Wakati Serikali ikihaha kukabiliana
na vitendo vya uhalifu, imebainika kuwapo kwa mtandao wa uhalifu ambao
unawawezesha baadhi ya watu waliofungwa kuratibu matukio ya uhalifu
wakiwa gerezani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Uchunguzi wa gazeti hili katika eneo hilo
uliojumuisha Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kigoma,
umebaini kuwa uhalifu huo unahusisha ujambazi, mauaji ya kukodiwa na
ujangili wa wanyamapori na watuhumiwa wanatajwa kuwa ni baadhi ya
wafanyabiashara na wanasiasa.
Kutokana na nguvu uliyonayo, mtandao huo umekuwa
ukitekeleza vitendo vya uhalifu kwa kufanya mawasiliano na watu wao
waliofungwa kifungoni kwa kutumia askari na watendaji wengine wa
Serikali wasio waaminifu.
Kwa nyakati tofauti watendaji wakuu wa polisi na
magereza katika mikoa hiyo, wamezungumzia hali hiyo na baadhi
wakionyesha kukiri kwa kueleza; ‘uhalifu wowote lazima uwe na mtandao na
kwamba mtu yeyote anaweza kuwa mhalifu.’ Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Wafungwa kuendesha uhalifu inawezekana. Inaweza
kusababishwa na aina ya rushwa, wapo wafungwa wenye akili pengine zaidi
ya askari, wakaweza kuwashawishi pia wanawatumia,” alisema Mkuu wa
Gereza Kuu la Butimba mkoani Mwanza,
Jail Mwamgunda. Katika mahojiano maalumu ofisini
kwake hivi karibuni Mwamgunda alisema: “Utandawazi unachangia hayo,
wakati sheria nyingi zimepitwa na wakati na vitendea kazi bado siyo vya
kutosha.
Yapo mawasiliano, zamani ilikuwa barua, sasa simu
za mkononi, televisheni ni vigumu kuvidhibiti. Shida hasa ipo kwa
wafungwa na mahabusu wanaotoka kwenda nje ya magereza na kurejea kama
wana kesi nyingine.
Pia, kuna shida ya uadilifu kwa baadhi ya
watendaji. Hata hivyo, sisi Magereza tupo makini, askari akipatikana na
kosa la aina hiyo, sheria iko wazi anafukuzwa kazi.”
Uchunguzi huo uliohusisha wananchi wa kawaida na
watendaji wa kada mbalimbali ikiwamo wa Jeshi la Polisi, Magereza na
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) katika maeneo tofauti ya mikoa
hiyo, umethibitisha kuwapo kwa matukio hayo.
Rushwa, tamaa ya utajiri, kipato hafifu, kukosa
uaminifu pia ushirikiano miongoni mwa watendaji wa Serikali ikiwamo
wanasheria, waendesha mashitaka, polisi na magereza na kukua kwa
utandawazi vinatajwa kuwa miongoni mwa sababu za kukithiri uhalifu huo
katika mikoa hiyo.
Katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya watuhumiwa
hao walio mahabusu na katika magereza kwenye ukanda huo huwasiliana na
mtandao wao wa uhalifu ulio nje kwa barua, simu na njia nyingine.
Wahalifu hao kutumia mtandao wao ikiwamo jamaa zao
wanaowaagiza kupeleka rushwa kwa baadhi ya wasimamizi wa sheria ili
kufanikisha mikakati yao ya kutoka, kubadilishiwa mashtaka au kukata
rufaa zitakazowawezesha kupata dhamana na kuweka mkakati maalumu wa
kutoka gerezani.
Habari hizo zinapasha kuwa licha ya baadhi ya watuhumiwa
kukamatwa kwa uhalifu wa kukutwa na silaha, mauaji hata ujangili na
Kikosi Maalumu cha Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na askari polisi
katika kukabili wimbi hilo, baadhi ya wahusika ya hawajawahi kusomewa
mashtaka.
Hali hii mbaya zaidi katika mikoa yenye hifadhi za
taifa za wanyamapori ambako licha ya uhalifu, walinzi na watendaji
wengine wa maeneo hayo wanaishi kwa hofu kutokana na kutishiwa maisha na
wahalifu wanaowakamata na wengine wakieleza kunusurika kifo mara kadhaa
kutokana na kushambuliwa na wahalifu wanaoingia hifadhini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Itaendelea Kesho
Na Mwananchi
Itaendelea Kesho
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment