Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara, Emmanuel Mbasha. PICHA|MAKTABA
Mwimbaji wa
nyimbo za Injili na mfanyabiashara, Emmanuel Mbasha amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa mashtaka ya ubakaji. Mbasha ambaye pia ni mume mwa mwimbaji maarufu wa
Injili nchini, Flora Mbasha alipandishwa kizimbani jana na kusomewa
mashtaka mawili ya ubakaji.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai kuwa
mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Mei 23
na 25, mwaka huu, eneo la Tabata Kimanga, Ilala, Dar es Salaam.Wakili Katuga alidai kuwa katika tarehe hizo,
mshtakiwa alimbaka mtoto (jina linahifadhiwa), mwenye umri wa miaka 17,
kinyume cha sheria.
Hata hivyo, Wakili Katuga alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Ingawa dhamana ya mshtakiwa huyo ilikuwa wazi,
aliswekwa mahabusu, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana
ambayo yalikuwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja akiwa ni mfanyakazi wa
taasisi inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni
kila mmoja.
Hakimu Wilberforce Luhwago anayesikiliza kesi hiyo
aliiahirisha hadi kesho itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia iwapo
mshtakiwa amekamilisha masharti ya dhamana. Mbasha alifikishwa mahakamani hapo asubuhi akiwa
amevaa shati jekundu la mikono mirefu, suruali ya rangi ya udongo na
kandambili nyekundu.
Mahakamani hapo alikuwa ameambatana na wanaume wawili. Wakati akisubiri kupelekwa mahabusu, saa 7:35,
watu hao aliokuwa ameambatana nao walikwenda kumnunulia chakula na maji
kabla ya kuongozwa na polisi kwenda kupanda basi la Magereza kuungana na
mahabusu kuelekea Gereza la Keko saa 7:05. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz