Tuesday, December 10, 2013

ANGALIA PICHA ZA BIRTHDAY PARTY YA NICK MINAJ, BONGE LA KEKI...!!!


First lady wa label ya YMCMB Nicki Minaj amesherehekea birthday yake ya kutimiza miaka 31 na mafanikio ya kujivunia kwenye kazi yake ya muziki ambapo party ilifanyika huko L.A na Restaurant nzima ilibadilika rangi yake na kuwa ya pink maalum kwa ajili ya party ya Minaj ambayo ilihudhuriwa na Lil Twist, Safaree boyfriend wa Nicki Minaj na watu wengine.
nicki-minaj-birthday-5nicki-minaj-birthday-3

YAFAHAMU MAAJABU 10 YA MSIBA WA MANDELA...!!!

RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, mweusi wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi na kijeshi barani Afrika, alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani kwake jijini Johannesburg.
Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa mara ya kwanza katika historia, dunia nzima imesimama nyuma ya jemedari huyo, kila mmoja akionesha masikitiko yake. Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo pia yatavunja rekodi ya mazishi yote yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa uso wa dunia hapo Desemba 15 mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu kumi yanayoambatana na msiba huo.

AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO WA MAREKANI
AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa Marekani aliye madarakani na kumpeleka popote duniani. Lakini katika hali ya kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa na wake zao, kuandamana na Rais Barak Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo wa dunia.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 10, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.


Monday, December 09, 2013

JE, UNAJUA KUWA WOGA, AIBU HUPUNGUZA KUJIAMINI KATIKA MAPENZI...??!

https://www.facebook.com/jambotz

KARIBU mpendwa wa blog yetu ya Jambo Tz inayopendwa na wengi na kuwashukuru wote wanaotumia muda wao kutupongeza wengine kutukosoa ili kuiboresha blog yetu.


Vilevile wapo walio na matatizo wanaoomba msaada ambao nashukuru umewasaidia wengi. Kama ilivyo ada, umekaa mkao wa kula kutaka kujua leo nimekuja na mpya gani. Nasema hakuna jipya chini ya jua kwa sababu kitu mapenzi kilikuwapo tangu enzi ya mababu na hata hao waliyakuta tokea enzi ya Adamu na Eva.
Tumepata malalamiko mengi kutoka kwa wasomaji wetu waliolalamika juu ya matatizo wanayokumbana nayo katika kula chakula cha roho, wengi wanalalamika kuwa hawali chakula kilichokamilika.
Kwa mfano mtu anauliza; Mbona mpenzi wangu si mtaalam wa mambo flani?, wengine hudiriki kusema tangu waanze mapenzi na waume zao au wake zao hawajafurahia mapenzi na kushangaa kusikia mapenzi yakikukolea hukufanya upandishe mashetani na kumaliza maneno yote mdomoni au kumfanya mwanaume atoe ahadi ambazo hana hata uwezo nazo kwa kusema atakununulia ndege wakati hata baiskeli hana.

Yote hayo ni mtu kuguswa pale panapomfanya ajione yupo dunia nyingine na kujiona juu hayupo wala chini hayupo. Wao hujiuliza kulikoni wenzao wafaidi wao wasifaidi kwani wamekosa nini.

Swadakta swali zuri sana, kumekuwa na utamaduni wa watu wengi kuona aibu kuuliza jambo walisilolijua hasa katika mapenzi hii imepelekea watu kuwa wavivu kujifunza kwa kuona aibu kuuliza kitu wasichokijua kwa kuogopa kuitwa washamba.
Nani alikuambia wote wamezaliwa wanajua, usichokijua uliza usisubiri aibu ikukute kwa mpenzio, kuuliza nje au kutoa nje udhaifu wako. Siku zote wasiojua huwa wajanja sana ili kuficha udhaifu wao lakini unauficha udhaifu wako wakati lazima uingie kwenye gemu.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA MIAKA 52 YA UHURU DESEMBA 09, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.

