Na Clifford Majani, Mwananchi
Kwa miaka mingi sana binadamu wa karne zote wamekuwa wakitafuta siri za maisha marefu, kuzuia uzee na hata kuzuia kifo. Lakini pamoja na jitihada nyingi mambo haya
yameendelea kuwa changamoto kubwa kwenye maisha ya mwanadamu katika nchi
mbalimbali duniani. Kwa Tanzania, inakadiriwa kuwa umri wa kuishi kwa wanaume ni takriban miaka 58.2 na kwa wanawake ni miaka 60.5.
Muda huu wa kuishi ni mfupi sana ikilinganishwa na
wenzetu katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani ambako wastani wa
kuishi ni unakadiriwa kuwa ni miaka 78.2. Wanasayansi wamekuwa na nadharia nyingi kuhusu
sababu zinazosababisha binadamu azeeke na kufa mapema. Ila wengi
hufikiri kuwa tunazeeka mapema kutokana na sababu za maumbile na
vinasaba tunavyorithi kwa wazazi wetu.
Wengine husema kuwa tunazeeka haraka kutokana na kuwa na mtindo usiofaa wa maisha. Mtaalamu wa Afya, Dk Mark Stibich anasema kwamba
kuzeeka haraka na kuishi maishi mafupi ni suala mtambuka na linahusisha
mambo kama vile vinasaba, kemia, fiziolojia ya mwili pamoja na tabia zetu kwa mujibu wa makala yake ya Mei 10, 2014 liyowekwa kwenye tovuti ya longevity.about.com.
Mtaalamu wa maabara nchini Ujerumani, Dk James
Vaupel anadai kuwa vinasaba huchangia kasi ya kuzeeka kwa asilimia tatu
pekee na sehemu kubwa ya visababishi vya kuzeeka haraka hutokana na
mtindo wa maisha usiofaa pamoja na lishe duni. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz