu ya kampeni kwa wajumbe wa mkutano huo wakidaiwa kumwaga fedha usiku kucha.

Gazeti hili lilishuhudia kampeni hizo zikifanywa na wapambe wa wagombea hao nje ya Ukumbi wa Nec uliopo nje ya jengo la White House mjini Dodoma na baadhi ya watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo.

Wapambe hao kwa siku mbili za vikao vya Nec vilivyofanyika mjini hapa kuanzia juzi walionekana wakifika mapema, kusalimia, kujitenga katika makundi madogomadogo na wajumbe wa Nec tofauti na vikao vingine vilivyotangulia.

Harakati hizo hazikuishia katika viwanja hivyo, bali hata nje ambapo mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo kutoka Kanda ya Ziwa ameonekana kukutana na makatibu wa CCM katika moja ya hoteli mjini hapa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DK. SHEIN APATA MPINZANI URAIS ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein  
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein, amepata mpinzani iwapo ataamua tena kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwakani, baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Tadea, Juma Ali Khatib (50), kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo visiwani humu.

Mgombea huyo ni watatu kujitokeza hadharani na kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo, baada ya katibu mkuu wa CUF, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kutangaza nia hiyo akifuatiwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed aliyetangaza pia nia hiyo.

Hamad Rashid alitangaza nia na kusema kuwa atawania nafasi hiyo kupitia CUF, mgombea binafsi au kwa tiketi Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

Ikiwa Maalim Seif atawania tena nafasi hiyo, itakuwa ni mara ya tano tangu mwaka 1995, ulipoanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RIPOTI MAALUM: WAFUNGWA WAENDESHA UHALIFU GEREZANI


Pingu za wahalifu

Wakati Serikali ikihaha kukabiliana na vitendo vya uhalifu, imebainika kuwapo kwa mtandao wa uhalifu ambao unawawezesha baadhi ya watu waliofungwa kuratibu matukio ya uhalifu wakiwa gerezani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Uchunguzi wa gazeti hili katika eneo hilo uliojumuisha Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kigoma, umebaini kuwa uhalifu huo unahusisha ujambazi, mauaji ya kukodiwa na ujangili wa wanyamapori na watuhumiwa wanatajwa kuwa ni baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa.

Kutokana na nguvu uliyonayo, mtandao huo umekuwa ukitekeleza vitendo vya uhalifu kwa kufanya mawasiliano na watu wao waliofungwa kifungoni kwa kutumia askari na watendaji wengine wa Serikali wasio waaminifu.

Kwa nyakati tofauti watendaji wakuu wa polisi na magereza katika mikoa hiyo, wamezungumzia hali hiyo na baadhi wakionyesha kukiri kwa kueleza; ‘uhalifu wowote lazima uwe na mtandao na kwamba mtu yeyote anaweza kuwa mhalifu.’ Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UN YATETEA JUHUDI ZA KUAANGAMIZA EBOLA

David Nabarro katikati
Mratibu wa shughuli za Umoja wa mataifa kuhusu ugonjwa wa ebola Davis Nabarro ametetea juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo magharibi mwa afrika.
Bwana Nabbaro alikuwa akijibu shutma kutoka kwa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF lililosema kuwa ahadi za misaada hazijakuwa na mafaniko yoyote katika vita dhidi ya ugonjwa wa ebola.
Ameiambia BBC kuwa mipango iko njiani ya kutoa vitanda 4000 kwa wagonjwa wa ebola ifikiapo mwezi ujao.
Matamshi yake yanajiri baada ya ripoti ya ndani ya shirika la afya duniani inayosema kuwa WHO imeshindwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM KUWAACHIA WANAFUNZI




Wanafunzi wa Chibok waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram

Serikali ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.
Mkuu wa jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.
Kulingana na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad Idris Derby.
Alisema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.
Pia alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, October 17, 2014

CHADEMA WAANZA SAFARI YA KUPINGA KATIBA NCHI NZIMA

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akizungumza kwenye mkutano na waandishi Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed. 

Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuendesha kampeni ya kupinga Katiba Inayopendekezwa kwa viongozi wake wakuu pamoja na wale wa mabaraza yake kufanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
Hatua hiyo imekuja siku tatu, tangu Rais Kikwete autangazie umma wa Watanzania alipokuwa akihutubia kilele cha Mbio za Mwenge mkoani Tabora kwamba Katiba Inayopendekezwa inafaa hivyo kuwataka Watanzania waipigie kura wakati wa mchakato wa kura ya maoni.
Ziara ya Chadema itaanzia katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako itachukua siku 20 ikiongozwa na Baraza la Wanawake (Bawacha), linaloongozwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na baada ya kumaliza, itaanza ziara nyingine ya siku 20 itakayofanywa na Baraza la Vijana (Bavicha).
Dk Slaa alisema CCM wameanza kazi ya kuwataka wananchi kupiga kura ya ‘ndiyo’ na Chadema wanaanza mikutano ya kuwashawishi wananchi kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana’.
Alisema kuanzia Novemba 5 mwaka huu, viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho nao wataanza ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
“Bawacha ndiyo itakuwa timu ya kwanza. Itakwenda Mwanza mjini, Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Busanda, Bukombe, Biharamulo, Muleba, Karagwe, Bukoba Mjini, Chato, Shinyanga Mjini na Maswa Mashariki,” alisema Dk Slaa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA: MSIKURUPUKE KUPITISHA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Picha na Maktaba 

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka Watanzania kutokurupuka kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa imeyaacha kando maoni yao mengi na akawataka waisome kwa makini kabla ya kuikubali au kuikataa.
Akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake Bunda, Mkoa wa Mara, Jaji Warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia Jukwaa lao la Uwazi na Fikra Yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu masuala mbalimbali hasa mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Harrieth, Jaji Warioba aliulizwa na kujibu maswali; anaionaje Katiba Inayopendekezwa na iwapo CCM imemgeuka kwa nini asihame chama?
Akijibu maswali hayo, Jaji Warioba alisema Katiba hiyo haina maoni yote ya wananchi kama Bunge Maalumu lilivyojinadi, bali yamewekwa machache ambayo hata hivyo yamo hata katika Katiba ya sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DIDA, JAJA, WABEBA JUKUMU ZITO YANGA


kipa Deogratius Munishi 'Dida' 

Pambano la watani wa jadi, Yanga na Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam litakuwa mtihani mkubwa kwa nyota watatu wa Yanga kwa sababu tofauti.

Watatu hao ni mshambuliaji, Genilson Santos ‘Jaja’ , kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na kiungo Andrey Coutinho.

Jaja, aliyeibuka shujaa ghafla alipoitungua Azam kwa mabao mawili kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, kisha akapoteza makali tangu Ligi Kuu ianze,  ana deni kubwa kwa mashabiki wenye matumaini kwake kuwa atafungua akaunti ya mabao dhidi ya Simba.

Makali yake ya Septemba 14 alipoisulubu Azam yaliyomkatia tiketi ya kuwa kipenzi cha mashabiki na  yanaweza kuongezeka au kufutika.

Mbrazili huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga, ingawa pia anaweza kuwa na wakati mgumu kesho kuthibitisha uwezo wake, kutetea nafasi yake kwenye kikosi  cha kwanza, akishindwa kuisaidia Yanga kuchomoza na ushindi, itakuwa tiketi yake ya kusahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

DSC04323
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...