Rais Kikwete alisema kuwa Serikali
haiwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa amani kwa sababu inajua wazi
kwamba nchi ikiingia kwenye mgawanyiko, mshikamano utavurugika na
shughuli za maendeleo zitasimama.
Wednesday, October 16, 2013
KUMBE SHOW ZA MAJUU SIO KAMA ZA BONGO! - OMMY DIMPOZ
Ommy alikuwa akiongea na kipindi cha Ampilifaya jana baada ya kurejea
kutoka nchini Marekani alikokuwa kwenye ziara ya wiki tatu.
“Naweza kusema hapa nyumbani tunalipwa hela nyingi kuliko tunavyopata
nje kwa msanii yeyote kwa asilimia kubwa. Inategemea pia unaenda kufanya
tamasha sehemu gani. Kwahiyo asilimia kubwa hela unatengeneza zaidi
nyumbani,”alisema Ommy.
Alisema hiyo ni kwasababu show za Tanzania huhudhuriwa na watu wengi
zaidi kuliko inavyokuwa nchi za nje ambako ni watu wachache sana huingia
japo kiingilio ni kikubwa na wengi wanaohudhuria ni watu waliotoka
Afrika Mashariki zaidi.
Katika hatua nyingine, leo Ommy Dimpoz kupitia Instagram, ameandika maneno ya shukrani kwa wote walioifanikisha show yake.
“AssaLaam ALeykum Ndugu zangu, Eid MubaraQ Ndugu, jamaa, Marafiki, and all
my Fans all over the world…Namshukuru Mungu Alhamdulilah nimerudi
nyumbani Salama Kuendelea na Majukumu mengine baada ya Tour ya Takriban
Mwezi Mmoja…Ningependa kuchukua Nafasi hii kuwashukuru
@Dmkglobal promotion na J&P kwa kufanikisha tour yangu ambayo imeweza
kuwa na Mafanikio makubwa Na kufanikisha baadhi ya malengo ambayo
mengine sikuyatarajia.Pia ningependa kuwashukuru watu wote ambao
walionyesha support kipindi chote cha tour yangu hususan Watanzania
wenzangu na Watu wa Africa Mashariki na Kati ambao walionyesha
Ushirikiano na support ya kutosha tangia mwanzo mpaka mwisho wa tour
yangu…Nachoweza kuwaahidi ni kuwa mengi mazuri Yanakuja na Naimani
sitawaangusha.Nawatakia mapumziko na sherehe njema za sikukuu ya
Idd…. Mimi na team nzima ya pozkwapoz tutakuwa DARLIVE tukitoa Huduma
Karibuni sana.LOVE U ALL.” na Vijimambo Blog
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA EID EL HAJ MSIKITI WA ANWAAR MSASANI, DAR ES SALAAM
Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao
katika Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa
Anwaar uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Ofisi ya
Makamu wa Rais
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na
Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani
jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Tuesday, October 15, 2013
WAPINZANI KUTINGA IKULU LEO ... MKUTANO MUHIMU WA JK, MBOWE, MBATIA NA PROFESA LIPUMBA LEO UTOE MAJIBU HAYA
Viongozi
wa vyama vikuu vya upinzani nchni kutoka kushoto: James Mbatia (NCCR
Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF).
Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani vyenye wabunge bungeni
wanatarajia kukutana leo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es
Salaam kuzungumzia utata wa baadhi ya masuala yaliyojitokeza katika
mchakato unaoendelea wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Kama wengi tunavyotegemea, mazungumzo hayo kwa vyovyote ni ya masuala nyeti ambayo yamesababisha mvutano na kuibua hisia kali miongoni mwa makundi ya kijamii, pengine kwa kutambua fika kwamba kupuuza madai ya wapinzani ingekuwa sawa na kumwaga petroli katika nyumba inayoungua, busara za rais wetu zimemfanya awaite viongozi wa kisiasa kuteta nao Ikulu.
Wakati viongozi hao, Freeman Mbowe wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi na Profesa Ibrahimu Lipumba wanakutana na kiongozi wa nchi leo, pengine akiwa hajasaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambao ulipelekwa mezani kwake baada ya kupitishwa bungeni na wabunge wa CCM wiki chache zilizopita, watampa mwanga kilichowafanya waugomee bungeni, maana katika hotuba yake alisema ameambiwa hiki na kile sasa atasikia laivu kutoka kwao.
KESI YA BABU SEYA NA PAPII KOCHA KUUNGURUMA OKTOBA 30
MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe.
Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.
KIKWETE: TUMESHINDA MAADUI ZETU
Rais Jakaya Kikwete amesema maadui
wote ambao walitaka kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kwa lengo
la kuvuruga amani ya nchi wamedhibitiwa .
