Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa
Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake kutoka
Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao
makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na
Papa nje ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na
kiongozi wa Kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu
katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema
ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.