Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipata kusema; “ Tatizo kubwa kwa nchi za Afrika si nakisi kwenye bajeti zao, bali, nakisi ya IMANI”.
Na Profesa Gaudence Mpangala naye amepata kusema; “ Msingi wa matatizo yetu mengi ni uwepo wa mfumo wa Chama Dola.”
Na kwangu mimi, changamoto kubwa kwa Katiba yetu ijayo ni kuona kama itatoa nafuu ya hayo mawili hapo juu.
Maana, haiyumkini tukafanikiwa kujenga taifa la kisasa kama
Jakaya Kikwete ameonyesha kuwa mfano wa kiongozi mwenye ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni na taratibu za kijima. Swali, ni wangapi wengine kwenye mfumo anaoutumikia wenye mitazamo kama ya kwake? Maana, maamuzi mengine ya kimageuzi anayoyafanya Kikwete yasingeweza kufikiriwa miaka kumi iliyopita.
Jana Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Jaji Francis Mutungi kushika nafasi ya John Tendwa kama Msajili wa Vyama. Ukweli unabaki, kuwa kwenye utendaji wake, Tendwa kama mlezi hakuaminika na baadhi ya aliowalea. Hilo ni pungufu kubwa na linakwaza juhudi za kukuza demokrasia ya nchi. Msajili wa vyama vya siasa anapaswa aonekane kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa na wala si mwonezi wa vyama vya siasa. Na kazi ya ulezi inatakiwa ionekane.