Ofisi ya Bunge la
Katiba itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji
kura kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge hilo
wanaokwenda Hijja.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo,
Yahya Khamis Hamad alipotakiwa kueleza idadi kamili ya wajumbe wa Bunge
hilo wanaotarajiwa kuwa nje ya nchi na jinsi watakavyopiga kura.
Juzi, Bunge hilo lilizifanyia marekebisho kanuni
zake ili kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo
wanaokwenda Hijja kuipigia kura Katiba inayopendekezwa, iliyokabidhiwa
kwa Kamati ya Uongozi jana.
Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya
Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au ya siri kwa njia ya fax au
mtandao kama itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na mwenyekiti.
Hamad alisema hadi kufikia jana mchana walikuwa
wamewatambua wajumbe wanane ambao watakwenda Hijja huko Uarabuni lakini
orodha ya watakaokuwa nchi nyingine bado haijajulikana.
Hamadi alisema ofisa wake huyo atasimamia kura za
wajumbe wanaokwenda Hijja katika upigaji kura unaotarajiwa kuanza
Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz