Monday, December 09, 2013

MARAIS KUINGIA KWA KADI MAZISHI YA MANDELA...!!!



Qunu, nyumbani kwa Mandela 
TISHIO la vitendo vya kigaidi vinavyotokea kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani, vimeifanya Serikali ya Afrika Kusini, kutoa kadi kwa marais na viongozi watakaohudhuria mazishi ya baba wa taifa hilo, Nelson Mandela. Mandela aliyefariki Desemba 5, atazikwa Desemba 15 kijijini kwake Qunu, eneo alilolichagua kabla ya mauti yake. 
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya kimataifa, usalama katika miji ya Afrika Kusini, unatarajiwa kuimarishwa zaidi kuliko hata ule unaotumika kwa marais wa Marekani wanapofanya ziara kwenye mataifa mbalimbali.  
Taarifa hizo zinabainisha kutokana na idadi kubwa ya watu kuhudhuria mazishi hayo, utawala wa nchi hiyo umebuni mbinu hiyo ya utoaji kadi kwa watu watakaokuwa eneo la maziko wakiamini itasaidia kuimarisha ulinzi.  
Mazishi hayo yanatarajiwa kuvunja rekodi ambapo yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili.  
Ratiba ya kutoa heshma za mwisho yatangazwa Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Serikali ya Afrika Kusini, mwili wa Mandela utawekwa katika jengo la serikali kwa muda wa siku tatu, kutoa fursa kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi waliyempenda. Meya wa jiji la Cape Town, Patricia de Lille, alisema ibada ya kumuaga Mandela itafanyika Jumanne kwenye uwanja wa mpira mjini Johannesburg.  
Jana maelfu ya raia wa Afrika kusini kutoka matabaka yote na rika zote walishiriki katika ibada ya pamoja ya dini mbalimbali, ambayo ilifanyika mjini Cape Town mahali ambako Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuachiwa huru kutoka jela. 
Chanzo: TANZANIA DAIMA

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...