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali
yake itaendelea kulinda amani ya nchi na maadui wote wanaohusika na
kutaka kuvuruga nchi watachukuliwa hatua kali za kisheria. "Kulikuwapo
na upepo mbaya, lakini kwa sasa Tanzania ni shwari na tumemshinda adui,"
alisema Rais Kikwete jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya
Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yaliyoandamana na sherehe
za kuzima Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.
Alisema katika siku za hivi karibuni,
maadui wasioitakia mema Tanzania walikuwa na mkakati wa kuvuruga amani
ya nchi, lakini Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola
vimewadhibiti na nchi iko salama.
RAILA ODINGA AELEZA NYERERE ALIVYOMSAIDIA KUSOMA NJE
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila
Odinga ameeleza kuwa bila ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada
na Mwalimu Julius Nyerere asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya
Idara ya Uhamiaji ya Kenya kumnyima hati hiyo ya kusafiria.
Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali.
Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.
Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali.
Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.
Hata hivyo, Mzee Jaramongi aliamua kusafiria hati ya kimataifa alizopewa na Kwame Nkurumah wa Ghana, pamoja na Gamel Abdel Nasser wa Misri.
Odinga alihitaji hati hiyo kwa kuwa baba yake alitaka amalizie masomo yake nchini Ujerumani baada ya kukatishwa masomo akiwa kidato cha pili mwaka 1962 katika Shule ya Maranda.
Katika kitabu hicho, Odinga alisema hakushangaa kunyimwa hati hiyo.
KLABU 7 ZATAWALA UBINGWA WA SOKA TANZANIA BARA
Na DANIEL MBEGA
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea
kutimua vumbi katika harakati za kutafuta bingwa katika mwaka wake wa 49
tangu harakati za kutafuta klabu bingwa zilipoanza mwaka 1965.
Mikiki mikiki yote hii isingekuwepo leo kama lisingekuwa wazo la kocha
wa Taifa Stars wa wakati huo, Milan
Celebic wa Yugoslavia, alilolitoa mwaka 1964 kama njia ya kusaidia
kuchagua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kutegemea michuano ya
Sunlight Cup (sasa Taifa Cup).
Badala ya michuano ya Sunlight
iliyohusisha klabu na timu za Majimbo, Celebic aliona kulikuwa na
umuhimu wa kuwepo mashindano ya klabu pekee katika ngazi ya taifa na
siyo yale ya mkoa, hasa wa Pwani (Dar es Salaam ya sasa), hivyo
'akaliuza' wazo lake kwa Chama cha Ligi ya Soka cha Dar es Salaam (DFLA)
ambao walianzisha mashindano hayo mwaka 1965 yakijulikana kama Ligi ya
Taifa.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TFA (TFF)
uliofanyika kati ya Desemba 19-20, 1964 (Jumamosi na Jumapili) katika
Ukumbi wa Arnautoglou mjini Dar es Salaam ndio uliojadili pamoja na
mambo mengine, uanzishwaji wa Ligi ya Taifa. Tembelea jambotz8.blogspot.com na kenypino.blogspot.com kila siku.
Monday, October 14, 2013
HAYA NI MAMBO 11 YALIYOPINGWA NA BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE
Ni miaka kumi na nne sasa imepita tangu mzee wetu mpendwa baba wa taifa hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere aiage dunia.
Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 22, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria .
Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 22, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria .
Alikuwa ni mototo wa chifu Burito
Nyerere wa kabila dogo la wazanaki
Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi [kwa saa za Afrika Mashariki], katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.
Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani.
Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi [kwa saa za Afrika Mashariki], katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.
Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani.
Mwalimu bado ni taa inayong’aa
gizani, umuhimu wake nazidi kuonekana kadiri miaka inavyokwenda licha ya
kwanza amekwisha tuacha.
Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere alichukia na kukemea vikali mambo yasiyofaa kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania , Afrika na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya mambo hayo ni:
Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere alichukia na kukemea vikali mambo yasiyofaa kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania , Afrika na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya mambo hayo ni:
1. UJINGA
Mwalimu Nyerere alikuwa ni miongoni mwa wasomi wachache na ni mtanzania
wa kwanza kupata nafasi yamasomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Edinburg ,
Uingereza na kuhitimu mwaka 1952 akiwa ni gwiji wa uchumi na historia.
Mwalimu hakupenda ujinga na hivyo alipigana vita kali dhidi ya ujinga,
na alifanikiwa kwa nafasi yake kuwaondoa ujinga watanzania wengi,
wakiwemo viongozi wetu wa sasa ambao walisomeshwa ‘bure’ katika
mazingira mazuri yakuridhisha kwa manufaa ya nchi yetu. Ndiyo maana Rais
Kikwete Februari 3, 2007 alisema “….sisi tuliwekezwa na ni lazima
tuwekeze kwenu ili miaka 30 ijayo Rais atoke miongoni mwenu….”