MARAIS KUINGIA KWA KADI MAZISHI YA MANDELA...!!!



Qunu, nyumbani kwa Mandela 
TISHIO la vitendo vya kigaidi vinavyotokea kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani, vimeifanya Serikali ya Afrika Kusini, kutoa kadi kwa marais na viongozi watakaohudhuria mazishi ya baba wa taifa hilo, Nelson Mandela. Mandela aliyefariki Desemba 5, atazikwa Desemba 15 kijijini kwake Qunu, eneo alilolichagua kabla ya mauti yake. 
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya kimataifa, usalama katika miji ya Afrika Kusini, unatarajiwa kuimarishwa zaidi kuliko hata ule unaotumika kwa marais wa Marekani wanapofanya ziara kwenye mataifa mbalimbali.  
Taarifa hizo zinabainisha kutokana na idadi kubwa ya watu kuhudhuria mazishi hayo, utawala wa nchi hiyo umebuni mbinu hiyo ya utoaji kadi kwa watu watakaokuwa eneo la maziko wakiamini itasaidia kuimarisha ulinzi.  
Mazishi hayo yanatarajiwa kuvunja rekodi ambapo yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili.  
Ratiba ya kutoa heshma za mwisho yatangazwa Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Serikali ya Afrika Kusini, mwili wa Mandela utawekwa katika jengo la serikali kwa muda wa siku tatu, kutoa fursa kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi waliyempenda. Meya wa jiji la Cape Town, Patricia de Lille, alisema ibada ya kumuaga Mandela itafanyika Jumanne kwenye uwanja wa mpira mjini Johannesburg.  
Jana maelfu ya raia wa Afrika kusini kutoka matabaka yote na rika zote walishiriki katika ibada ya pamoja ya dini mbalimbali, ambayo ilifanyika mjini Cape Town mahali ambako Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuachiwa huru kutoka jela. 
Chanzo: TANZANIA DAIMA

Saturday, December 07, 2013

PICHA ZAIDI ZA MUONEKANO WA NDANI NA WA NJE WA BASI LIENDALO KASI


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK UPANDE WA KULIA



Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni. Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga



Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni.  Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 07, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.

HII HAPA RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA MADIBA

Rais Jacob Zuma ametangaza kwamba mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape.
Rais Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo.  Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
 Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinto na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki. 
 Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa  FNB  Desemba 10, 2013  jijini Johanesburg.
Mwili wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia  Desemba 11 hadi 13,   kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi
 Uwanja wa Taifa wa michezo wa Johannesburg ambako sala rasmi ya Kitaifa ya mazishi itafanyika  siku ya Jumapili ya Desemba 10, 2013
 Jengo la Union Buildinga ambapo mwili wake utawekwa kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013
Ulinzi mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake Qunu ambako atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Desemba 15, 2013.

Friday, December 06, 2013

HII NDIO SENTENSI YA KISWAHILI ALIYOIANDIKA NICK MINAJ INSTAGRAM KUHUSU KIFO CHA MZEE MANDELA


Kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kimewasikitisha watu wengi wakiwemo watu wa maarufu duniani kama rapper Nicki Minaj mwenye wafuasi zaidi ya milioni tatu na nusu kwenye instagram amevunja rekodi ya kuwa staa pekee wa dunia ambae ameandika yake ya moyoni na kuongezea maneno ya lugha ya Kiswahili.
1
2

HISTORIA YA KUSISIMUA YA NELSON MANDELA


JINA KAMILI: Nelson Rolihlahla Mandela
A.K.A: Mandela
MAJINA YA UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI: Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.
ASILI YAKE
Nelson Mandela, Mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini mwake, ni mtoto wa Chifu wa kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika mji mdogo wa Transkei.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 6, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.

MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA, TANZANIA KUOMBOLEZA SIKU TATU

Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.


Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!




Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"


Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.


Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.


Alikuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...