Pambano la watani wa jadi, Yanga
na Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam litakuwa mtihani
mkubwa kwa nyota watatu wa Yanga kwa sababu tofauti.
Watatu hao ni mshambuliaji, Genilson Santos ‘Jaja’ , kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na kiungo Andrey Coutinho.
Jaja, aliyeibuka shujaa ghafla alipoitungua Azam
kwa mabao mawili kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, kisha akapoteza makali
tangu Ligi Kuu ianze, ana deni kubwa kwa mashabiki wenye matumaini
kwake kuwa atafungua akaunti ya mabao dhidi ya Simba.
Makali yake ya Septemba 14 alipoisulubu Azam
yaliyomkatia tiketi ya kuwa kipenzi cha mashabiki na yanaweza
kuongezeka au kufutika.
Mbrazili huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga,
ingawa pia anaweza kuwa na wakati mgumu kesho kuthibitisha uwezo wake,
kutetea nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza, akishindwa kuisaidia
Yanga kuchomoza na ushindi, itakuwa tiketi yake ya kusahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Dida na rekodi za Kaseja, Barthez
Msimu uliopita, kipindi kama hiki, Mustapha Ali
‘Barthez’ alikuwa kipa nambari moja, akisaidiana na Dida, lakini baada
ya mchezo wa watani uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3, aligeuka adui
kwa mashabiki.
Kipa huyo alipotea kwenye ramani ya klabu hiyo,
akikosa namba kwenye kikosi hicho, nafasi yake ilichukuliwa na mkongwe,
Juma Kaseja aliyekuwa amesajiliwa.
Kaseja, au ‘Tanzania One’ kwa miaka mingi
hakutamba kwani kibarua chake cha kwanza kabla ya mzunguko wa pili wa
ligi kuanza, kilikuwa ni mechi dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Nani
Mtani Jembe aliporuhusu mabao rahisi na Yanga kufungwa 3-1.
Ndipo Kaseja alipoingia kwenye matatizo baada
kujaribu kumpiga chenga Awadh Juma, alishindwa na kusababisha bao la
tatu, huo ukawa mwisho wake na mwanzo wa kuwekwa benchi na nafasi yake
kukabidhiwa kwa Dida, ambaye ujio wa Kaseja ulionekana kumtupa kwenye
chaguo la tatu.
Hivyo, mtihani kwa Dida ni kulinda vyema lango la
Yanga kwa umakini, kusahau masaibu ya watangulizi wake, walioponzwa na
matokeo ya mechi dhidi ya Simba.
Ni kawaida, Yanga inaposhindwa kutamba kwa Simba, kipa mmoja huonja benchi au kutimuliwa.
Kwa staili hiyo, Dida akishindwa kufanya makubwa kwenye mchezo
wa kesho, anaweza kuishia benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Kaseja au
Barthez.
Naye Coutinho, aliyefunga bao la mkwaju wa adhabu
ndogo dhidi ya Prisons katika ushindi wa mabao 2-1 wa Ligi Kuu, amekuwa
hafanyi mambo makubwa kulinganishwa na mategemeo ya mashabiki. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Hilo, linamweka kwenye mtihani dhidi ya Simba, ambayo imesheheni kwenye kiungo, ingawa ukuta una nyufa.
Mtoto kipa Yanga kuidakia Simba
Kuumia kwa wazoefu, Ivo Mapunda na Hussein Shariff
kuinaifanya Simba ibaki na kipa mmoja mwenye uhakika wa asilimia 100
kucheza kesho. Huyo ni mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga, Peter Manyika.
Manyika Peter alijiunga Simba kabla ya msimu huu
na hajadaka mechi yoyote ya ligi, lakini anategemewa kulibeba jukumu
hilo zito. Huo ni mtihani wake wa kwanza ambao utamvusha au kumwangusha
kinda huyo.
Vikosi vinatarajiwa kuwa:
Kocha Marcio Maximo anaweza kuwapanga; Deogratius
Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Said Makapu, Rajabu Zahir,
Mbuyu Twite, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Genilson Santos ‘Jaja’,
Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.
Mabeki chipukizi, Said Makapu na Rajabu Zahir
wanaweza kurithi nafasi za wakongwe, Kevin Yondani na Nadir Haroub
‘Cannavaro’ wanaosumbuliwa na majeraha.
Kikosi cha Simba iliyokuwa Afrika Kusini kinaweza
kuwa: Manyika Peter, William Lucian, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’,
Joseph Owino, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’,
Shaaban Kisiga, Amissi Tambwe, Emmanuel Okwi, Haroun Chanongo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment