Tuesday, December 10, 2013
Monday, December 09, 2013
JE, UNAJUA KUWA WOGA, AIBU HUPUNGUZA KUJIAMINI KATIKA MAPENZI...??!
KARIBU mpendwa wa blog yetu ya Jambo Tz inayopendwa na wengi na kuwashukuru wote wanaotumia muda wao kutupongeza wengine kutukosoa ili kuiboresha blog yetu.
Vilevile
wapo walio na matatizo wanaoomba msaada ambao nashukuru umewasaidia wengi.
Kama ilivyo ada, umekaa mkao wa kula kutaka
kujua leo nimekuja na mpya gani. Nasema hakuna jipya chini ya jua kwa sababu
kitu mapenzi kilikuwapo tangu enzi ya mababu na hata hao waliyakuta tokea enzi
ya Adamu na Eva.
Tumepata malalamiko mengi kutoka kwa wasomaji wetu waliolalamika juu ya matatizo wanayokumbana nayo katika kula chakula cha roho, wengi wanalalamika kuwa hawali chakula kilichokamilika.
Kwa mfano mtu anauliza; Mbona mpenzi wangu si mtaalam wa mambo flani?, wengine hudiriki kusema tangu waanze mapenzi na waume zao au wake zao hawajafurahia mapenzi na kushangaa kusikia mapenzi yakikukolea hukufanya upandishe mashetani na kumaliza maneno yote mdomoni au kumfanya mwanaume atoe ahadi ambazo hana hata uwezo nazo kwa kusema atakununulia ndege wakati hata baiskeli hana.

Yote hayo ni
mtu kuguswa pale panapomfanya ajione yupo dunia nyingine na kujiona juu hayupo
wala chini hayupo. Wao hujiuliza kulikoni wenzao wafaidi wao wasifaidi kwani
wamekosa nini.
Swadakta
swali zuri sana,
kumekuwa na utamaduni wa watu wengi kuona aibu kuuliza jambo walisilolijua hasa
katika mapenzi hii imepelekea watu kuwa wavivu kujifunza kwa kuona aibu kuuliza
kitu wasichokijua kwa kuogopa kuitwa washamba.
Nani alikuambia wote wamezaliwa wanajua, usichokijua uliza usisubiri aibu ikukute kwa mpenzio, kuuliza nje au kutoa nje udhaifu wako. Siku zote wasiojua huwa wajanja sana ili kuficha udhaifu wao lakini unauficha udhaifu wako wakati lazima uingie kwenye gemu.

MARAIS KUINGIA KWA KADI MAZISHI YA MANDELA...!!!
Sunday, December 08, 2013
Saturday, December 07, 2013
PICHA ZAIDI ZA MUONEKANO WA NDANI NA WA NJE WA BASI LIENDALO KASI
HII HAPA RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA MADIBA
Rais
Jacob Zuma ametangaza kwamba mazishi ya Nelson
Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu,
katika jimbo la Eastern Cape.
Rais
Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera
zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku
ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya
maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari
msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata
dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinto
na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao
wamethibitisha kushiriki.
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
Mwili
wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia
Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa
kijijini Qunu kwa mazishi
Uwanja
wa Taifa wa michezo wa Johannesburg ambako sala rasmi ya Kitaifa ya
mazishi itafanyika siku ya Jumapili ya Desemba 10, 2013
Jengo la Union Buildinga ambapo mwili wake utawekwa kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013
Ulinzi
mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake Qunu ambako
atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Desemba 15, 2013.
Friday, December 06, 2013
HII NDIO SENTENSI YA KISWAHILI ALIYOIANDIKA NICK MINAJ INSTAGRAM KUHUSU KIFO CHA MZEE MANDELA
Kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kimewasikitisha watu wengi wakiwemo watu wa maarufu duniani kama rapper Nicki Minaj mwenye
wafuasi zaidi ya milioni tatu na nusu kwenye instagram amevunja rekodi ya kuwa
staa pekee wa dunia ambae ameandika yake ya moyoni na
kuongezea maneno ya lugha ya Kiswahili.
HISTORIA YA KUSISIMUA YA NELSON MANDELA
JINA KAMILI: Nelson Rolihlahla Mandela
A.K.A: Mandela
MAJINA YA UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI: Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.

ASILI YAKE
Nelson Mandela, Mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini mwake, ni mtoto wa Chifu wa kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika mji mdogo wa Transkei.

MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA, TANZANIA KUOMBOLEZA SIKU TATU
Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.
Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi
uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!
Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"
Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.
Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.
Alikuwa
akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake
ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.
Thursday, December 05, 2013
PAPA FRANCIS ADAIWA KUTOROKA VATICAN USIKU....!!!
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.
Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao
usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu
Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka
kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.
Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa
akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada
maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.
Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa
Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda
kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.
“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda
kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda
kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.
MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA DESEMBA 21
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro George Kavishe, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na
Mkurugezi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba wakioshela alama ya dole
baada ya kutangaza Simba na Yanga kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe
itakayochezwa Desemba 21 jijini Dar es salaam (Executive Solutions)
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya
Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi,
Desemba 21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe
amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI
MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE MATCH).
Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni
maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa
kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu
zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Subscribe to:
Posts (Atom)