HIVI NDIVYO MKASA WA MWANDISHI WA ITV UFOO SARO ULIVYOKUWA
Mwandishi wa habari wa
ITV, aliyejeruhiwa kwa risasi jana asubuhi, alilazimika kuvumilia
majeraha ili kujiokoa yeye mwenyewe na wadogo zake watatu waliokuwa
wakipigwa risasi, baada ya mama yake mzazi, Anastazia Saro (58), kuuawa.
Mauaji hayo ya
kusikitisha, yalifanyika katika eneo la Mbezi Kibwerere, nyumbani kwa
mama yake Ufoo ambako alikuwa akiishi na wadogo zake Ufoo ambao ni
Goodluck, Innocent na Jonas.
Mtuhumiwa wa unyama huo
ametajwa kuwa ni Anthery Mushi, ambaye ni baba mtoto wa Ufoo, na siku ya
tukio wawili hao walitokea Mbezi Magari Saba nyumbani kwa Ufoo, kwenda
kuzungumza kifamilia na mama mzazi wa mwandishi huyo.
Mushi (40) ni Mhandisi wa
kitengo cha Mawasiliano katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini
Sudan na aliwasili nchini juzi na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Ufoo
Mbezi Mgari Saba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, Ufoo amejeruhiwa katika
paja na tumboni, mama yake mzazi alikufa papo hapo baada ya kupigwa
risasi ya kifuani na mtuhumiwa Mushi ambaye naye alijiua baada ya
kujipiga risasi kichwani katika eneo la kidevuni.
Walivyowasili nyumbani
Akizungumza na wavuti hii
jana mdogo wake Ufoo, Goodluck alisema; "Walikuja wakiwa pamoja (Ufoo
na Mushi) mapema alfajiri wakiwa ndani ya gari saa 12 kabla ya kuingia
ndani walitusalimia kisha wakaingia sebuleni na kuanza mazungumzo na
mama."
SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA KWA WALIMU
SERIKALI imesema, mwakani inatarajia kuajiri walimu wapya 27,000 wa
shule za msingi na sekondari nchi nzima. Taarifa hiyo ilitolewa jijini
hapa jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),
Kassim Majaliwa (pichani) alipokuwa akifunga mkutano wa wadau wa Mfuko wa Pensheni
wa LAPF.
Alisema kwamba kitendo cha kuajiriwa kwa walimu hao, kitatoa
fursa ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, kupata wanachama wengi na
hivyo kuendelea kuboresha shughuli na maisha ya waajiriwa wao.
“Mwakani tunatarajia kuajiri walimu wapatao 27,000 nchi nzima na hii itakuwa ni fursa nzuri kwa mifuko ya jamii kwani watajiunga katika mifuko ya jamii iliyopo,” alisema Majaliwa.
“Mwakani tunatarajia kuajiri walimu wapatao 27,000 nchi nzima na hii itakuwa ni fursa nzuri kwa mifuko ya jamii kwani watajiunga katika mifuko ya jamii iliyopo,” alisema Majaliwa.
ZITTO KABWE ATAJA MSHAHARA WA RAIS HADHARANI, ADAI NI ZAIDI YA MILIONI 380 KWA MWAKA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto
Kabwe, ametaja mshahara anaolipwa Rais Jakaya Kikwete. Amesema kwamba
kwa wadhifa alionao, Rais Kikwete analipwa zaidi ya Sh milioni 30 kwa
mwezi.
Mbali na mshahara huo, Zitto amesema kiongozi huyo wa nchi, analipwa
wastani wa zaidi ya Sh milioni 380 kwa mwaka ambazo ni marupurupu
pamoja na mshahara wake.
Zitto aliutaja mshahara huo mjini hapa jana, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa Zitto, hakuna sababu kwa mshahara wa kiongozi kufanywa siri kwa kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaolipa kodi inayolipa mishahara ya viongozi.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ametaja mshahara huo ikiwa ni wiki moja baada ya kutaja mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alisema analipwa zaidi ya Sh milioni 20 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi
Zitto aliutaja mshahara huo mjini hapa jana, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa Zitto, hakuna sababu kwa mshahara wa kiongozi kufanywa siri kwa kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaolipa kodi inayolipa mishahara ya viongozi.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ametaja mshahara huo ikiwa ni wiki moja baada ya kutaja mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alisema analipwa zaidi ya Sh milioni 20 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi
Subscribe to:
Posts (Atom)