Monday, December 09, 2013

JE, UNAJUA KUWA WOGA, AIBU HUPUNGUZA KUJIAMINI KATIKA MAPENZI...??!

https://www.facebook.com/jambotz

KARIBU mpendwa wa blog yetu ya Jambo Tz inayopendwa na wengi na kuwashukuru wote wanaotumia muda wao kutupongeza wengine kutukosoa ili kuiboresha blog yetu.


Vilevile wapo walio na matatizo wanaoomba msaada ambao nashukuru umewasaidia wengi. Kama ilivyo ada, umekaa mkao wa kula kutaka kujua leo nimekuja na mpya gani. Nasema hakuna jipya chini ya jua kwa sababu kitu mapenzi kilikuwapo tangu enzi ya mababu na hata hao waliyakuta tokea enzi ya Adamu na Eva.
Tumepata malalamiko mengi kutoka kwa wasomaji wetu waliolalamika juu ya matatizo wanayokumbana nayo katika kula chakula cha roho, wengi wanalalamika kuwa hawali chakula kilichokamilika.
Kwa mfano mtu anauliza; Mbona mpenzi wangu si mtaalam wa mambo flani?, wengine hudiriki kusema tangu waanze mapenzi na waume zao au wake zao hawajafurahia mapenzi na kushangaa kusikia mapenzi yakikukolea hukufanya upandishe mashetani na kumaliza maneno yote mdomoni au kumfanya mwanaume atoe ahadi ambazo hana hata uwezo nazo kwa kusema atakununulia ndege wakati hata baiskeli hana.

Yote hayo ni mtu kuguswa pale panapomfanya ajione yupo dunia nyingine na kujiona juu hayupo wala chini hayupo. Wao hujiuliza kulikoni wenzao wafaidi wao wasifaidi kwani wamekosa nini.

Swadakta swali zuri sana, kumekuwa na utamaduni wa watu wengi kuona aibu kuuliza jambo walisilolijua hasa katika mapenzi hii imepelekea watu kuwa wavivu kujifunza kwa kuona aibu kuuliza kitu wasichokijua kwa kuogopa kuitwa washamba.
Nani alikuambia wote wamezaliwa wanajua, usichokijua uliza usisubiri aibu ikukute kwa mpenzio, kuuliza nje au kutoa nje udhaifu wako. Siku zote wasiojua huwa wajanja sana ili kuficha udhaifu wao lakini unauficha udhaifu wako wakati lazima uingie kwenye gemu.

  Kwa kuwa aliyeuliza ni mwanamke, hata akielezwa bado utakuwa mzigo kwa kuwa hawezi kufanya vile kwanza ataogopa kukuelekeza mtindo flani au ufanye vipi ili kumridhisha kwa kujua ameupata nje na kulisaliti penzi lenu.-
* Jifunze kwanza kabisa kumuandaa mpenzio 
Hii humfanya mpenzi ashikwe na ashki ya mapenzi na mwili kuwa tayari kwa tendo. Hakikisha mpaka sehemu zake zimelainika na kutoa ute unaokuruhusu kumuingilia bila maumivu wala kuweka michubuko.
* Utajuaje mpenzi wako yupo tayari kama si muongeaji? 
Sikiliza sauti yake kama mihemo yake huwa kama mtu mwenye pumu hata mwili wake hulegea. Hapo ruksa kumuingilia. Lakini wanaume wengi wamekuwa wajanja wajanja kwa kuficha udhaifu wao katika uelewa katika mapenzi matokeo yake kila siku kushindwa kumridhisha mpenzi wake kimapenzi.
 

Kama nilivyokwisha kusema mwanzo kama hujui bora uulize kwa mtaalam wa masuala ya mapenzi kupitia mitandao ya kijamii na sehemu nyinginezo ili kuliokoa penzi lako.
Huenda unaweza lakini hofu iliyokujaa moyoni hukufanya ushindwe kujiamini. Kuuliza si ujinga na kukaa mkimpya si ujanja. 
Tafadhari like page ya Jambo Tz kwa kubofya hapa ili kupata mambo mazuri kila wakati na endelea kutembelea blog hii kila siku.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...