Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed
Shein, amepata mpinzani iwapo ataamua tena kugombea nafasi hiyo katika
uchaguzi mkuu ujao mwakani, baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Tadea,
Juma Ali Khatib (50), kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo visiwani
humu.
Mgombea huyo ni watatu kujitokeza hadharani na
kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo, baada ya katibu mkuu wa CUF,
ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad,
kutangaza nia hiyo akifuatiwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed
aliyetangaza pia nia hiyo.
Hamad Rashid alitangaza nia na kusema kuwa
atawania nafasi hiyo kupitia CUF, mgombea binafsi au kwa tiketi Chama
cha Alliance for Democratic Change (ADC).
Ikiwa Maalim Seif atawania tena nafasi hiyo,
itakuwa ni mara ya tano tangu mwaka 1995, ulipoanza mfumo wa vyama vingi
mwaka 1992. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika
mwaka 1995, ambapo Seif alishindwa kwa mara ya kwanza na Dk Salmin Amour
Juma wa CCM huku mara mbili akichuana na Dk Amani Karume na kushindwa
pia.
Katika maelezo yake kuhusu hatua hiyo, Khatib
alisema amechukua uamuzi huo kutokana na matatizo yanayowakabili
wananchi wa Zanzibar.
“Matatizo ya Wazanzibar ndiyo yaliyonisukuma
kuchukua fomu ya urais wa Zanzibar. Huduma za jamii zimezorota,
kuongezeka kundi la vijana wasio na ajira mitaani, wazee kuishi
mazingira magumu na ongezeko la ombaomba visiwani Zanzibar,”alisema.
Alisema pamoja na Serikali ya Umoja wa Kitaifa
(SUK), kuundwa Zanzibar miaka minne iliyopita, utendaji wa Serikali
katika kuutumikia umma hauonekani.
“Rais anahitaji kuangalia upya viongozi na
watendaji aliowateua na kuwapa majukumu. Nafikiri wameshindwa kubuni
mipango ya kuwatumikia watu. Utendaji wa watu wanaomsaidia haujengi
taswira halisi, baadhi yao wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo,”
alisema Khatib.
Alisema pamoja na kuwepo sheria nzuri,
kumekosekana utashi na usimamizi makini, juhudi na dhamira ya wazi na
kutokuwepo utendaji unaotarajiwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment